Nimshughulikie au? Naombeni ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimshughulikie au? Naombeni ushauri

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Michael Pima, Jan 22, 2012.

 1. Michael Pima

  Michael Pima Member

  #1
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nilikutana na huyu binti kwa mara ya kwanza ndani ya basi moja maarufu lifanyalo safari zake kati ya Dar na Morogoro. Tulikaa nae siti zilizopakana, na sikuongea nae kwa takribani nusu saa nzima ya safari. Baadae akawa amepitiwa na usingizi na kunilalia kwa kuniegemea. Kama ilivyo kawaida ya wanaume walio wengi sikuthubutu kumkatiza usingizi wake kwa kumwamsha asiniegemee. Nilivumilia na robo saa baadae basi likapiga tuta akaamuka na kuniomba radhi kwa kuniegemea. Nilitabasamu nikamwambia usijali na hapo ndio ukawa mwanzo wa maongezi yetu yaliyo pelekea kufahamiana na hadi kubadilishana mawasiliano. Tumetokea kuwa marafiki wakubwa sana sijawahi kuona. Hadi watu walio wengi wanadai nina mahusiano nae ya kingono kwa jinsi nilivyo karibu nae.

  Ilikuwa ni mwezi uliopita siku ya boxing day alinipa mwaliko maalumu kumtembelea katika chumba chake anachoishi. Hii haikuwa mara yangu ya kwanza kwenda kumtembelea na hata yeye alishawahi kunitembelea kwangu mara kadhaa. Kwa kweli kama ni zile sifa za uzuri zinazovuma mitaani naona zote anazo. Ninachokiona cha zaidi kwake ni ile sifa ya kumcha Mungu sana. Nilifika mida ya saa kumi jioni, nikabisha hodi bila kuitikiwa. Kwa kuwa mlango ulikuwa umeachama kidogo yapata uwazi wa sentimeta kumi hivi nilijua hayuko mbali yupo karibu tu. Lakini msukumo mkubwa ulioibuka mshindi ni ule ulionituma kuchungulia kwa kuongeza kidogo upenyo wa uwazi wa mlango. Baada ya kuufungua mlango mboni zangu za macho zikatua katika mwili wake uliositiriwa na kanga moja tu. Alikuwa amelala kifudifudi na ilionekana kama alikuwa amesinzia fofofo.

  Nililazimika kumwita mpaka mara nne ndipo akastuka, akanikaribisha, nikaingia na kuketi. Tulibadilishana mawazo, tukaangalia music katika screen, tukacheka, nikala, nikanywa na ilipofika saa moja jioni nilimuaga. Alinisihi nimsubiri aoge ili anitoe kidogo maana nae alikuwa anataka kutoka jioni hiyo. Alikwenda kuoga na aliporejea na kanga yake moja hiyo hiyo nilitaka kumpisha ili avae lakini alikataa na kuvaa nikiwa ndani humohumo. Baadae akaniambia anataka anifanyie surprise lakini sharti nifumbe macho kwanza. Nilitii sharti kwa kuwa nilipatwa shauku ya kuiona surprise yenyewe. Baada ya dakika kama moja akaniambia nigeukie upande wa kitanda ndipo nifumbue macho, nami nikafanya hivyo. Sikuelewa elewa baada ya kufumbua macho kwa juu ya kitanda niliona vitu ambavyo sikutarajia kabisa kuviona. Nilikuta ametapakaza kitanda kizima vipakti vya mipira ya kiume. Nilipogeuka ili kumuuliza kulikoni nilijuta kugeuka. Nilikuta amevua nguo zake zote yupo mtupu kama alivyozaliwa.

  Damu yangu ilichemka, akili ikawa sio yangu tena maana kwa kweli maungo yake hadharani yana sifa nzuri mno sijawahi kuona. Damu ilitembea mpaka kwa mwana wa pale kati akakasirika na kuamka. Ghafla iliniijia sura ya mchumba wangu ambaye ninae kwa miaka miwili sasa na mwezi wa kumi mwaka huu tunatarajia kufunga ndoa. Nikamwambia simuelewi mambo anayofanya, wakati huo nikiwa nimetizama pembeni. Tulijibizana huku akiniongelesha kwa sauti ya mahaba na hata akadhubutu kunifuata kwa nyuma na kunigusa gusa. Ili kuepusha mengi niliamua kumuaga huku nikielekea usawa wa mlango pasipo kuinua kichwa kumtazama. Nikakishika kitasa cha mlango na kukinyongea chini huku nikiuvuta mlango kwa ndani. Haukufunguka nikajua amefunga na kuutoa ufunguo. Kuikata stori iwe fupi, ilibidi niwe mpore busara ikatawala zaidi mpaka mdada huyu akaamua kuvaa nguo zake na mambo yakarudi kawaida. Akanisindikiza mpaka nikapanda daladala nae akarudi kwake.

  Toka siku hiyo hakomi kunipigia simu na kunitumia meseji za kimahaba. Bahati mbaya mchumba wangu anasoma mwaka wa tatu na wa mwisho chuo kikuu Dododma nami nipo ninaishi Dar es salaam hivyo inakuwa vigumu hata kumchunia rafiki yangu huyu au kuwa na hofu na meseji zake anazonitumia. Toka tukio hili litokee nimekuwa mbali kidogo nae lakini yeye amezidi kuwa karibu sana. Kitu kimoja kikubwa ninachokihusudu toka kwake ni sifa ya urembo pamoja na kujichunga lakini nashangaa kwa nini mimi ananifanyia hivyo. Kuna watu wenye pesa wengi sana huwa wanamfukuzia na hajawahi kumkubalia mtu hata mmoja kati yao na kila kukicha idadi ya wanao ongezeka kwenye list ya wanaomtokea inaongezeka tu. Mda wote wa urafiki wetu sikuwahi kumuona na boy friend tofauti na mimi, na amekuwa akipenda sana kuwa nami na ndio kisa cha watu kusema nina mahusiano nae.

  Ndugu zangu wapendwa hayo ndiyo yanayonisibu kwa wakati huu. Nimekamatika njia panda, watu wengi sana wanamtaka tena watu wazito kabisa na maarufu lakini hawajampata lakini kwangu mimi amekuja yeye mwenyewe! Sasa kila siku najiuliza sijui nimshughulikie? au sijui vipi? Naombeni ushauri wenu wana jamii forum wenzangu.
  Aksanteni sana.
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Yaani umekaliwa uchi hujafanya kitu, hapa unataka tukushauri kitu gani? Alaa...!
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Kamuuzie shigongo hii hadithi
  akiiwekea nakshi nakshi vizuri, utajipatia kipato.

  Afu naomba hiyo soseji nitengenezee hotdog maana haina kazi tena.
   
 4. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mshughulikie uipate, nina jamaa yangu hapo Moro ana mahusiano na jini sasa hivi anataka kutoka hawezi. Kwani hujaridhika na mchumba wako. Tamaa mbele mauti nyuma!
   
 5. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  We tusikilizege tu wadada na story zetu..alikuambia nani anawakatalia hao wengine(yeye)? we una nini hasa akutake wewe? Shtuka!

  Mtu anayejichunga na kumcha Mungu halazimishi mambo wala kumtega rafiki yake wa karibu kwa makusudi....huyo kakubuhu....!

  Una mchumba wako, tunza uhusiano naye na Mungu akusaidie,huyo dada achana nae, before its too late!
   
 6. k

  kisukari JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,764
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  mmmh,siku hizi watu wa dini ni wachache.kama angekuwa mtu wa dini,asingekufanyia hivyo.nyege hizo nyege gani?inaonyesha aliyapanga hayo zamani.na wewe pia inaonyesha ni sitaki nataka.kwa nini usimwambie ukweli kama una mchumba wako?na mueleze msg za mapenzi asikutumie kwenye wewe na yeye sio wapenzi.kama kweli unampenda mchumba wako,jaribu kumkwepa.kama unavyosema ni mcha mungu,mmwagie mistari ya kidini dini
   
 7. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Umesha vuka maji marefu sasa almost uko upande wa pili ndio uzame tena?
   
 8. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  We ni mtu wa ajabu, kwanza nadhani siyo mkweli hivi kitu kiwe chozi kweli unaweza kukiacha halafu demu hadi zana amekwekea ili usije fikiria anataka kukuua!!!!!

  Kweli kwenye miti hakuna wajenzi!!!!=

  Na huyo mchumba wako mmesha do au ndiyo ujapiga soga bado??
   
 9. M

  Mwanyava JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu, yataka moyo!! Kama mtu kavua kila kitu na ukafanikiwa kutii nafsi yako ya "hapana" basi yakupasa ufuate nafsi inasemaje maana hapa tutakushauri mengi mazuri na wengine ...

  Funga na umuombe Mungu akuonyeshe mke wako!! Usifanye maamuzi kwa kufuata tamaa za mwili wako istoshe ulivuka mtihani mmoja!!
   
 10. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Jihesabu hauko normal kiume ! Ktk hatua uliyofikishwa na uka'resist kung'wenya ! Salute !
   
 11. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  duh!!! aibu!!! sasa mie naona hapa nikumkojolea nakusepa.
   
 12. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Una uhakika gani kama hao wengine anawakataa? Kwa hiyo na hizo kondomu zote alikuwa amekuwekea wewe tu??
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Halafu ni kusadikika kwa mtu asiefanya hayo mambo kukuingia namna hiyo> Huyo ni mzoefu bora umkibie!
   
 14. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Acha kutuzingua babu na vijistori vya kutunga
   
 15. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #15
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mchape nao acha kuremba dogo...
   
 16. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #16
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Km kweli hujamtafuna,nakusieu sn coz ni wanaume wachache sn wanaoweza kuchomoka kwenye huo mtego,na km kweli unampenda huyo mchumba wako cdhan ungeendelea na urafiki na huyo bint baada ya tukio lile!ishinde tamaa tulia na mchumba wako!
   
 17. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #17
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  ......Hii nayo sifa ya Mcha mungu??
   
 18. D

  DOOKY JF-Expert Member

  #18
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  umeshazini tayari kwa kumuangalia, maliza mchezo ili ujenge heshima alafu achana naye, la sivyo atakudharau sana.

  maliza mchezo kaka, tena huyo ana akili anamipira ya condom hujui kwamba yuko serious na afya zenu
   
 19. b

  big bos New Member

  #19
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hebu tafuta soft copy za vitabu vyake vya dini vya kumcha bwana uweke apa labda namimi naweza ingia kwenye dini yake labda ayo ndo mafundisho wanayopewa kwenye kanisa lao sijui msikiti?

  ila we mzima kweli?
   
 20. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #20
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  We inaonyesha unataka kula mzigo ila unataka upate namna ya kuondoa Guilt conscious baada ya kumsaliti mpenzio. Wanawake huwa wanatega ila huyo kazidisha, ametumia 'bomu' siyo nyavu.
  Kama unataka kumwepuka mwambie ukweli kwamba una wako, na mkatie mawasiliano. hizo story kwamba anawakataa wanaume ni sound 2 , soma alama za nyakati mkuu.
   
Loading...