Nina msongo mkali wa mawazo uliosababishwa na wanawake nimekata tamaa kabisa

jjs2017

JF-Expert Member
May 25, 2019
2,023
4,213
Kila nikijaribu kukataa wanawake siwezi. Napata msongo mkali sana wa mawazo wanawake wame nitibua hata ladha ya mapenzi siijui tena .

Nahitaji matibabu ya kiakili,kifikra, dawa au sindano kama zipo ili nafsi yangu na moyo wangu utulie.

Mimi nimejitahidi sana kunywa pombe kali, kushinda bar ila nimeshindwa na nikiwa njiani nikiona gari natamani nijirushe humo ni gongwe wakati mwingine nikiwa katika floor za juu kabisa za magorofa marefu moyo unaniambia ni jirushe chini.

Nimeomba sasa nimechoka ndugu zangu . Niombeeni ni baki baki angalau maana naona sasa na teketea kabisa kabisa.

Pia aliyeteyari kua company yangu na mkaribisha. Awe ananipigisha story na kunipa mawaidha mpaka nikae sawa..
 
Pole wote tunapitia magumu Mi leo kidogo nimsamehe Ex-G kaniambia anataka kuja nyumbani mimi nikajibu bila kufikiria na nikamruhusu aje ila kabla hajaja kuna kitu moyoni kikawa kinaniambia kwanini umemruhusu mtu ambae hastahili kusamehewa?
Nikaanza kuomba Mungu bora asije na aniepushe nae kama huyo mwanamke ni shari kwangu nashukuru Mungu imeshuka mvua kubwa hadi ameshindwa kuja

Sitamruhusu tena , mi nachokushauri bro jipende mwenyewe furaha yako isimtegemee mtu mwingine kuna muda inabidi tuwe na maamuzi magumu kukubaliana na hali hata kama maamuzi yanatuumiza.
Mfute huyo mwanamke kwenye maisha yako futa namba, badilisha njia, futa picha zake, Acha kumsearch kwenye media, epuka maongezi ambayo yatakua yanamuhusisha jina lake.

Utamsahau taratibu.
 
PATA BWANA MKUU.
Sasa kama wanawake wamekushinda dawa ni wewe uwe mwanamke tu.
 
Pole sana mkuu, ngoja nimeze konyagi nikusanye akili nitarudi kukushauri...😊
Okay.........

Angalia kitu yenye unapenda sana then jikite kuifanya ili uifurahishe nafsi yako (kama sio hatarishi), na hiyo ndio itakua dawa yako na utapona kabisa.

Kwasasa nakushauri uachane na pombe kabisa maana tutakupoteza ikiwa hauna uwezo wa kujizuwia.
Anza kujifunza michezo na chagua mchezo ambao utakua unakufanya upate uchovu wa mwili, hata aina ya mazoezi ili uweze kulala vizuri usiku.

Lakini pia naomba nikukumbushe kwamba.... mwanaume ili amu win mwanamke basi ni lazima aishi nae kwa akili (yaani mwanaume amzidi mwanamke akili). Na ukiona hauwezi kuishi na wanawake basi jiweke kwenye kundi la wanaume wanao zidiwa akili na wanawake na kisha wanakutawala.

By the way...... mapenzi/mahusiano is not for everyone, ndio maana kuna madanguro ya nyabe za kupima.
 
Pole kwa changamoto unayopitia Mkuu.

Ukiona hadi unatamani kujiua kisa Mapenzi basi utakuwa hujakishirikisha kichwa chako ipasavyo.

Umewahi kujiuliza hawa mabinti waliomaliza kidato cha 4 juzi wataolewa na nani iwapo utajiua.

Bado kuna Warembo wengi Nchi hii, iweje ukubali Mwanamke mmoja akuchezee maisha yako.

Hata hivyo bado una nafasi ya kumshirikisha Mungu suala lako ili alipatie ufumbuzi wa kudumu.

Kumbuka kusoma kitabu cha Yeremia 33:3 kinachosema "Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua."

Mungu yupo hapo kutusaidia magumu yetu.
 
Pole sana , kikubwa kubali maomivu ya vae na uyaoge , kaza moyo jikaze kweli na huo ndiyo uanaume ukiona nafsi na moyo unapasuka kwa uchungu nenda bafuni jifungie huko maana ni haramu mwanaume kutoa machozi hadharani chukua maji jimwagie alafu lia sana ukimaliza oga , vaa vizuri nenda kajichanganye na watu.
 
jjs2017 kuna nguruwe mwenzio DungaMawe nae anataka kujiua kama wewe tu.

Kila nikijaribu kukataa wanawake siwezi. Napata msongo mkali sana wa mawazo wanawake wame nitibua hata ladha ya mapenzi siijui tena .

Nahitaji matibabu ya kiakili,kifikra, dawa au sindano kama zipo ili nafsi yangu na moyo wangu utulie.

Mimi nimejitahidi sana kunywa pombe kali, kushinda bar ila nimeshindwa na nikiwa njiani nikiona gari natamani nijirushe humo ni gongwe wakati mwingine nikiwa katika floor za juu kabisa za magorofa marefu moyo unaniambia ni jirushe chini.

Nimeomba sasa nimechoka ndugu zangu . Niombeeni ni baki baki angalau maana naona sasa na teketea kabisa kabisa.

Pia aliyeteyari kua company yangu na mkaribisha. Awe ananipigisha story na kunipa mawaidha mpaka nikae sawa..

Acha ujinga tafuta hela
 
Pole wote tunapitia magumu Mi leo kidogo nimsamehe Ex-G kaniambia anataka kuja nyumbani mimi nikajibu bila kufikiria na nikamruhusu aje ila kabla hajaja kuna kitu moyoni kikawa kinaniambia kwanini umemruhusu mtu ambae hastahili kusamehewa?
Nikaanza kuomba Mungu bora asije na aniepushe nae kama huyo mwanamke ni shari kwangu nashukuru Mungu imeshuka mvua kubwa hadi ameshindwa kuja

Sitamruhusu tena , mi nachokushauri bro jipende mwenyewe furaha yako isimtegemee mtu mwingine kuna muda inabidi tuwe na maamuzi magumu kukubaliana na hali hata kama maamuzi yanatuumiza.
Mfute huyo mwanamke kwenye maisha yako futa namba, badilisha njia, futa picha zake, Acha kumsearch kwenye media, epuka maongezi ambayo yatakua yanamuhusisha jina lake.

Utamsahau taratibu.
Hii njia nilijaribu nikashindwa

Bado naumia aisee
 
Back
Top Bottom