Naomba ushauri juu ya afya yangu

namba moja tuu

Senior Member
May 4, 2017
162
142
Ni takribani wiki sasa inapita napatwa na dalili hizi
1. Muwasho sehemu za siri kwenye uume na pumbu zinapata zinapata vipele flani havijai maji ila nikivikuna vitamu sana nasikia raha sana mpaka natoka michubuko.
2. Muwasho matakoni karibia na msingi najikuna sana mpaka matako yamechubuka.
3. Muwasho baadhi ya sehemu za mwili sehemu hizi nikijikuna nasikia raha pia ila zinatengeneza wekundu kama damu kuivilia au nimetembelewa na mdudu.

Historia kimatibabu.
Nimepima magonjwa ya zinaa, HIV vyote sina nikatumia dawa BBE ya kupaka ya ukurutu ilipungua kiasi ila muwasho uliobaki ndo kama huo nilioeleza hapo juu naombeni msaada wenu wana jamvi madaktari najikuna mpako uume unachumbuka.

Nawasilisha kutoka kwa mdau.
 
Ni takribani wiki sasa inapita napatwa na dalili hizi 1: muwasho sehem za siri kwenye uume na pumbu zinapata zinapata vipele flani havijai maji ila nikivikuna vitamu sana nasikia raha sana mpaka natoka michubuko
2:muwasho matakoni karibia na msingi najikuna sana mpaka matako yamechubuka
3:muwasho baadhi ya sehem za mwili sehem hizi nikijikuna nasikia raha pia ila zinatengeneza wekundu kama damu kuivilia au nimetembelewa na mdudu

Historia kimatibabu
Nimepima magonjwa ya zinaa,HIV vyote sina nikatumia dawa BBE ya kupaka ya ukurutu ilipungua kiasi ila muwasho uliobaki ndo kama huo nilioeleza hapo juu naombeni msaada wenu wana jamvi madaktari najikuna mpako uume unachumbuka
Nawasilisha kutoka kwa mdau
Mkuu pole kwa hayo maradhi yako kama umepima maradhi ya zinaa huna basi huenda una Allergies ulisha wahi kupima hiyo Allergies? naje umesha wahi kupima mkojo wako?

Ninahisi Damu yako chafu ndio inayo kusababisha upatwe na kuwashwa sehemu zako za siri. au itakuwa sababu ya fangasi ndio pia wanasababisha upatwe na kuwashwa. Ngojea ushauri wa watu wengine watakao kupa usipo kusaidia nitafute mimi kwa wakati wako ili niweze kukutibia maradhi yako upate kupona uguwa pole.
 
Njia za kuepuka kuwashwa
Wanaume wanapaswa kufuata hatua mbalimbali ili kuepuka kuwashwa sehemu za siri. Miongoni ni kuosha vizuri uume na kwa wale ambao hawajatahiriwa wanapaswa kuosha kwa umakini zaidi hadi sehemu za ndani za govi.
Namna nyingine ni kuweka sehemu za siri katika hali ya usafi na ukavu, kwa maana unyevunyevu unaweza kusababisha maambukizi. Matumizi ya poda yanaruhusiwa hasa kipindi cha joto kali.

Vaa nguo isiyobana sana, iliyotengenezwa kwa vitu asilia kama pamba. Badili nguo ya ndani angalau kila siku na vaa kondomu kila unapofanya ngono na mwanamke usiyejua hali yake kiafya
 
Hapo ni kuwa msafi tu, Vaa boxer mara moja, fua na hakikisha inakauga vizuri! Kuna powder ambazo ni medicated unaweza kupaka pia.

Ila hapa naona Usafi unahusika sana sana
 
Back
Top Bottom