Nina hofu ya Hepatitis B naomba ushauri

Hofumoyoni

Member
Nov 28, 2019
71
99
Ndugu, habarini za maisha.

Nachukua fursa hii kuwashirikisha hofu kubwa na kujikatia tamaa kunakoniandama kutokana na kugunduliwa kuwa na HBV.

Mwaka 2000 nilianza kuhisi kwamba size ya spleen imeongezeka. Lakini nilikuwa sijisikii kuumwa na chochote. Nilienda kituo cha afya Dr. akasema ni kweli ni kubwa lakini akasema ni jambo la kawaida, kuna utofauti wa size za spleen kati ya mtu na mtu lakini pia akasema jamii zingine kama Wamasai wanakuwa na spleen kubwa. Hilo lilinipa amani japo mimi sio Mmasai.

Mwaka 2006 nikiwa masomoni, niliamua kwenda kwenye zahanati ya chuo ili nisikie nitaambiwaje pia. Yule Dr. alinipa maelezo yanayo shabihiana na yale ya mwanzo lakini akanituma kwenye kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi. Daktari wa chuo alinitaka niende Muhimbili kufanya vipimo zaidi, ambavyo ni Ultra Sound na Full Blood Picture.

Matokeo ya Ultra Sound ni kwamba nilikuwa na Portal Hypertension ambapo flow ya damu kwenda kwenye ini haikuwa normal na kwamba damu inayokwama inalazimika kwenda kwenye spleen na ndiyo chanzo cha spleen kuenlarge.

Kwenye upande wa damu ndipo ikathibitika kuwa nina Hepatitis B. Kabla ya hapo nilikuwa sijawahi kuusikia ugonjwa huu. Hivyo nilianza kusoma ili niufahamu na ndipo nilipogundua kuwa hauna tiba. Kwa kweli niliishiwa nguvu na mwili kufa ganzi.

Kwa miezi kadhaa nilikuwa sijui natakiwa nifanye nini. Kuna wakati nilijiuliza, kuna haja gani ya kuendelea kusoma? Ila nilipokumbuka mpendwa mmoja ambaye tulikuwa wote chuo ambaye kwa wakati huo yupo chuo alikuwa na saratani, nami nilijipa moyo kwamba bado tumaini lipo.

Dr. wa chuo aliniandikia kufanya kipimo kingine cha mfumo wa chakula Endoscopic pale Regency ambapo ilionyesha kuna mishipa inaanza kutanuka kutokana na kupokea damu nyingi lakini inayotoka ni kidogo. Hivyo nilishauriwa kutofanya mazoezi mazito sana kwani yanaweza kupelekea kupasuka kwa mishipa hiyo.

Taarifa hii ilinikumbusha kipindi nipo darasa la sita, kuna mwalimu mmoja alikuwa analazimisha wanafunzi wote kukimbia kuzunguka uwanja hadi round 20 na kuendelea, na ukishindwa unapata viboko visivyo na idadi. Ni kipindi hicho tunakimbia nilijihisi kifua kubana, ila kwa hofu ya viboko niliendelea.

Baada ya kutulia nilianza kukohoa mate au makohozi yaliyochanganyika na damu. Hali hii iliendelea kwa miaka kila nilipokimbia, kufanya zoezi la viungo linalohusisha kunyonga mikono au kifua, au kuogelea kwa muda mrefu baadaye nilitoa makohozi yenye damu. Na nilipoenda kwenye kituo cha afya nilipimwa makohozi nikaambiwa niko salama sina TB.

Baada ya taarifa mpya juu ya afya yangu, niliendelea kuhudhuria Clinic Muhimbili, na Dr. aliyekuwa ananiona kwa wakati huo alisema sina sababu ya kutumia dawa yoyote. Mwaka 2016 nilifanyiwa US ambapo baada ya kupimwa walionyesha mshituko wa wazi, nilipomdadisi yule mmoja alisema kwa hiki kinachoonekana Mwenyezi Mungu akuonekanie.

Ni maneno ambayo yaliibua hofu yangu ya siku nyingi. Ikumbukwe kwamba, pale nilipo huwa ninajihusisha na mambo ya ushauri kwa vijana, kwa hiyo hata ninapowauliza madaktari ninaona kama wanajaribu kunituliza tu kwa kutumia mbinu ambazo hata mimi huzitumia.

Kitu cha ajabu zaidi ni kwamba, sijisikii kuumwa lakini ninapokuwa na watoa huduma wananiangalia kwa mshangao wa dhahiri. Kuna wakati ninaulizwa, mgonjwa yuko wapi? Kwa sasa ninaendelea na tiba Muhimbili, lakini inavyoonesha nimeshapata Liver Cirrhosis. Kuna wakati nilisikia kwamba MNH wana mpango wa kuanza huduma ya kupandikiza ini, lakini kwa sasa inaonekana kama zoezi limesimama na kwa sisi Watanzania masikini hatuna hata ndoto ya kupata huduma nje.

Kwa muonekano wangu mimi ni mzima sana, na sina historia ya kupata hata malaria au mafua. Ajabu ya kuumwa kwangu ni kwamba kunaonekana kwenye vipimo tu wakati mimi ninendelea na majukumu yangu kama kawaida.

Ninajua sote tu mavumbi na mavumbini tutarudi, lakini kuna wakati nafsi yangu inakuwa na maumivu makali ambayo siwezi kuyaelezea. Sijui mpaka lini, ila ninamuomba Mungu awasimamie wale wanoendelea na tafiti za tiba halisi ya maradhi haya.

Nina hofu na maumivu ya nafsi. Mungu awabariki nyote na kuwaepusha na madhila ya namna hii.

Asanteni.
 
Mkuu hii dunia hakuna mtu anaishi kwa amani, hayupo nakwambia. Kila mtu ana jambo linalomtatiza mshukuru Mungu huna maumivu ya mwili au dalili za kuumwa. Hayo maumivu ya moyo ndo binadamu tumeumbiwa, kuwa na furaha na amani
 
kuna sauti inaniambia nikwambie u won't die but you will live bro.... Mungu wetu ni mwema funua ufunuo 1 mstari wa 4 neno linasema yeye ni Alfa na omega yani mwanzo na mwisho naamini Mungu anakusudio zuri zaidi.

Pia usikate tamaa mkuu watu tumeisha humu ndani mwilini ni Mungu ndo anajua ukienda hospital utaona watu wanavyohangaika mkuu.
 
Kulingana na maelezo yako na vipimo mbambali ulivyofanya tatizo lako ni "Asymptomatic chronic viral hepatitis B with portal hypertension"

Kutokujisikia kuumwa au kuonyesha dalili yoyote haimananishi ya kwamba upo mzima. Kwa kawaida ugonjwa una tabia yakupitia hatua mbalimbali kabla ya kuonyesha dalili au ishara.

Mara nyingi kwa ugonjwa wa ini ili upate dalili ni lazima ufikie hatua ya ini kuanza kushindwa kufanya kazi (liver failure). Hivyo basi kipimo kinaweza kuonyesha una Liver Cirrhosis lakini bado ini linafanya kazi vizuri (normal liver function) kwa hatua hiyo unaweza usiwe na dalili au ishara inayohusiana na shida ya ini.

Ushauri
Napenda kukushahuri kufanya vipimo vifuatavyo kama haujavifanya
1. CT scan ya ini
2. Liver function test
3.Kidney function test
4. Hepatitis B viral load
5. Fanya tena kipimo cha endoscopy.
Tiba yako itategemeana na majibu ya vipimo tajwa apo juu

Ushauri wa ziada
Ondoa wasiwasi kwa maelezo yako sijaona kigezo cha wewe kuwa candidate wa liver transplant.
 
moesy, Nakushukru mkuu.
1. Viral load nimefanya ikasoma negative wakati hbv antibody ni postive.
2. LFT nimefanya ikaonesha linafanya kazi vivuri. japokuwa kulikuwa na baadhi ya maeneo 2 ambayo moja ilikuwa juu kidogo ya kiwango na nyingine ilikuwa chini kidogo.
3. Figo normal
4. CT Scan ya ini ndo sijafanya.
5. Endoscop nilifanya nikashauriwa kufanyiwa band ligation, miezi sita baada ya banding nikarudia wakasema iko normal.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom