nimsaidieje ndugu yangu huyu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nimsaidieje ndugu yangu huyu?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by noella, Jan 23, 2012.

 1. n

  noella Senior Member

  #1
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Wapendwa natumai mlikuwa na weekend njema.
  Naandika kwa niaba ya cousin yangu ambaye tumetokea kuwa ndugu pamoja na marafiki sana. Anahitaji ushauri. Swala hili limemtokea jana na hivi sasa kachanganyikiwa hata kazini amegoma kwenda.
  Alikuwa kwenye mahusiano kwa miaka saba na ana mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano. Siku zote wako kwenye uhusiano mkaka ameonyesha kumjali na kuwa hakuna mwingine zaidi yake. Mwaka huu walikuwa wamepanda or rather yule mwanaume alimwambia kuwa atakuja kutoa posa hivi karibuni kwenye mwezi wa tatu. Dada anajulikana na ukoo mzima wa mwanaume alimpeleka kwa mara ya kwanza kijijini kwao mwaka jana disemba.
  Sasa basi,tatizo ni kwamba,jana katika maongezi yao,kijana akatamka ninanukuu "kila ninayekuwa nae tunaendaa wee lakini namwona puu wewe ndio my best hakuna anayekukuta". Mdada akapaniki kumbe muda wote huo jamaa alikuwa anamchora,kumbe alikuwa akidate wanawake wengine!kumbe alikuwa hayuko serious nae!anajiuliza ya kuwa what if angepata mwenye sifa anazotaka si ndo angemdump for that somebody. Jamani cousin yangu alichofanya ni kumfukuza kijana wa watu na kumwambia aende akaendelee kusearch. Anasema kinachomuuma ni kuwa kuonwa mjinga,ina maana kijana angekaa kimya tu asiseme si maisha yangeendelea kwa nini amwambie.
  According to binti ni kwamba kijana kamwambia anachojua yeye anamuhitaji kwenye maisha yake. Binti kawa mbogo hataki kumsikia na jamaa kamwambia kuwa anamtesa mtoto kwa ajili ya ujinga wake na kama ameamua hivyo basi hataki hata kumuona mtoto akikua atamtafuta baba yake na akiumwa asimwambie afe nae mwenyewe kwani ana card ya medical insurance. Binti kachanganyikiwa atamsomeshaje mtoto peke yake. Ameona wanaume wote ovyo haamini tena mwanaume anasema ataishi single for the rest of her life.
  Kwa kweli mimi naona amekata tamaa ya maisha ndugu yangu huyu mana hata kazini leo amekataa kwenda yupoyupo tu kama mjinga haongei na mtu hataki kula halii,afadhali angelia ningejua moja uchungu unatoka but ye anatoa macho tu.
  Jamani nisaidieni cha kumshauri huyu my dearest cousin sitaki kumpoteza. Anajiuliza sijui arudi for the sake ya mtoto ila hapohapo anasaema hatosahau. Hadithi ni ndefu ngoja niishie hapo kwa sasa nawahi job mie. Mchango wako wenye busara utamsaidia huyu binti. Shukran.
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Jamaa kaamua ku confess, nadhani mdada alitakiwa ashukuru Mungu na maisha yaendelee. Alichokifanya ni kususa, nashauri amrudie Jamaa.
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Muambie achukue muda kutafakari na kufanya uamuzi. Hahitaji kuamua leo na asubuhi hii, alishamfukuza yeye aende kazini. Akitoka kazini atafakari anachotaka, kutoenda job si ndo ndoto zote anazizimisha sasa?
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mwache tu ashukuru na waendelee kuishi kwa ajili ya mtoto. Yeye pia ana makosa mahusiano ya miaka 7 na hamjaonana, yaani ningekuwa mimi ningeshasepa zamani kuliko kuupotezeana muda, 7 years yaani muda wote huo inamaana jamaa alikuwa not ready for commitment ?

  Wanaume bana!!
   
 5. n

  noella Senior Member

  #5
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Jamaa anasema alikuwa anatafuta maisha kwanza hakuwahi kufikiria kusettle na kuoa until last week na ni bora aseme ukweli,na on the process bado alikuwa anatazama nje kama kuna anayemfaa kuwa mke zaidi ya cazo. Mwe!!nimemuacha kitandani cazo kagoma kwenda job anawaza kumwachisha mtoto shule aliyopo amtafutie nyingine ambayo anaweza kuafford. Namuombea kwa Mungu,mmh!
   
 6. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Mpe pole nduguyo,
  Ila mwambie tu avumulie arudiane na bwanake walee mtoto, kama maamuzi hayo magumu ya kuachana ilibidi achukue kitambo kabla hajazaa ila sasa hvi ni too late.
  :A S-coffee:
   
 7. salito

  salito JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  mhh huyo mwanaume nawasiwasi na akili zake,sasa wamegombana wao mtoto kaingiaje???alikuwa anatafuta sababu na mtoto alimuona kama mzigo,nduguyo akae akijua baba mtu hana mapenzi na mwanae,mapenzi ya baba na mwana yameshikiliwa na penzi lake yeye kwa baba,ni sawa kabisa amuhamishe mtoto shule ampeleke atakayoweza kulipia ili litakalotokea akabiliane nalo,na swala la kuendelea na huyo mwanaume o kumuacha ausikilize moyo wake..
   
 8. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  sasa kuna baya gani hapo? si jamaa amemueleza ukweli tu? na jamaa si ndo kaamua kuwa huyo cousin wako ndo anafaa kua mkewe ndo maana wanaenda kutoa mahari na kufanya taratibu za kufunga ndoa? mwambie arudi kwa mwenzie waongee wayamalize.

  wenye ndoa zao tu wanaibiwa sembuse girlfriend na boyfriend

   
 9. h

  hayaka JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ni jambo la kushukuru mungu kupata mwanaume ambaye anakubali kusema ukweli. wanaume wengi ni walagai. sioni anachokisusa hapo ni kipi ilihali akipata mwingine mchezo ni uleule. hakuna binadamu ambaye ni mkamilifu. amrudie jamaa na maisha ya songe mbele.
   
 10. h

  hayaka JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ningekuwa mimi ningejifagilia mbaya, kumbe jamaa kazunguka kote na hakuna wa kunizidi!
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  La mwambie arudi tu wafunge ndoa waanze maisha katika wengi kachaguliwa yeye na imani jamaa atabadirika caiuse kaongea mwenyewe kwa kinywa chake
   
 12. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  sasa hapo alipenda kuambiwa au kusifiwa kwa aina gani?? anasifiwa analaumu na kuachana na mtu
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  huyo cousin wako anahitaji to grow up
  wapo wanaoambiwa moyo wangu haupo kwako
  na kuoa ii tu mtoto asiteseke
  yeye angefanyaje hapo
   
 14. n

  noella Senior Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Yaani makubwa haya,jamaa nae eti hajaenda kazini analewa tu nyumbani ananambia my cousin anamfrustrate anaharibu plan zake za maisha zote. Hahaha ama kweli mapenzi kizunguzungu.jamaa ananambia ni ukweli nimemwambia hivyo sasa yeye si angefurahi amewin game. Hahaha kweli mapenzi hayana mtu mzima.
  Nilichoweza kumwambia my cazo aingie Jf asome maushauri hapa na aburudike badala ya kulala na kutoa macho nyumbani. Asanteni kwa michango yenu wapendwa.
   
Loading...