Nimfanyenini huyu mwanamke?

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,213
56,849
Ni chibonge hivi ila mzuri. Leo nilimkaribisha apike tule, tunywe baadaye tufanye. Sasa wakati anapika mi nilikuwa sebuleni nimetulia Niko nalipensi langu la kupungia upepo huku nikiwa kifua wazi.. nikaona isiwe tabu nikamfata hukohuko jikoni ili tuzungumze kidogo n.k

Nilikuwa na glass ya juisi cola nikaibebelea moja kwa moja mpk jikoni.. ye hakuniona nikaenda nanyata kimahaba! Mpk nikamfikia hajashituka si nikamtekenya!

Asalalee vibonge nyie ni wauwaji!.. hata hajageuka wala nini kabebelea limwiko ambalo lilikuwa kwenye ujiuji wa ugali unaotokota!.. ile narudi nyuma huku nikitabasamu ghafla nikashangaa limwiko lenye miuji ya moto linatua kwenye kakitambi kangu ka minyoo!! Komamanga wa watu nikatoa ukelele mpk masikio yangu mwenyewe yakaanza kulia nzwiiii

Hilo halikutosha wakati nakimbia ile nageuka tu nimemuachia mgongo nikasikia pigo jengine la mwiko katikati ya mgongo!!.. sikuwahi kujua kuwa ninauwezo wa kujikunja mithiri ya nyoka!.. na pia sikuwahi kujua kuwa ninamikono mirefu inayoweza kushika mgongo kwa mipapaso ya kujikamua Kama unavyoweza kukamua nguo!! Tabu haikuwa mwiko tu tabu ilikuwa ule ujiuji wamoto! Ndugu zanguni nilianguka nikaanza garagara kama kambare wa hamida!.. nashukuru ule mpensi wangu walau ulinisitiri!

Yule chibonge alibaki akinitazama tu nilivyokuwa nikigaragara hovyo! nisiwachoshe alibaki kazubaa tu baada ya dk moja nikaamka nimefura huku nimetapakaa juisi kola maana ilimwagika.

Nilichomfanya nilimkamata nikamfunga kamba nimemuweka reserve najitibu kwanza majeraha.. Sasa chaajabu haombi msamaha nilijaribu kumtia vibao kadhaa akawa anapiga kelele mpk nikawa naona kidaka tonge mdomoni mwake!. Na sio kukiona tu kilikuwa mpk kinatikisika!..

Nipeni ushauri nimfanye nini huyu chibonge maana kaniharibia weekend? Nataka adhabu murua ili nimrudishe kwenye mstari.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣lmao

Kenzy kaka angu una matatizo🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣i diee
Sasa mi tatizo langu hapo likowapi..??
 
.


Wallah mecheka kam pimbiii

Ila mkuu mtoe out muende mkapige k vant nakuja lipia ee
Kama ndani tu nimechezea Miko huko out kwenye siraha kedekede sijui tu..! Hatoki mtu out leo ni ndani tu mpk kieleweke
 
Kiutani utani mtauana kijinga jinga tu. Hebu fikiria ungeangukia kichwa??!!! Unamkumbuka Kanumba???
 


Kwa namna ulivosimulia, niko hoi,hata vidole havina nguvu ya kuandika


Msamehee tu chibonge alikasirishwa na ka mchepuko kake baada ya wewe pia kumuudhi alipokuta meseji ya ka hawala kako.

Sasa alikua ana hasira kotekote.
 
Back
Top Bottom