Nina hakika ujinga sasa umevuka mipaka

Hakika hata mimi ilinishangaza sana wakati waziri Jenista Mhagama anatoa maelezo mbele ya Mhe. Rais. Badala ya kuongea hoja za msingi anaanza kusifu kijana wa UVCCM.
Nikajiuliza vipi kuhusu wale wasiokuwa na chama waliojitoa usiku na mchana kuwahudumia waathirika, majirani waliowapa hifadhi waathirika, ndugu na jamaa wanaotuma michango mbalimbali, madaktari na askari wanaokesha kuokoa na kuwahudumia waathirika na mengine mengi.

Niliishia kupata maswali mengi pasipo majibu
 
Hii tabia a uchawa iliyoanza kuota mizizi ni mbaya sana,itaharibu taifa na kizazi chetu,Cha ajabu kabisa inaonekana watawala wanagurahishwa sana na machawa,na Ili upate teuzi au ulinde nafasi Yako inabidi tu uwe chawa,Kwa bahati mbaya chawa hawana rafiki wa kudumu,wao wanamasirahi ya kudumu.
 
Heshima haiji automatic, Bali huwekwa mazingira ya heshima kuwepo. Hakuna namna utaweza kumuheshimu kiongozi kwenye mazingira yasiashiria heshima. Labda kama kwako rais ni Mungu. Lakini kwa Hawa viongozi wanaoingia madarakani kwa chaguzi za kishenzi, ni nadra kuwapa heshima.
 
Ukweli kabisa, wewe ni mtu wa hovyo kulikoni wote nchini, unahitajika kushughurikiwa ili ujinga ukuishe! Ushurutishwe urudi shule na upite JKt na msimamizi wako awe mwenye roho mbaya kuliko ya yeyote nchini

Unaboa sana mwashambwa wewe
 
Uongozi kwa Tanzania, unamfanya mtu kupungukiwa akili, hekima na tafakari. Na uongozi ndani ya CCM unamfanya mtu kuwa punguani kabisa.

Umesema kweli, yaani Jenista Mhagama anasifia UVCCM wakati anajua kabisa kuwa watu wa kwanza waliowasaidia sana wahanga, ni majirani, ambao walienda kuwasaidia wenzao bila hata fikra za vyama vya siasa. Lakini akili na macho ya Jesista, vyote vimepofushwa na mahaba ya chama. Chama kimemfanya kuwa punguani, asiobe hata yaliyo wazi. Anashindwa hata kuwaona wale wanajeshi waliozama ndani ya tope, anawaona UVCCM tu wanaorandaranda.
 
Ukweli kabisa, wewe ni mtu wa hovyo kulikoni wote nchini, unahitajika kushughurikiwa ili ujinga ukuishe! Ushurutishwe urudi shule na upite JKt na msimamizi wako awe mwenye roho mbaya kuliko ya yeyote nchini

Unaboa sana mwashambwa wewe
Huyu Mwashambwa yumkini ni mgonjwa wa akili. Na sijui aliishia darasa la ngapi? Ni aheri ambaye hajaenda hata darasa moja lakini mwenye akili ataongea la maana hata kama hajui kuandika, kuliko huyu Mwashambwa. Huyu siamini kama ana mchango wowote kwa yeyote, lakini kwa vile ni mwanadamu, basi wacha aishi, tumvumilie, kama tunavyoweza kuwavumilia viumbe wengine wasio na utashi wa kujua jema na baya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…