HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,569
Mimi ni mtanzania mwenye jinsia ya kiume nina umri wa miaka 33, nina tatizo lina nipa shida katika maisha naomba ushauri wenu wana JF. nlipata msichana ambae alikua amezalishwa na mwanmme asiyekua na msimamo wa maisha na yeye msichana akiwa kaishia kidato cha nne na matokeo mabovu....tulipendana na na huyo mwanamke nikawa na matarajio ya kufunga nae ndoa japo alikua na mtoto, ili awe mke mwenye manufaa nikajitolea kumpeleka shule akachagua chuo cha wanyama pori ambacho ni bei mbaya na kinalipiwa kwa dola, kipato changu ni kidogo ila nikajitahidi kujibana kumuandikisha hapo chuo na kutokana na kutokidhi kiwango cha kujiunga na chuo akatakiwa kuanza na Foundation course ambayo nililipa zaid ya mil. 2 akajitahidi akafaulu na kujiunga na cheti mwaka 2008, kwa bahat nzuri baba yake mdogo akasaidia kuchangia ada hadi akamaliza cheti, mungu akasaidia akapatikana mfadhali wa kumsomesha toka marekani ambapo alimlipia ada ya Diploma aliyomaliza mwaka jana,na atamsomesha DIGRII.
katika kipindi hiko chote alinifanyia vitimbi vingi ambavyo nilivivumilia kiasi kikubwa, kwan alidiriki hadi kunisaliti lakini nilisamehe na kuvumilia kwani nilijua na kuwekeza kwake kua atakua mke wangu. mwaka huu amepata ajira serikalini ana mwezi wa 6 sasa cha ajabu amekua akinifanyia vitimbi vingi japo yupo mbali na mimi ila anavionyesha mfano mdogo ni kwenye sikukuu iliyopita amtoka kwenye kituo chake cha kazi na kwenda mjini kulewa akidai amelala chumba kimoja na rafiki yake wa kike na mumewe, kifadha hana msaada na huku anajua mim kwa sasa ni mwanafunzi chuoni.
WADAU NIFANYEJE?? NIMKWAMA MKE NATAKA ILA NDIO HUYO NMECHOKA JAMANI

Ningepata mvumilivu kama ww, loh. piga chini huyo hakuna mjadala.
kuna dem mmoja nilipiga chini faster baada yakungundua ni kirusi ndani ya maisha yangu alipata zero meta sec. Nikamtafutia chuo cha ufundi cha ajabu alipohitimu siku tu amepata cheti kesho yake na kutana naye nyondo ilikuwa kubwa sana nikamwambia wewe utakula jeuri yako nilimwapia nikamwambia cheti hakika hutakitumia alicheka sana nikamwambia nenda kakifiche kuanzia leo ila nitakuja kukichukua. nilikichukua hakuamini alipokuja kuangalia alipoweka hakukikuta kesho asubuhi alikuwa kwangu. Viatu miguuni vilikuwa vimeshindikana kuvaliwa, aliliya kama amefiwa lakini hakika cheti hakukiona hadi leo. na huo ndio ulikuwa mwisho wa mimi kuwa karibu nami.