Nina hasira kupita kiasi!

Nina hasira kupita kiasi!

tian

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2007
Posts
1,770
Reaction score
538
Ndugu zanguni mimi huwa napatwa na hasira kupita kiasi,Nikiudhiwa kidogo najikuta roho ishachafuka,nifanyeje ili niweze kuziepuka hizi hasira zilizopitiliza??

Mwanasaikologia ambaye yuko humu anipe ushauri tafadhali.
 
Mimi sio mwanasaikolojia, ila si vibaya nikikupa machache kwa mtazamo wangu.
Kwanza wewe una mwenzio? Kama yupo basi kila hasira inapokujia kama upo karibu nae anza kumuangalia usoni, vuta picha mnapokuwa kwenye kipindi cha furaha na mambo mazuri mliopitia ikiwezekana anza kumsogelea halafu mpe maneno matamu ukiona anaanza kutabasamu na wewe kidogokidogo utaanza kushusha hasira na akili yako kuhamia upande mwingine.

Kama unapenda michezo, hiyo hali ya hasira ikikujia nenda sehemu za michezo, hata kama hushiriki angalia(kuwa mtazamaji). Akili yako itaanza kuhama taratibu na hasira itakuwa inashuka kadri muda unavyoenda.

Kama mpenzi wa filamu,ondoka taratibu eneo la tukio nenda CINEMA itakusaidia kwenda kujichanganya na watu wengine na wewe akili yako itakuwa kwenye filamu nina uhakika kabla ya filamu haijaisha utakuwa umeshashusha munkari.

Nafikiri kwa haya yangu machache na kwa wakuu wengine watakaofuata kuleta michango yao inaweza kukusaidia

Kila la kheri
 
Ndugu zanguni mimi huwa napatwa na hasira kupita kiasi,Nikiudhiwa kidogo najikuta roho ishachafuka,nifanyeje ili niweze kuziepuka hizi hasira zilizopitiliza??

Mwanasaikologia ambaye yuko humu anipe ushauri tafadhali.

kaa mbali na wakutiao hasira....

kuwa mtu wa maombi sana, ishike biblia, usiiache iende zake...

kunywa maji mengi, upunguze high blood presure...

epuka makundi ya ovyo ovyo yasiyo na tija kwako, maana hayo ni machukizo...

jiweke busy muda mwingi... usiwe mgomvi wala mshabiki wa mambo yasiyo na maana..

somehow nadhani nimekusaidia.
 
Wewe ni dini gani? Kama ni muislam jitahidi kukaa na udhu mda mwingi, kama sio muislam ata kunywa maji inapunguza hasira na amini sana Mungu, hasira ni weakness kua imani yako ni ndogo. Lakuongezea hamia jukwaa la jokes/utani
 
Kuwa mtu wa maombi,mkabidhi Yesu maisha yako.
-Hapa utapata faraja,furaha na amani ya kweli.
-Utakuwa busy na mambo ya kujenga,yaani baada ya kazi zako unarudi kumtukuza Mungu.
-Pata muda wa kukaa peke yako kwa masaa kadhaa ukiwa umepumzika.
Si kila wakati lazma ujichanganye na watu.
-Epuka kuchanganyikana na watu ambao unajua anytime wanaweza kuwa kero kwako.
-Pata muda wa kutosha kukaa na familia yako,kwa mf:ktk taarifa ya habari,kushiriki pamoja chakula cha usiku.
-Pia jifunze kusamehe na kusahau,hata kabla hujakosewa uwe na roho ya msamaha.
-Mwisho jibidiishe ktk kazi zako,hii itakukeep busy na hautakaa kufikiria mabaya.
 
Asanteni kwa ushauri mzuri,nitajitahidi kuutilia maanani

Mbarikiwe mno.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom