Nina imani na Jeshi la Polisi lakini...

Nina imani na Jeshi la Polisi lakini...

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,512
Reaction score
870,041
Siwezi kulikosea heshima hili jeshi ambalo ni chombo muhimu cha usalama wa raia... Kuna mapungufu mengi lakini bado lina nafasi kwenye jamii yetu kulingana na majukumu yake

Rai yangu kwa viongozi wa hiki chombo muhimu wabadilike wabaki na taaluma yao.. Wabaki na weledi wao uliotukuka.. Wajiepushe kutumika vibaya na wanasiasa wenye malengo na agenda z a siri.. Mambo yanapoharibika lawama fedheha kashfa na matusi huwaendea wao.. Huku waliowatumia wakiwa kimya na wasiojinesha... Ni sawa na shetani anakutumia kikinuka anakuacha unaaibika....!!!
Sakata la Kijana wetu Nondo linazidi kulichafua na kuliabisha jeshi letu adhimu... INAUMA SANA.. Mikanganyiko inayoendelea kutokea inaliweka jeshi letu hili katika nafasi ngumu zaidi ya kuheshimiwa kuheshimika, kuaminiwa na kuaminika
Maelezo ya kukinzana yaliyotolewa na viongozi waandamizi wa jeshi hili Iringa na Dar baada ya kijana kupatikana yaliacha shaka kubwa kuwa hakuna mawasiliano ndani yao....
Kusafirishwa na kuweka mahabusu huku viongozi wa jeshi la polisi wakiwa ndio wazungumzaji wakuu na bila kumpeleka mahakamani kwa siku kadha ni kashfa ya aina yake pia... Utawala wa sheria uko wapi?
Yaliyofuata yanajulikana Lakini kali kuliko yote ni sababu ya kumnyima dhamana mtuhumiwa kwa kisingizio kwamba NI KWA AJILI YA USALAMA WAKE.... kwakuwa waliomteka bado hawajakamatwa
Hii ni aibu kubwa kwa jeshi letu kwakuwa awali tukiambiwa na jeshi hilohilo kupitia wasemaji wake kwamba mtuhumiwa anashikiliwa kwa kosa la kujiteka na kuleta sintofahamu kwenye jamii akisingizia kuwa katekwa....

Inakuwaje leo hii aliyejiteka anyimwe dhamana ambayo ni haki yake kwa kisingizio cha waliomteka hawajakamatwa!? Ina maana mtuhumiwa ana nafsi mbili!?

Daima uongo hupanda lift lakini ukweli hukwea nagazi.... Natoa rai kwa viongozi wa jeshi hili kurudisha heshima ya hiki chombo kabla hatujachelewa sana

Jamiiforums na moderator pls spare this post
IMG-20180322-WA0024.jpg
 
Hapo sasa! Nasikia na huko Iringa Nondo AMEFIKISHWA Mahakamani. Watu wamezuiwa kumpiga picha....Kesi yake itatajwa tena Jumatatu ya Machi 26.
 
Siwezi kulikosea heshima hili jeshi ambalo ni chombo muhimu cha usalama wa raia... Kuna mapungufu mengi lakini bado lina nafasi kwenye jamii yetu kulingana na majukumu yake

Rai yangu kwa viongozi wa hiki chombo muhimu wabadilike wabaki na taaluma yao.. Wabaki na weledi wao uliotukuka.. Wajiepushe kutumika vibaya na wanasiasa wenye malengo na agenda z a siri.. Mambo yanapoharibika lawama fedheha kashfa na matusi huwaendea wao.. Huku waliowatumia wakiwa kimya na wasiojinesha... Ni sawa na shetani anakutumia kikinuka anakuacha unaaibika....!!!
Sakata la Kijana wetu Nondo linazidi kulichafua na kuliabisha jeshi letu adhimu... INAUMA SANA.. Mikanganyiko inayoendelea kutokea inaliweka jeshi letu hili katika nafasi ngumu zaidi ya kuheshimiwa kuheshimika, kuaminiwa na kuaminika
Maelezo ya kukinzana yaliyotolewa na viongozi waandamizi wa jeshi hili Iringa na Dar baada ya kijana kupatikana yaliacha shaka kubwa kuwa hakuna mawasiliano ndani yao....
Kusafirishwa na kuweka mahabusu huku viongozi wa jeshi la polisi wakiwa ndio wazungumzaji wakuu na bila kumpeleka mahakamani kwa siku kadha ni kashfa ya aina yake pia... Utawala wa sheria uko wapi?
Yaliyofuata yanajulikana Lakini kali kuliko yote ni sababu ya kumnyima dhamana mtuhumiwa kwa kisingizio kwamba NI KWA AJILI YA USALAMA WAKE.... kwakuwa waliomteka bado hawajakamatwa
Hii ni aibu kubwa kwa jeshi letu kwakuwa awali tukiambiwa na jeshi hilohilo kupitia wasemaji wake kwamba mtuhumiwa anashikiliwa kwa kosa la kujiteka na kuleta sintofahamu kwenye jamii akisingizia kuwa katekwa....

Inakuwaje leo hii aliyejiteka anyimwe dhamana ambayo ni haki yake kwa kisingizio cha waliomteka hawajakamatwa!? Ina maana mtuhumiwa ana nafsi mbili!?

Daima uongo hupanda lift lakini ukweli hukwea nagazi.... Natoa rai kwa viongozi wa jeshi hili kurudisha heshima ya hiki chombo kabla hatujachelewa sana

Jamiiforums na moderator pls spare this postView attachment 722666
Tutasikia mengi sana hiki kipindi
 
Kesi ya huyo kijana iko mahakamani. Polisi wanaingiaje kwenye suala ambalo maamuzi yako mikononi mwa Mahakama?

Mahakama ndio iliyomnyika dhamana.

Ningekuelewa kama lawama ungepeleka kwa hakimu aliyesema anaomba muda akasome sheria kuhusu mazingira ya kutoa au kutotoa dhamana.
 
Mimwenyewe nime shangaa eti "asipewe dhamana walio mteka wapo mtaani"hadi kichefu chefu.

Tukisema ukweli tunakuwa maadui eti tunalisariti taifa.

Mungu nipe ujasili haya nayo yapite.
 
Kesi ya huyo kijana iko mahakamani. Polisi wanaingiaje kwenye suala ambalo maamuzi yako mikononi mwa Mahakama?

Mahakama ndio iliyomnyika dhamana.

Ningekuelewa kama lawama ungepeleka kwa hakimu aliyesema anaomba muda akasome sheria kuhusu mazingira ya kutoa au kutotoa dhamana.
Acha blah blah angalia sababu za kunyimwa dhamana!? Je jukumu la ulinzi wa raia ni la polisi au mahakama!?
 
Kesi ya huyo kijana iko mahakamani. Polisi wanaingiaje kwenye suala ambalo maamuzi yako mikononi mwa Mahakama?

Mahakama ndio iliyomnyika dhamana.

Ningekuelewa kama lawama ungepeleka kwa hakimu aliyesema anaomba muda akasome sheria kuhusu mazingira ya kutoa au kutotoa dhamana.
Soma vizuri tuliza akili.usipende kuruka ruka mistali unapo soma.
 
Kesi ya huyo kijana iko mahakamani. Polisi wanaingiaje kwenye suala ambalo maamuzi yako mikononi mwa Mahakama?

Mahakama ndio iliyomnyika dhamana.

Ningekuelewa kama lawama ungepeleka kwa hakimu aliyesema anaomba muda akasome sheria kuhusu mazingira ya kutoa au kutotoa dhamana.
Acha kuwa mbumbumbu kwa kupotoshwa na ushabiki! Wewe ni zaidi ya hapo. Mahakama gani iliyomnyima dhamana huyo kijana?
Sababu za kuahirishwa kutolewa dhamana ni maombi ya serikali (DPP &Polisi) kuwa watekaji wake bado wako huko nje hivyo sio salama kwake kuwa nje.
Hayo maombi ndiyo yanayo hojiwa na mleta mada na watu wengine wote kuwa hivi Polisi waliomshtaki kwa kujiteka wanatumia weledi kweli?
 
Itakiwa mshtakiwa kuna kivuli chake kipo nje so akipewa dhamana tu kivuli chake kitamteka tena, imekuwa MATRIX[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji377] [emoji377] [emoji377] [emoji124] [emoji125] [emoji125]
 
[emoji15] [emoji13] [emoji13] au kigawe cha pili na cha tatu
 
Back
Top Bottom