Wakuu,
Haya ni maoni binafsi na yanaongozwa na hisia za ndani nisizoweza kuzi-control bali kuzishirikisha kwenu nanyi mtazame;
Kutokana na kasi ya Upinzani kushamiri bila kuchoka tangu Mwaka 2005, ambayo ilisababisha CCM kupata mtikisiko mkubwa na kukaribia kuachia madaraka kwenye Uchaguzi mkuu wa 2010, katu haiwezekani wakawa wame-relax na kurudia makosa..
Ninachojaribu kusema, vuguvugu na nguvu ya upinzani katika Bunge la 10, Muungano wa vyama vya Upinzani vyenye nguvu miaka michache baada ya uchaguzi mkuu wa 2010, Uenezi usio na shaka Upinzani kwenye majimbo mengi zaidi nchini na mikakati imara ya kisiasa waliiyonayo Upinzani , CCM haiweze kurelax na kurudia makosa...
Imetengenezwa Sinema, ya kutuaminisha kwamba Mheshimiwa Lowassa, one of the prominent political figures from CCM, is no more 'wanted' in the Party despite nguvu kubwa ya ushawishi aliyonayo ndani na hata nje ya chama.. CCM haitaki tena kurelax na kurudia makosa..
This to me feels like a bail ambayo wapinzani wameshindwa kuing'amua na mpaka sasa wanacheza ngoma ya Chama tawala, ambacho kimekoma kurelax na kurudia makosa..
Hisia zangu zinachagizwa na Matamshi ya katibu wa Uenezi na hata Mwenyekiti wa CCM - Taifa, kwamba CCM itashinda hata kwa 'Goli la Mkono'.
Bahati mbaya, tafsiri ya Goli la mkono mpaka sasa wengi wameiona kama 'wizi wa kura', lakini kwangu ni zaidi ya hivyo; Safari hii naamini inatumika njia ya ku-win trust ya wapinzani kwa mtu wao (pandikizi), kupitia movie iliyotungwa na kuanza kutekelezwa kwa muda mrefu nao CCM - Hili ndio Goli la Mkono haswaaa!
Hisia zangu zisipuuzwe!