Nina miaka 42 ana miaka 18 anang'ang'ania nimuoe. Mimi namuona mdogo mno kuwa mke, nahisi atanisumbua

eity 4

Senior Member
Dec 7, 2014
147
206
Mimi kwa sasa naishi mwenyewe baada ya kuzinguana na wife na kila mtu ku-move on. Baada ya muda nikaingia kwenye mahusiano na binti ana miaka 18, mimi yangu 42.

Nampenda na anaonyesha ananipenda. Juzijuzi kagoma kwenda chuo alikotakiwa kwenda kisa hataki kuwa mbali na mimi katafuta chuo hapahapa mjini tunapoishi.

Sasa kaja na hoja anataka kuhama kwao akae na mimi kama mke wangu. Kifupi anataka nimuoe. Mi namwambia wewe bado mdogo kuwa mke na pili tofauti yetu kiumri sioni kama ni sahihi kwake kuolewa na mimi. Kakomaa anasema anajua tofauti yetu na alishaambiwa na watu wengi ikiwemo wazazi wake kuwa mimi mkubwa sana kwake lakini haya ni maamuzi yake, amejiridhisha kabla ya kuamua.

Je, ni sahihi kwa mimi kumuoa? Sitajuta baadae? Tofauti ya umri haiwezi kuwa shida baadae?

Msaada.
 
Kuna mwenzio(Ni marehemu sasahivi) alikuwa na umri Kama Wako na Akaoa Binti mdogo Kama huyo Wako kilichofuata aliambulia kupondwa tofari la kichwani tu kisa wivu wa kimapenzi. So take care mkuu wangu inaonekana mnafanana kila kitu na marehemu na unakoelekea na wewe Ni huku kwa mwenzio usipo change
scv20200119_111820.jpeg
 
Kwanini usitulie na mkeo kujipanga na maisha ya baadae..maana uzee una approach, hafu wewe ndio kwanza unaomba ushauri juu ya binti mwenye 18 anakupelekesha. Wakati ni kama mwanao
 
Back
Top Bottom