Nina mashaka na UZALENDO wa Mwanasheria mkuu wa SERIKALI

Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
14,401
7,307
Huyu jamaa kila siku anapenda kutetea maslai ya wanao Watesa watanzania

1.Kipindi wanapitisha sheria ya manunuzi Bungen,Mnyika anasema iwekwe azabu kali kwa wale watao kiuka sheria hiyo,yeye akawa anasema hapana si vizuri,juzi sheria ya pesa chafu,na jana kuhusu bidhaa za feki
 
jamaa si mtanzania, ni ndugu zake raila odinga wa kenya. huoni wanafanana? anajua kenya watakuja kufanya kufuru hapa kwetu
 
Mimi nimesha-assign NILL kwa huyu jamaa toka enzi za mwanzo wa harakati za mchakato wa katiba mpya, baada ya yeye kutoa tamko ktk vyombo vya habari kwamba "HAONI HAJA YA KUWA NA KATIBA MPYA SABABU ILIYOPO INATOSHA KABISA". Sijui Kikwete anawatoa wapi hawa watu? Werema ni janga la kitaifa, bendera inayoongozwa na muelekeo wa upepo
 
Tatizo la hawa jamaa wa magamba ni kwamba ukiwaambia kitu ambayo itaelekea kuwabana wao na mizungukoi yao ya chapaa wanakuwa mbogo bora uingilie familia zao kuliko mzunguko wao wa chapaa wanachosha sana
 
naunga mkono hoja. naongeza kuwa nina mashaka na uwezo wake kiakili na kielimu. sidhani kama ana uwezo wa kujenga hoja yoyote dhidi ya mwajiri wake pale aonapo si muafaka na akaitetea kama mtaalamu wa sheria. nna mashaka nae siku nyingi sana tangu alipoanza kubwabwaja juu ya mchakato wa katiba mpya. with respect lkn alionekana kama hayawani!
 
Embu ukitaka kuona kichekesho itoke sheria ya kuzuia mikutano ya kisiasa kabla ya uchaguzi utapenda wajamaa wa magamba watakavyoshangilia na kurukaruka coz kwao kukutana na wananchi kuzungumzia maendelo ya jimbo ni mwiko ndio maana wengi wao huama majimboni mwao na kukimbiala Dar ili hata kero za jimboni siziwakwaze.
 
Huy jamaa hata mimi namashaka na weledi wake. Jana niliona jinsi alivyokuwa anajibu hoja zilizotolewa na Mhe. John Mnyika wakati Bunge lilipokuwa linapitisha mswada wa mabadiliko wa sheria mbalimbali za biashara. Hoja zote mbil za mnyika zilikwa na mantiki kabisa lakini yeye alikubaliana na moja tena kwa shingo upande sana. Ningemshauri yeye kama mtaalamu asiwe conservative kwamba kila mswada utakao letwa bungeni lazima upitishwe bila kubadilishwa wao sio malaika wanaweza wakawa wamechemsha na wameiburuza kabineti kupitisha mswada upelekwe bungeni so ukipingwa anaona soo kwamba hakushauri vizuri kabineti. Kusema kweli jamaa huyo anatuandalia miswada mibovu na ya kishenzi na inapitishwa tu kutokana na wingi wa wabunge wa ccm ambao wengi wao hawana muda wa kuisoma miswada kwa undani na kuichambua wakati wa kupitisha wenyewe wanakuwa wanasubiri kupitisha tu huo mswada kwa kuli ya ndiyooooo na kugonga meza.
 
Kama watu wamepata nafasi na kuanza kuwatetea waharifu, wanyang'anyi na wazandiki wa nchi hii basi tusubiri kufanya maamuzi kwa kutumia nguvu ya umma. Wote watakimbia nchi
 
Huyu jamaa kila siku anapenda kutetea maslai ya wanao Watesa watanzania
1.Kipindi wanapitisha sheria ya manunuzi Bungen,Mnyika anasema iwekwe azabu kali kwa wale watao kiuka sheria hiyo,yeye akawa anasema hapana si vizuri,juzi sheria ya pesa chafu,na jana kuhusu bidhaa za feki

Ondoa mashaka kaka jamaa ni MTZ sema ndo kulewa na madaraka!
chukua LIKE
 
Huyu mtani wangu WEREMA sijui kama aliwahi kuhukumu hata kesi moja, na kama aliwahi basi ni mtata sana.
Jana anaonyesha saa yake OMEGA kuwa kama ni feki ni yake, lakini hoja iliyokuwa mbele ya bunge ni kuwa na sheria inayodhibiti mianya ya kuleta bidhaa feki kwa ajili ya matumizi ya mtu.
Amekuwa tofauti na Wasomi, anasema ipite tu, akaambiwa mtu ataleta vifaa vya umeme feki kwa ajili ya nyumba ikipangishwa wakati pakitokea shoti ya umeme watu watadhulika na mali zaolakini yakaingia kushoto yakatokea kulia.
Baya zaidi hawa wabunge walio wengi sijui ni wa chama gani wakasema NDIYOOOOOOOOOOOOOOOO, maana wao wanajiwakilisha si miongoni mwa wananchi waliowapeleka hapo, kwakweli jana nilihuzunuka sana kwa sheria kuruhusu bidhaa feki kuinguzwa nchini.
Mwana JF kweli hilo limetia shaka kwa mtani wangu huyu anayeona saa yake kama ndicho kigezo cha kuonyesha uanasheria wake.
 
Sijasoma sheria ya darasan(makaratasi)lakin huyu mzee ana tofauti na yule aliyestaafu MWANYIKA alisema hivi ishu ya RICHMOND yeya siku watu wanatia sain,alikua kama shahid kuona ila hausiki
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom