Nimjibu vipi anielewe?

Nimjibu vipi anielewe?

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,369
Reaction score
27,785
Habari wanaMMU,


Ni hivi, wakati nikiwa chuoni nilitokea kumpenda binti mmoja mzuri, toto la Kipare.Katika maisha yetu ya pale chuoni tulikuwa tukishirikiana kwa kila hali, iwe kimaisha na hata kimasomo pia.Ilifika wakati ikabidi nivunje ukimya na kumtakia lililokuwa moyoni mwangu, alichukulia masihara nilipomwambia kwamba nampenda na yeye akadai kwamba hawezi kuwa mpenzi wangu ilhali yeye kanizoea mimi kama kaka yake.

Nilipoona msimamo wake umekuwa mkali basi nikaamua kutupa karata yangu kwa msichana mwingine wa palepale chuoni ambaye kiukweli alinielewa na tukaanzisha naye mahusiano. Nilitangulia kumaliza chuo nikamuacha bado akiwa masomoni.Sasa cha kushangaza siku ya Leo nimepokea message kupitia akaunti yake ya Whatsapp akiwa amenitumia picha ambayo ameidownload kutoka kwenye profile ya huyo mpenzi wangu ambaye walikuwa wakisoma wote akiniambia " Unajua hii picha nimeitoa wapi? Nashukuru Mungu niligundua hunipendi".

Wakuu sijamjibu chochote mpaka dakika hii na ikumbukwe nikiwa chuoni sijawahi mtongoza msichana yeyote kabla yake, nilikuja kuanzisha mahusiano na msichana huyu wa sasa baada ya yeye kunikatalia.Nashindwa kujua ana lengo gani ilhali alishanikatalia tangu mwanzo na mimi nikayaheshimu mawazo yake.Nahitaji ushauri wenu namna gani nitamjibu kwa busara anielewe pasipo kumkwaza au kumgombanisha na huyu mpenzi wangu.

Natanguliza shukrani, samahani kwa habari ndefu
 
Hisia huwa zinabadilika kadri siku zinavyobadilika
so hakukupenda then...lakini now hisia zimebadilika...
kazi kwako kusuka au kunyoa...

Duh mkuu, nimekunyaka kwa mbali sana, unataka kusema ame regret maamuzi yake ya awali....
 
Duh mkuu, nimekunyaka kwa mbali sana, unataka kusema ame regret maamuzi yake ya awali....

hebu jitathmini, swali gani hapo unalotaka usaidiwe ambalo hujui jibu lake?
hujui alipoipata hiyo picha?
mbna kwenye maelezo yako umetaja?
 
Jamaa utakuwa Pendapenda

Unampenda huyu unamtokea akikuzingua huchukui muda mrefu unampenda mwingine
 
Back
Top Bottom