Congo
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 2,079
- 2,334
![]()
Kwa maana hiyo BILIONI 90 ni kwa ajili ya construction ya shule na kujaza fenicha na kila kitu
sasa watu wa huko kwao wanasema BILIONI 90 NI ESTIMATE ZA CHINI mno
Sina picha za hizo shule lakini kama kweli kaiba na kisha mapesa yenyewe kajenga shule Tanzania na inasemekana kazikabidhi serikali ambayo imeshindwa kuziendesha....mnasemaje wakuu?
sasa kama mapesa yote hayo yametolewa kwa wananchi jiulizeni kiasi gani jamaa kaweka nje ya nchi?
Hivi kweli mtu kama Ndesamburo anaweza kumfikia Mkono kwa investment ya elimu aliyofanya huko Musoma?
mkipata picha zileteni
Ohh I should point out ni PESA ZAKE BINAFSI....na kwa sababu hajawahi kuhukumiwa na chombo chochote cha sheria I assueme ni pesa halali
Mimi sikubaliani na maelezo haya kuhusu kiasi kilichotumika (billioni 90). Haiwezekani hata kudogo. shule hizi ni za kawaida kabisa. sio za gorofa. Ujenzi wa mtu binafsi ni tofauti kabisa na ujenzi wa serikali ambapo bei ya kitu inazidishwa hata mara 3.
Bwana Mkono alijenga kama mtu binafsi, hivyo gharama zake za ujenzi zilikuwa za chini hata kama alitumia contractor. Mimi sio mtaalamu wa ukadiriaji majengo lakini ukweli unabaki kuwa sio fedha nyingi kiasi hicho kilichotumika.
Bado siamini kama kila shule ilitumia bilioni moja. Ndugu zangu kama zile shule zimetumia kiasi hicho cha pesa basi yule bwana anayemiliki St. Mathew iliyoko Kongowe atakuwa trilionea.
nazifahamu shule tatu zinazozungumziwa ni uzushi wa ajabu. naweza kukubali tu kama utasema shule moja imetumia millioni 90. hapo ni pamoja na kuweka vifaa vyote. tazameni majengo hayo kwenye website yake ya http://www.musomarural.org