Kaka ya shangazi yako anakuwaje mjomba wako tena?🤔
Kaka wa shangazi yako ni aidha baba mkubwa au baba mdogo wako,wewe amekuwaje mjomba tena?
Ndugu zangu, mkiona tunakemea malezi ya upande m'moja madhara yake ndio haya sasa.
Watoto wanaozaliwa na kulelewa upande m'moja tu yaani upande wa mama huwa hawanaga mipaka na hawajui vibaya.
Huyu sasa ni dhahiri kuwa amelelewa upande wa mama yake tu na hayupo karibu na upande wa baba yake kiasi kwamba anaona ndugu za upande wa baba yake ni halali yake kuingiliana nao kimwili.
Huu ndio upuuzi wa malezi ya kiholela ambapo watoto wanakuzwa na ukoo nusu na hawajui nusu nyingine ilipo na mbaya zaidi wakikutana wanakuwa hawa taarifa kamili za misingi ya uzao wao na asili yao.
Haya sasa yataendelea sana kutokea especially nyakati hizi ambazo wanawake wanajizalia tu kama bata na wanaume kisha wanatelekezana mwanaume mtwara mwanamke kigoma na hawajuani koo.
MUNGU atutetee