Nimvumilie mume huyu au nimuache?

mdau,nadhan hujaelewa maelezo yangu vzr.hajawah kunifumania zaid ya kuhis tu fulan au fulan hata kwa
kusalimiana tu.hatak niwe karibu na rafk yyt tangu
nasoma,kila mtu alimuona hafai .na km nngetaka kuua
cdhan km tungekuwa nyumba moja had muda huu.
kuna wenza wanafanya mambo makubwa zaid ila husameheana na maisha huendelea,n lip hilo baya kuliko lote ntakuwa nmetenda lisiweze samehewa?
ckatai cwez nkawa perfect lazma nna mapungufu yangu,je wote waishio kwa aman ktk ndoa zao hawana mapungufu na hawagomban?mbona hawatendw hv!

WE DADA UTAKUA UMEFANYA ISSUE MBAYA SANA KWA HUYU MSELA, YEYE PIA NI BINADAMU MWENYE AKILI ZILIZOTIMIA NA ZENYE UTASHI, SIO RAHISI MTU AHAME CHUMBA KWA MAKISIO TU YA MATUKIO MABAYA UYAFANYAYO.... TUNGEPATA FURSA YA KUMUULIZA NA HUYO MSELA WAKO TUNGEWEZA KUSHAURI KWA UFASAHA KABISA.................. :smash:
 
He yaani mpaka kahama chumba?? Bado umekaa tu unasubiri nini???
Anarudi saa 8 or 9 usiku are you serious?? Ni mlevi?? Je! anakuwa anatoka wapi??
Mahusiano ya nje?? Unajua??

We chukua hatua si mpaka kwa hisani ya watu wa marekani ndo uelewe
Chapa mwendo Ndoa ndoa ndo nini??? Waliachana kina Winie Mandela ije kuwa wewe??
Yanini ujipe matezo duniani wakati bado unajipenda?? Tena una degree halafu unailalia
Tu kitandani?? Halafu we mwanamke wa wapi wewe bado umelala mpaka leo
Eti unanyanyaswa umekaa tu?? Hivi husikii hata wanaharakati wanavyosema??
Wanawake wanaweza??? Hebu funguka macho wewe acha kulegea ahhh
Cha uzembe kama huo bana............


The real DENA AMSI hatimae....
 
Mama huyo mwanaume amesha kuwa Mariboro ya mavi isipo kunukia itakuelemea kuwa makini hakufai huyo toweka karibu nae anagonga nje huyo atakuletea maradhi bure. Mama'e hafai huyo.
 
......Kama kweli pole sana, na umeweza kuvumilia wewe!! Ni hivi umemaliza bachelor yako, tafuta kazi.....jifanye upo busy wala usiwe na time naye, yeye mwenyewe atajishtukia kama bado anakupenda kweli.

Ukiona umekuwa busy na bado anaonyesha madharau yake, sasa hapo waweza kuendelea na mipango yako ya kumuacha. Ndoa ya kanisa ni kweli ni ngumu kuachana lakini ina mwisho wake mwenzangu.....wewe bado mdogo na tena uliwahi kuolewa kwa kumpenda yeye lakini hustahili hizo adhabu anazokupa........ujue kunyimwa tendo la ndoa ni adhabu tosha kwa umri huo, maana hiyo age ndio yenyewe kufurahia tendo.
 
Shost, mi nimwanamke ila mumy jitambue unamatatizo na jirekebishe kwani nina hakina hujitambui. Jamani shule sio sawa kuishi na jamii, elimu ya shule ni kukufanya ujue kutunza kumbukumbu na elimu ya duniani ndio mwisho wa mambo yote? We mtu mpaka anahama chumba akupe nafasi ujirekebishe bado hutambui? Huyo baba mwenzio alivyokuowa alikuwa ameshajitambua kuwa anafanya nini na ameshamaliza kutangtanga anataka atulie sasa wewe bado hujajitambua. Na hata ukiachana naye huyo, hutopata mwingine ambaye utadumu naye. Umeshindwa kurekebisha huyu uliyenaye utaweza kumrekebisha ambaye humjui? La hasha. Ukiweza kutunza kidogo na kikubwa pia utakitunza.
 
Kiukweli pole na maisha uliyomo kwa sasa, nimejisikia huruma sana kumtenda mtoto wa mwanaume mwenzio kiasi hiki.

Sasa basi kabla sijatoa ushauri wangu ninaswhali kwako tafadhari. Kama huyu jamaa ni shetani kiasi hiki kwanini ukiondoka kurudi kwenu akufuate kwa kupiga magoti, na ukirudi kwake anaendelea na ushetani wake maradufu????

Unadhani ni kwanini huyu shetani anataka uendelee kuishi kwake huku ukiwa unalala chumba cha wageni??
 
......Kama kweli pole sana, na umeweza kuvumilia wewe!! Ni hivi umemaliza bachelor yako, tafuta kazi.....jifanye upo busy wala usiwe na time naye, yeye mwenyewe atajishtukia kama bado anakupenda kweli.

Ukiona umekuwa busy na bado anaonyesha madharau yake, sasa hapo waweza kuendelea na mipango yako ya kumuacha. Ndoa ya kanisa ni kweli ni ngumu kuachana lakini ina mwisho wake mwenzangu.....wewe bado mdogo na tena uliwahi kuolewa kwa kumpenda yeye lakini hustahili hizo adhabu anazokupa........ujue kunyimwa tendo la ndoa ni adhabu tosha kwa umri huo, maana hiyo age ndio yenyewe kufurahia tendo.


ni kweli ajaribu naye kutoa adhabu kwa kumwangalia na kumdharau na kujiweka busy na kazi itamsaidia kupunguza msongo wa mawazo na pia kama ikiwezekana afanye mazoezi kwa ajili ya kupunguza stress pia.. inatakiwa asifanye maamuzi ya kukurupuka ni kweli anakosa mlo halisi na halali lakini akikurupuka matokeo yake anaweza kujikuta anaruka mkojo na kukanyaga kinyesi
 
pole mamii ..ila hivo ni vijimambo tuu ..ila swali anarudi saa 8/9 hizo maneno ya umbea anatoa wapi?na je huwa unamjibujibu vip maana pengine akiwaka na wewe unaongeza petrol hapo hamuwezi tatua tatizo.Suala la wewe kuondoka halitakusaidia cha msingi wewe tafuta kazi kuwa bize ila epuka kuanzisha mahusiano nje ya ndoa utavuruga kila kitu mama huyo si wa kushindana naye.
Mnapaswa kujua ndoa ni taasisi inayoshambuliwa sana na mfalme wa dunia hii (ibilisi) cha kufanya anza utaratibu wa maombi muombee mumeo,na ikiwa umemkosea chochote ombaneni radhi tena inaonyesha ana tabia ya kuweka vinyongo muombee tabia hiyo imuache..Mungu anafanya..na Mungu amekuweka uwe mlinzi kwa mumeo.
Kuwa mlinzi haimaanishi umfwate kila anakoenda ..ila amini utapoanza kumsamehe maneno yake ya kero na pia mweleze kuwa hushindwi kununua vyakwako na muombe akupe muda ili umuonyeshe kuwa unaweza.
Fanyianeni kwa upole mwambie kuwa unataka muanze upya mnahitaji kujenga familia bora,kukimbia chumba hamtaweza fika popote.
Muulize kwa upole kuwa kwanini alikuoa ikiwa unalala mwenyewe? alikuoa uje uwe mlinzi au alikuwa anawaza nini? mwambie aache tabia ya kukusimanga hupendwezi nayo .Tafuta ulipokosea kama chanzo ni wewe kutopata mtoto mweleze kuwa watoto wanatoka kwa Mungu na hilo ni jaribu tu mbona Sara alipata mtoto uzeeni? na pia Ibrahim hakumtenda hayo?
 
mpige chini fasta, sijajua unangoja nini hapo kwako, huu ni mwanzo tu, utaona makubwa zaidi ya hayo siku zinavyozidi kusogea. fanya maamuzi mapema.
 
Pole sana!..Je, kuna kitu umemfanyia mumeo mpaka ana-react hivyo? Hebu kaa chini uongeee nae akikwambia vitu vyako vilivyomkera halafu tuambie na tuone jinsi ya kushauri..
Vinginevyo pole, fanya maamuzi yatakayokuridhisha wewe maishani mwako...maana hilo ndio muhimu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom