Nina ADA, CPA(T) na Masters in Accounting and Finance lakini sina kazi zaidi ya mwaka sasa!

Kwa sifa zako za elimu hustahili kulala huna kazi. Nachoweza kukushauri ajira kwa sasa ni gharama kwa mtu kama wewe ambaye huna uzoefu wowote maana utakuwa unahitaji mshahara mkubwa sana wakati uzalishaji wako (productivity) unaweza kuwa chini ya mtu mzoefu mwenye ATEC.

Nachokushauri tafuta audit firm ambayo iko busy uombe hata kukaa pale kama "Voluteer" wakikulipa kwa "assignment basis" baada ya miezi sita CV yako itapanda na utakuwa unatafutwa badala ya wewe kutafuta kazi. Kuna mtu alikuwa na tatizo kama lako nilikaa naye kama mwaka sasa hivi yuko kwenye chati na mara ya mwisho ilibidi aombe ushauri maana alipata zaidi ya kazi tatu kwa mara moja.

Kama uko Arusha unaweza jaribu Welcome to Facebook - Log In, Sign Up or Learn More

Ushauri mzuri sana, watu wengi hawapendi kutumia fursa hii ya ku-volunteer. Watu wakishaona matunda ya kazi yako, watakulipa tu na huo utakuwa mwanzo mzuri.
 
ndiyo kaenda masters, lakini kakaaje tena kitaa mwaka mzima.

Jamani si post yake iko wazi? kasema ameenda masters sawa, lakini yeye alichokuwa anasisitiza ni kuwa ana mwaka tangu apate CPA na si tangu apate masters. Mana aliweka wazi kuwa masters keshamaliza course work bado desertation sa mwaka kaumalizaje na masters. Kwa maelezo yake atakuwa amegraduate mwaka jana maana hii thread ni ya muda kidogo.
 
pole sana,kama huna connections i suggest u look for a job in organizations that value education background such as TRA,TBL,and other private companies ambazo hazina wabongo wengi!!!!kuwa mvumilivu,utapata kazi!!!
By the way mie naenda hapo mzumbe,mbona wametuongezea ada,wanatupa kweli hivo vitabu au ndo tunalipia tu

TRA asijisumbue, hawaajiri mtu mwenye sifa kama hizo! ajira zilizopita kama miaka 2 iliyopita, CPA ilikua ni kigezo cha kukuondoa kwenye kinyang'anyiro! Njia nzuri ameshakupa Ndachuwa
 
Umeunganisha ya nini? Wengine wana Ada tu wakati we unaongeza hayo madudu wanakula goodwill na udhoefu, sasa wana ajira, na wanasomeshwa, Wewe uliyakimbilia hayo ya niño?

Jamani wadau naomba msaada, mana nimeangaika hadi nimechoka kutafuta kazi. Nina Ordinary Diploma in Accountancy GPA 4, Advance Diploma in Accountancy GPA 4.2. zote nimepiga IFM.

Nilipomaliza Advance mwaka 2009 niliunganisha kufanya masters ya Accounting and Finance toka Mzumbe University, and on the same time nikawa nafanya CPA.

CPA nilipass zote at 1st sitting na June mwaka jana nikawa nimeipata. Masters nina GPA 4.1, bado kudefend thesis tu. lakini wadau nimetafuta kazi tangu nilivyopata hiyo CPA hadi leo hola! Nisaidieni basi ndugu zangu!
 
Ukitaka uone faida ya elimu yako tafuta kazi yakufundisha utapata hasa kwenye vyuo mbalimbali omba utapata
 
Tuma application yako kule Tumaini University, Iringa. Nilisikia wanahitaji assistant lecturer kwenye fani yako. Best wishes.
 
Pole;Ila ulikosea sana kuunganisha elimu,inatakiwa ukimalaiza hatua m,oja tu tafuata kazi kwanza huku ukisoma ukiwa kazini.
Master is non sense in Accounting na hahitajiki coz accounting is the same in all level na pia wenye GPA kubwa ktk kampuni za kawaida huwa hawahitaji coz huwa wanatabia ya kujiona sana.
NB:Huu ni ushauri kwa wanaounganisha masomo.mfano ofisini kwetu kuna mtu alienda kusoma master aliporudi aliongezewa elfu hamsini tu.
Uzoefu ndio muhimu

Cha kufanya omba kazi na vyeti vya ADA tu halafu baada ya kuanza unakuja kuvilteta baadaye.
 
Jamani wadau naomba msaada, mana nimeangaika hadi nimechoka kutafuta kazi. Nina Ordinary Diploma in Accountancy GPA 4, Advance Diploma in Accountancy GPA 4.2. zote nimepiga IFM.

Nilipomaliza Advance mwaka 2009 niliunganisha kufanya masters ya Accounting and Finance toka Mzumbe University, and on the same time nikawa nafanya CPA.

CPA nilipass zote at 1st sitting na June mwaka jana nikawa nimeipata. Masters nina GPA 4.1, bado kudefend thesis tu. lakini wadau nimetafuta kazi tangu nilivyopata hiyo CPA hadi leo hola! Nisaidieni basi ndugu zangu!

Hilo ndio kosa lako too much bookish with ziro experience , ulikosea kukimbiza haraka haraka bila kufanya kazi na elimu uliyo nayo inacomand mshahara mkubwa sana wakati hujakua productive kwa kampuni ndio maana hupati kazi haraka,tafuta mahali ujitolee (Volunteer ) kwa miezi sita hasa UN agencies ukitoka hapo utapata kazi ya maana.
 
Daah natamani uniazime hiyo CPA yako. Bosi angu kila nkimwambia aniongezee mshahara ananiambia eti mie cio Accountant mpaka niipate hiyo kitu ndo napata inkrimenti.
 
Ordinary Diploma ya Accounts haikuwepo mwaka 2006/2007 bali kulikua na Certificate na sio ya accounts pale IFM kama sijakosea, hebu funguka hiyo Diploma yako ni ya wapi?
 
Mimi ni mvulana, nina miaka 27 kwa sasa, vyuo niliomba lakini hivi vyuo vikuu vinatukataa sisi tuliotoka kwenye hivi vyuo ambavyo haviko chini ya TCU! IFM nilifatilia lakini walisema wanawalimu wa kutosha kwa masomo ya Accounts. CBE napo waliniambia niandike barua ya kuwa mwalimu wa part time, hadi leo sijapigiwa!
Nimejaribu kufatilia kwenye Auditing firm naona kama wananielewa lakini bado hakijaeleweka!
aiseeee kumbe!
mi nilishaapply kazi UDOM kama mara 3 hivi sijawai kuitwa hata mara moja japo kwenye interview, kumbe ndio UKIRITIMBA wao, loh
 
Kwenye interview una perform vipi? Kwa hiyo GPA mbona unaweza kuwa academician, au hutaki? Kwa hizo qualifications tatizo pia huenda likawa ni aina ya kazi unayoitaka... Kazi nyingi zinazohitaji masters, pia zinahitaji uzoefu kadhaa... kuwa tayari kujishusha... Masters being a specialized research degree, mtu hawezi tu akakupa high office kwa masters peke yake, there are lots of things kwanza... So, just think ni kazi gani unataka, angalia kwa kawaida wanaotakiwa ni watu gani, and then think of how to get there. Cha muhimu, qualification yako kwenye makaratasi iendane na performance yako... Naamini hiyo marks ilipatikana kihalali.
 
Back
Top Bottom