Huyu mtani wangu WEREMA sijui kama aliwahi kuhukumu hata kesi moja, na kama aliwahi basi ni mtata sana.
Jana anaonyesha saa yake OMEGA kuwa kama ni feki ni yake, lakini hoja iliyokuwa mbele ya bunge ni kuwa na sheria inayodhibiti mianya ya kuleta bidhaa feki kwa ajili ya matumizi ya mtu.
Amekuwa tofauti na Wasomi, anasema ipite tu, akaambiwa mtu ataleta vifaa vya umeme feki kwa ajili ya nyumba ikipangishwa wakati pakitokea shoti ya umeme watu watadhulika na mali zaolakini yakaingia kushoto yakatokea kulia.
Baya zaidi hawa wabunge walio wengi sijui ni wa chama gani wakasema NDIYOOOOOOOOOOOOOOOO, maana wao wanajiwakilisha si miongoni mwa wananchi waliowapeleka hapo, kwakweli jana nilihuzunuka sana kwa sheria kuruhusu bidhaa feki kuinguzwa nchini.
Mwana JF kweli hilo limetia shaka kwa mtani wangu huyu anayeona saa yake kama ndicho kigezo cha kuonyesha uanasheria wake.