Nimsaidiaje aachane na ulevi wa kupindukia

Habarini wana jukwaa?

Nina kaka yangu amegeuka kuwa mlevi wa kupindukia kiasi cha kwamba akiamka anaamka na pombe mpaka analala yupo na pombe siku saba za wiki.

Wazazi wamejaribu kuongea nae kwa namna zote lakini imeshindikana, hata majirani na ndugu wa karibu kama wajomba wamejaribu kuzungumza naye kama hawezi kuachana nayo japo apunguze lakini imekuwa kazi bure.

Naishi mjini yeye anaishi kijijini, kila ninaporudi kijijini watu wananitazama mimi kwamba ndiye pekee naweza kulitatua hilo tatizo, name nimeshaongea sana mara nyingi na huwa ananiahidi kuachana nayo kabisa lakini nikiondoka tu nyuma anarudia tabia yake ile ile.

Kuna wakati mama alikwenda mpaka kwa sangoma akiamini huenda bro amerogwa lakini hakuna kilichobadilika mwendo ni ule ule pombe na yeye, yeye na pombe

Naombeni ushauri wenu wanaJF nifanyaje kumsaidia kaka angu, kama sio kuacha basi hata kupunguza tu.

NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU
Cha kwanza ni kushughulikia mazingira yake, kujua sababu na vichocheo vya ulevi wake. Tatueni chanzo cha ulevi wake (Migogoro ya ndoa, msongo wa mawazo, kuachishwa kazi, migogoro ya kifamilia, kukosa kazi nk) kisha muwekeni mbali na vichocheo vya ulevi wake (marafiki walevi, kukosa kazi za kufanya, kukosa viburudisho mbadala, vilabu kuwa karibu yake nk). Baada ya hapo sasa munaweza kuanza kumuachisha kwa urahisi.

Kuacha pombe ni hiari ya mlevi mwenyewe, kwa hiyo semeni na akili yake na moyo wake. Mukifanikiwa kubadili akili yake na moyo wake basi mazingira ya kumuachisha yatakuwa yanafaa na atapunguza au kuacha kabisa.

Pia kuna dawa kwa ajili ya kumvunja moyo kila akinywa na atalazimika kuacha ili kukwepa athari anazopata kila akinywa pombe huku akiwa anatumia hiyo dawa na ataacha FOREVER!

Naomba niishie hapa, ila kama ukihitaji zaidi niambie niongezee nini (Ila sio jina la dawa 😀😀😀 maana athari zake zinahitaji uangalizi wa karibu, cheki na daktari hospitali iliyo karibu na wewe)

Good day!
 
Mkuu mimi nina dawa ambayo ukimpatu pombe ataacha maramoja akinywa pombetuu atatapika yote
 
Ni yupo hivyo tangu zamani au kaanza sasa hivi? lazima kutakuwa na sababu, na ili uweze kumsaidia ni lazima ujue hiyo sababu au chanzo cha hiyo tabia
 
Cha kwanza ni kushughulikia mazingira yake, kujua sababu na vichocheo vya ulevi wake. Tatueni chanzo cha ulevi wake (Migogoro ya ndoa, msongo wa mawazo, kuachishwa kazi, migogoro ya kifamilia, kukosa kazi nk) kisha muwekeni mbali na vichocheo vya ulevi wake (marafiki walevi, kukosa kazi za kufanya, kukosa viburudisho mbadala, vilabu kuwa karibu yake nk). Baada ya hapo sasa munaweza kuanza kumuachisha kwa urahisi.

Kuacha pombe ni hiari ya mlevi mwenyewe, kwa hiyo semeni na akili yake na moyo wake. Mukifanikiwa kubadili akili yake na moyo wake basi mazingira ya kumuachisha yatakuwa yanafaa na atapunguza au kuacha kabisa.

Pia kuna dawa kwa ajili ya kumvunja moyo kila akinywa na atalazimika kuacha ili kukwepa athari anazopata kila akinywa pombe huku akiwa anatumia hiyo dawa na ataacha FOREVER!

Naomba niishie hapa, ila kama ukihitaji zaidi niambie niongezee nini (Ila sio jina la dawa 😀😀😀 maana athari zake zinahitaji uangalizi wa karibu, cheki na daktari hospitali iliyo karibu na wewe)

Good day!
Ongeza kwenye KIBURUDISHO MBADALA na pia naomba kufahamu Zaidi kuhusu hiyo dawa na uangalizi wake japo umenizuia kukuuliza NIVUMILIE 😀😀😀😀
 
Habarini wana jukwaa?

Nina kaka yangu amegeuka kuwa mlevi wa kupindukia kiasi cha kwamba akiamka anaamka na pombe mpaka analala yupo na pombe siku saba za wiki.

Wazazi wamejaribu kuongea nae kwa namna zote lakini imeshindikana, hata majirani na ndugu wa karibu kama wajomba wamejaribu kuzungumza naye kama hawezi kuachana nayo japo apunguze lakini imekuwa kazi bure.

Naishi mjini yeye anaishi kijijini, kila ninaporudi kijijini watu wananitazama mimi kwamba ndiye pekee naweza kulitatua hilo tatizo, name nimeshaongea sana mara nyingi na huwa ananiahidi kuachana nayo kabisa lakini nikiondoka tu nyuma anarudia tabia yake ile ile.

Kuna wakati mama alikwenda mpaka kwa sangoma akiamini huenda bro amerogwa lakini hakuna kilichobadilika mwendo ni ule ule pombe na yeye, yeye na pombe

Naombeni ushauri wenu wanaJF nifanyaje kumsaidia kaka angu, kama sio kuacha basi hata kupunguza tu.

NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU
Pole sana ndugu kwa changamoto hio. Anatumia Pombe za aina gani hasa?
 
Mwambie mke wake kama ananyonyesha akamue maziwa yake ,achemshe chai ya maziwa ya ng😱mbe ikiiva aweke maziwa yake kwenye hiyo chai ya maziwa ( robo Lita tu).

Akimaliza ampe anywe hiyo chai na ahakikishe asijue iwe siri yake na wewe.

Atakuwa kila akinywa pombe anaitapika kila akinywa anatapika.

Mwisho ataiicha

Utaleta mrejesho humu humu
 
Mkuu kama ujuavyo hii ni kazi yangu hivyo utapaswa kuchangia garama kidogo sijui kama utakuwa upo tayari kuchangia,
Hamna shida kama naimudu nitachangia tu. Kikubwa tatizo litatuke
 
Kwanza kabla hujaingilia undani wa tatizo hilo jua chanzo chake. Mwanaume huenda kulewa ili aweze kumkabili mwanamke. "Germany Courage." Yaani anajionaga duni kwa mwanamke flan hivi.
Ka si hivyo; Je kaoa? Ka bado, ana kiba100 hivyo anaogopa ukijaoa weye mdogo na yeye bado bado watu watamgundua. Mtafutie mke umfungie ndani naye
 
Back
Top Bottom