Nimrod Mkono aitisha CCM

Hivi CCM kuna wenye sifa kweli? Mie naona wamebaki kupeana uongozi kwa makundi.....ila sifa hapana!
Wanaangalia sura ndo sifa yao kuuGombea na mama salma ujumbe wa nyumba kumi uone
 
Sasa kama baba dhaifu, unategemea familia itakuwaje?
 
Mkono alitia mkono wake kwenye daftari la Zitto pale mjengoni. Asishangae atakapoona hata uenyekiti wa mtaaa hapati. Ndiyo uzuri wa magamba. Ukileta fyokofyoko unaadhibiwa immediately. Wanachotaka wao ni wanachama kuendelea kuwa royal kwa viongozi hata kama hawaridhiki na utendaji kazi wao.
 
Huyu si ni mmoja wa wafadhili wa magamba na ana kiburi cha fedha (jeuri yake anaijua Maregesi Abiud-Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi CCM pale alipojaribu kupenyeza jina kugombea kupitishwa na CCM kugombea ubunge Musoma Vijijini). Huyu mzee CCM wanamgwaya, watamuomba radhi tu maana ni GAMBA gumu
 
Nimrodi siyo tu amekula fedha za Umma akisaidana na CCM, bali anajua madudu mengi ya CCM na viongozi wake. Mkwara huu ni kama ule wa Lowassa kule kikaoni Idodomya! Sasa wakimwaga ugali (kumwengua) atamwaga mboga (kuanika mabaya yao), kitu ambacho sidhani kama CCM wako tayari!
 

Hi wakati wa ujio wa vyama vingi Mkono alikuwa wapi?
 
Kwako Mchambuzi, heshima mbele.

Nimeridhika sana na ukomavu na weledi wako katika kujibu hoja za mleta mada husika.

Mimi sio gamba na wala sijawahi kuwa gamba; mimi nilkuwa mmoja wa wale waliokuwa wanatia alama ya vema kwenye kivuli/giza (in general elections) enzi zile za chama kushika hatamu!

Ila uliyobainisha ni mapungufu ya muda mrefu sana NDANI ya CCM na kwa ujumla ya demokrasia nchini Tanzania toka awamu ya kwanza. Athari za ukosefu huo tuliziona mapema wakati wa mchakato wa kura za maoni za vyama vingi 1990-92. Sheria nyingi na mienendo ya serikali haikuashiria ukunjufu wa moyo ktk kukubali mfumo shindanishi wa vyama vya siasa. Ndio maana yale mambo muhimu sana ya Tume ya Nyalali yalipuuzwa. Kifupi ghiliba na hiana vilionekana na madhara yake ni kuwa na sheria mbovu za vyama vya siasa na ile ya uchaguzi.

Ila nitaomba kutofuatiana nawe kidogo kuhusu mirija ya mapato CCM kupata fedha. CCM kwa kuliona hilo na kwa hila nyingi walijimilikisha mashamba, miradi ya umma, majengo na hata viwanja vya michezo kwa lengo moja la kuhodhi mirija ya mapato. Baada ya siasa chafu za fedha na makundi kushika kasi (kama ulivyoeleza kwa ufasaha), siasa ndani ya CCM zikawa ni uwekezaji (investment politics) wenye lengo la faida na mrejesho (profit and return on investment basis).

Na kwa vile mchezo/mfumo wa fedha (haukuweza) kuthibitiwa na uongozi wa CCM (kwa sababu tofauti tofauti) ikabaki kuwa ni "demokrasia ya fedha". Muda huo watu walijua kuwa hakuna "fair ground" kuwawezesha kutimiza malengo yao ya kisiasa ndipo "mwanya na mfumo wa ufisadi tunaouona ukaasisiwa rasmi". Yote ni ktk kuongoze upana wa mirija ya mapato ya CCM, EPA, KAGODa ni mifano michache.


Iko sababu nyingine nitaitaja bila kuielezea, kuporomoka na kufa kwa mfumo wa kijamaa na hasa USSR. Hii ilkuwa na impact sio tu ktk vyama bali chumi na nchi zilizokuwa zimeegemea upande. Hilo lilibadili kwa sehemu itikadi na msimamo wa baadhi ya wajumbe......ndio maana walipoenda Z'bar kilifuata ni historia. Lakini wale wajumbe hawakubadilika walipokuwa Z'bar, bali walihitimisha tu kilichokuwa mioyoni mwao
 
Nimrod Mkono ni mmoja wa ma King Makers wa CCM. Kama 'Amepigwa chini' basi mjue hata hao ma King Makers wana mpasuko


Remember the thread kuna kundi jipya la urais....Na akina makongo mahama's kesi..Nchi hii kizungu zungu kweli! Watu wanapunguza vihunzi....Ukizoea kula nyama za watu hutaacha Nyerere said..Akubali tu zamu yake imefika
 
si ni huyu mzee alisign hoja ya zitto kwamba waziri mkuu ni dhaifu.... kashasahau? haya ndiyo matokeo yake - tena akiwaudhi zaidi watamfirisi.
 
Niliwaambia hali ilivyo CCM wana kitendawili cha kutengua( ama mgombea awe mzigo ama chama kiwe mzigo ama vyote kwa pamoja) na si vinginevyo.CCM ndio kifo cha jumla.Kam na huyu mzee naye yumo sijui watamshawishi vipi asubiri miaka mingine kuanzia 5 na kuendelea.Kila mtu umri wake umemtupa mkono na hawana hakika ya kuikuta CCM baada ya miaka 5.

Wapo wapi akina pasco na mchambuzi na Mkandara waje na big theory(doing things right,doing right thing).Siku zinavyoenda CCM inagain momentuma kuelekea to the hell wazee wanamchawasha (akina 6),chadema wana uhuru wa kuwapisha au wawapishe na kuwaongea rollon/spin ili wawahi kuzimu.
 

There is no FUTURE for CCM, there is only PAST & PRESENT;
 
There is no FUTURE for CCM, there is only PAST & PRESENT;

Nawe umeona hilo,ila bado wanaevolve cha kusubiri ni how watabadilika na jinsi gani watakuja kuanza safisha damages kabla uchaguzi haujafika.Pia kuweza reebisha mioyo ya wataokosa.

By the way JK muda unayoyoma,unakuja ule muda wa panic kila kitu hakijakaa sawa ili kujiandaa kuondoka ikulu.hakuna tena nafasi ya kujenga nchi wala kumalizia ahadi zaidi ya kuja pga watu porojo kuwa fulani atamalizia.CDM watakuna na game itakayowafanay wananchi wajisikie guilty kwa kupigia CCM hata pale Dr. slaa alipowaonye kuwa watajutia sana uamuzi wao.
 
ccm ni janga katka kuliko hata ukimwi taifa le2....
 

Mchambuzi: Asante sana kwa maelezo mazuri yanayotia moyo kuwa bado kuna matuamini ya kubadilisha hii hali ya kisiasa iliyopo hapa nchini. Kama ulivyosema matatizo yote matano uliyoainisha yanasababisha nchi kuyumba. CCM kama chama kikubwa na chenye uzoefu kilitakiwa kiwe mfano wa kuigwa na hivi vyama vingine vya siasa lakini hali ni tofauti kabisa. The problem with this is the ill political residual effect that is within the nation. Siyo rahisi kuzalisha viongozi wa kisiasa wazuri hata katika vyama vya upinzani kwa kuwa wananchi wamelelewa katika huu mfumo mchafu. Hata kumlaumu Kikwete kuwa uongozi wake una matatizo ni kumwonea because the system is sick. What can he do as an individual in a ruined political environment??

Siku isiyo na jina na ije ili viongozi wanasiasa wakae pamoja wakubaliane kuwa ile sheria ya uchaguzi ibadilishwe ili ifanye kazi katika misingi ya haki na kweli vinginevyo ni shida tu
 
Mkuu Mchambuzi nashukuru kwa hoja mujarabu. Nilijua tu nitapata kitu toka kwako. Umenena vyema kuhusu matycoon wa CCM ambao inaonekana ndio wanakivuruga chama. Lakini nakumbuka kwamba matycoon walikuwepo tangia enzi za TANU wakichangia Chama lakini hawakuwa wakikemea na kuvuruga chama. Hivi watu kama akina Rupia enzi hizo si walikuwa matycoon ambao walifikia hata kumapatia mwalimu nauli ya kwenda UNO pamoja na kumpangia nyumba ya kuishi jijini lakini hawakuwa na makeke kama haya? Akina Al nuur Kasum vipi wao hawakuwa wachangiaji wa chama kweli?

Haya tukija miaka ya tisini ndipo hapo nakumbuka wale pace makers nao waliamua kuingia kwenye chungu kuona kuna nini humo. Kumbuka yule pace maker wa Ifakara akiitwa Abbas Gulamali na akina Biku mbona wao hawakuwa kama hawa wa sasa? Nadhani kuna shida nyingine kubwa zaidi ya huu utycoon. Hivi tunaweza kusema kwamba CCM ina mkemeaji ambaye anaweza kusimama na kukemea na watu wakamsikia siyo kwa ukali wa sauti yake bali kwa historia na usafi wake?
 
Last edited by a moderator:

Gulamali alikuwa muuza na mtumia unga chini ya ulinzi wa CCM.Mkono ni mwanasheria wa deal zote halali na haramu chini ya serikali ya CCM.Yaani anayo Carrot and Stick .CCM wachague.

Ningependa issue za Nyerere kuchangiwa nauli sijui na suti zisiwe issue sana,kwani kila mahali tunaambiwa hayo.Hata Ndesa alichanga...ila iliingia TANU halafu chama kikapanga,na huu ulikuwa mchango wa matajiri na masikini kama itolewavyo sadaka.Hizo za kupeana pembeni huwezi jua km Nyerere alitumiaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…