Habarini wana jukwaa?
Nina kaka yangu amegeuka kuwa mlevi wa kupindukia kiasi cha kwamba akiamka anaamka na pombe mpaka analala yupo na pombe siku saba za wiki.
Wazazi wamejaribu kuongea nae kwa namna zote lakini imeshindikana, hata majirani na ndugu wa karibu kama wajomba wamejaribu kuzungumza naye kama hawezi kuachana nayo japo apunguze lakini imekuwa kazi bure.
Naishi mjini yeye anaishi kijijini, kila ninaporudi kijijini watu wananitazama mimi kwamba ndiye pekee naweza kulitatua hilo tatizo, name nimeshaongea sana mara nyingi na huwa ananiahidi kuachana nayo kabisa lakini nikiondoka tu nyuma anarudia tabia yake ile ile.
Kuna wakati mama alikwenda mpaka kwa sangoma akiamini huenda bro amerogwa lakini hakuna kilichobadilika mwendo ni ule ule pombe na yeye, yeye na pombe
Naombeni ushauri wenu wanaJF nifanyaje kumsaidia kaka angu, kama sio kuacha basi hata kupunguza tu.
NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU