is it so very important?
jamani mimba miezi 9,imagine na hiyo miguu inavokua kweli uwe safarini hata siku tatu kisa tu wazazi wamesema? AshaDii i beg to differ with yu samahani mamii!
kwa kweli hili la huyu dada ni zaidi ya kwenda kujifungua ukweni!
sijui labda mie mimba zangu zinakuwa tofauti lakini kama ndo anakuwa na tumbo la kukata kona kama langu linavokuwa i see siendi kokote!
yaah!nakuelewa mamiiSnowhite... unaweza kuwa sawa... Majibu yangu yamezingatia haya:-
- Tumetofautiana makabila... Kuna makabila ni marufuku kutoa mimba ama kuzaa mtoto wa kwanza nje ya nyumbani kwao. Nina mfano hai, binamu yangu aliolewa (mume wake alifariki may he rest in peace); mume wake alimwambia akazalie kwao... Binamu yangu ni mbishi... aligoma. Mimba ilipitiliza miezi 10 anaumwa uchungu anapona but hazai... Mashangazi wakachekecha wakaingilia kati na kumbwambia binamu aende kijijini. Of course alipofika tu kituoni uchungu ulimuanza na alipoingia tu ndani mule alizaa pale pale! Ki science tunaweza sema safari ilikuwa ndefu saana akachoka na ndio maana akazaa... Ki imani tunaweza sema upande wa kiume walimfunga kutozaa... Lipi ni kweli? Mimi na wewe hatujui.
- Lingine la msingi ni kuwa mshewa2 kaliwasilisha hapa tatizo lake... BUT yeye ndie anamface mume wake. Hatujui the nature ya mume wake ipo vipi. Inaweza kuwa moja ya wale wanaume ambao sio waelewa, kama kaamua ndio hilo hilo. Nimeona nikishikilia kwua dada akatae maamuzi ya mumewe SIO mumewe anaeteseka... Mshewa ndio anateseka zaidi. Akikubaliana katika nafsi yake kuwa anaweza enda itamfanya arudi hali nzuri na mood nzuri... Najua for personally nikiwa mjamzito SIPENDI wala SITAKI maudhi... Badala ya kumpa hiyo vita ya kupigana (kimaneno na mumewe) basi aangalie unafuu wa kuweza kubaliana na hilo.
- Mleta mada kisha onesha upande wake na ni wazi kuwa HATAKI! Nam support... BUT kutazama reality ni muhimu pia. Kuwa anaweza asitake lakini apende asipende lazima aende. Kama umenisoma vema nimempa options mbili... Aidha aende ma muuguzi AMA aombe mtu mzima kuwakilisha kuwa asubiri kujifungua.
Asante sana kwa ushauri wako ntaufanyia kazi,mshewa2, Hongera saana kuwa kukaribia kuwa mama na kwa kubeba ujauzito hadi hapo ulipofikia.
Haya mambo ni mtihani saana. Hii inakuonesha kuwa ndoa sio ya watu wawili ni zaidi ya hapo. Naamini kuwa hadi umelileta hapa umejaribu kwa kila namna kumsomesha na kumuelewesha mumeo na hajakuelewa Pole saana. Kwa condition ya uja uzito uliyo nayo bahati mbaya ama nzuri una emotions zaidi ya siku zote Ila nakuomba vuta subira, jitahidi rudisha moyo na akili yako chini na uliangalie upya.
Kwa mtazamo wangu ni kuwa mumeo hakuwa na shida wewe kujifungulia ulipo sasa (yaani nyumbani kwenu); itakuwa nyumbani kwa wakwe zako wamesikia kuwa karibu unajifungua wakati wowote na wamemsisitiza mumeo kuwa ukazalie nyumbani kwao. Yeye kuomba hilo sio mbaya; mbaya ni kuwa hakukuarifu mapema kwani ilitakiwa uende hata mwezi mmoja kabla.
Nashauri ukubaliane nae Sababu kujifungua huyo mtoto na hali wazazi wana vinyongo haitapendeza. Kama nilivyosema ni mtihani mkubwa aidha mwambie mumeo akubali kukodi mtu wa afya ya uzazi muambatane naye safari hadi nyumbani - USITHUBUTU kukubali mkawa wawili tu. AMA omba mtu mzima yeyote ambaye ni upande wa mumeo na ni karibu na familia ya upande wa mumeo na ueleze hali halisi Na umuombe akufikishie hizo salamu kwa wakwe ukiahidi kuwa baada tu ya kujifungua salama utaenda huko nyumbani baada ya siku saba.
Hai mati kitu gani utachagua najua kwua lolote lile litakuumiza sababu mumeo hajatanguliza welfare yako na mtoto. Ila ndio hivo, hapa ni mwanzo taratibu mtasomana na kujuana na kujifunza namna ya kuchukuliana. Kila la kheri Na Mwenyezi Mungu muweza akuwekee wepesi katika ujauzito hadi kujifungua. Pamoja Saana.
Asante sana kwa ushauri wako ntaufanyia kazi,
Habari Wana JF
Mimi Nina mimba ya Miezi 9 nimebakisha week mbili nijifungue ila mume wangu analazimishia niende nikajifungulie huko kwao kanda ya ziwa, I thought of flying ila flights haziruhusu mtu wa type yangu kupanda ndege,so anasema tutaenda na gari taratibu hadi tufike even if it take us 3 days, Hospital nimeambiwa nisisafiri coz niko karibia kujifungua,he doesnt want to understand he think I'm jus making it coz I'm a medical personel 2, Hataki hata twende kwa specialist wote,wala hajawahi kwenda na mimi clinic,its our first born ,
Nifanyeje?nisafiri tu. kuwaridhisha ila its risk...anataka tusafiri 20th my due date ni 28th
kama alikuambia mapema nawe ukadharau huna ujanja kodini tu huyo wa afya tena mkunga mtu muende hata wiki asemayo mmeo njiani maana mambo ya wakwe tena kwenye ndoa ni balaa,
usipuuze kutokwendaz unles wakwe wameridhjia baada ya kuongea nao hasara za wewe kusafiri na hali yako,
na wakigoma pia nenda na uwe umeclear all posible risk kama kusafiri na huyo mtu atakyetoa msaada kiafya anything can hapen njiani