Nina hakika ujinga sasa umevuka mipaka

Vyeo walivyonavyo wamevipata kutokana na vitendo vyao vya kujikomba, kujipendekeza na kusifia kwa unafiki. Je, wataachaje kufanya vitendo hivyo wakati ndivyo vinawapatia shibe yao ya kila siku???
"Mtumikie kafiri ili upate mradi wako."
Jambo la msingi wanalotakiwa kujua wenye kutoa vyeo ni kwamba, watu wanaojikomba sana ni rahisi kusaliti hata kuua viongozi wanaowateua kuliko wale wasiojikomba.
Akili inayojikomba sana ni hatari kuliko ndui.
 
Mkuu,

Hujui kwamba kampeni za 2025 zishaanza kwa kasi kubwa sana?
 
Ujinga nao ni kipaji Mkuu.

WAACHE WAONYESHE VIPAJI VYAO

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Katiba ya Tanzania imempa Rais umungu mtu, hivyo 'waja' lazima wajikombe wapate neema yake.
Rais anatakiwa apime, ateue watu wenye akili za kawaida, zilizoridhika kulingana na mazingira, wasiojikomba sana ili kujenga taifa la watu wanaojielewa.
Changamoto ni jinsi ya kuanza, kwa ni yawezekana wengi wa wanaopendekeza na kufanya vetting, wakawa na fikra hizo hizo za sifa za kujipendekeza na kujitoa ufahamu.
 
Rais ni MMOJA wa wafiwa, sababu wananchi anaowaongoza wamepoteza ndugu zao na Mali.

Kumpongeza Rais msibani, ni kumpongeza Kwa kufiwa.

Kucheza ngoma katika tukio Hilo Si sawa.
 
CCM wana upumbavu mwingi sana
 
Wewe nadhani Ni mgeni Tz .....hao hao watu walitangulia Hanang kutanua na Chopa na kupiga selfie nyingiii. Endelea kuwashangaa wakishakusanya posho wanakuja kuwanunulia vijana pombe Kali vya buku mbili mbili wawasifie
 
Watu wanataka kiki hadi Msibani🤣🤣
 
Jambo la msingi wanalotakiwa kujua wenye kutoa vyeo ni kwamba, watu wanaojikomba sana ni rahisi kusaliti hata kuua viongozi wanaowateua kuliko wale wasiojikomba.
Akili inayojikomba sana ni hatari kuliko ndui.
Ni kweli, upo sahihi.

Watu wanaojikomba ni watu walioukatia tamaa utu wao. Ni wale watu ambao mioyoni wameshajiapiza kuwa, "nipo tayari kufanya chochote alimradi nipate cheo au fedha". Huyu hata akiambiwa aue ili apate cheo au fedha, yupo tayari. Hata akiambiwa awe shahidi wa uwongo ili apate cheo au fedha, yupo tayari. Huyu akiwa na cheo kidogo, akishawishiwa amwue hata boss wake ili achukue madaraka mtu mwingine, na yeye apewe cheo kikubwa zaidi, atakuwa tayari kufanya hivyo.
 
Huwa nawashangaa sana nyie, mnawalaumu hao watu kweli?

Tatizo sio wao, tatizo lipo juu huko. Kama kweli "HOS" anajua kilichompeleka huko, asingeruhusu wala ku-entertain huo ujinga, lakini it was okay for him/her( whoever is concerned), sasa unawalaumu kweli hao watu unamuacha huyo?????
 
Tu
Tuogope sana kuwa na taifa la wajinga wengi wengi maana wakiwa wengi wanao uwezo wa kuchagua kiongozi kutoka kwenye kundi lao hivyo taifa litaongozwa na kiongozi mjinga (James Mbatia akitoa mchango wake Mbungeni).
 
Hawezi kukosa kubeba lawama, maana si rahisi watu wakufanyie mambo usiyoyapenda.
 
Chawa hupendelea mazingira machafu ama uchafu.
 
Hapo, bila kupepesa macho, tatizo kubwa ni kwa anayesifiwa. Chawa wanajua ulipo uchafu wakazamie
 

Kaka hata Kama ni uchawa sio Kwa stail yako.
Watanzania pamoja an upunguani walionao, wanaujua ukweli halisi. Usijitoe ufaham kiasi cha kupoteza utu wacko
 
Mkuu tstizo siyo system bali tatizo ni wagombea wa uraisi. Unamleta mgombea uraisi anaishi nje ya nchi tena kampeni zake ni za masimango na majigambo mwanzo mwisho. Wewe unategemea nini?

Unavyowazia kubadilisha uongozi wa nchi jadili pia na kubadili uongozi ndani ya chama. Why kiongozi wa chama anakuwa ni kiongozi wa kudumu? Why waelewa tusifikilie kwamba kiongozi huyo amewekwa na chama tawala kwa manufaa ya chama tawala

CDM BADILISHENI UONGOZI WA NGAZI YA TAIFA ILI KUPATA MAONO MAPYA. ACHENI KUKIFANYA CHAMA KAMA NI MALI YA MTU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…