Nina hamu kweli leo!!!!!!!!!!!!!!!!

Nina hamu ya kukesha leo, mtu yeyote asiye na usingizi aje hapa tukeshe mpaka majogoo tukipiga soga
Karibuni kibarazani, hapa nina tende na halua na kibirika cha kahawa pembeni

fanya mpango hizo bidhaa zitufikie na siye...ndio tufikirie kukesha nawe
 
halua na kahawa ni tamu ka nini, yaani huku visiwani twafaidi kweli, huko kwenu bara mmezoea kashata za karanga wala si tamu kama halua
 
Hivi halua yaonekanaje mpendwa, ujanja wangu wote hata sijui vile yaonekana...
 
sana tu aisee hapa mate tu yanazidi nitoka

utajiju mwakosa vitamu nyie
nawashangaa mwenda Tanga badala ya kuja huku ZNZ.
Shauri zenu mkipigwa zongo huko, mie simo maana hata sijui kutabana zongo
 
Hivi halua yaonekanaje mpendwa, ujanja wangu wote hata sijui vile yaonekana...

iko kama sega la asali hivi, lakini imekolea rangi.
inapikwa kwa maji ya mvua na sukari na sesame, usiombe upate iliyopikwa na mzee Saidi Makame
 
mmh haya bhanaa...hadi maji ya mvua lol...
leo inakuaje haulali au ndio kibarua kile kimeanza?
 
kazi naanza Januari 15.
Niko huku Makunduchi kuna mkesha wa KIDUMBASI na MSEWE, mie iko chumbani nimejifungia nimechoka kucheza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…