Nimfanye nini huyu Mwanamke? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimfanye nini huyu Mwanamke?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tegelezeni, Dec 30, 2011.

 1. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mke wangu nimedumu naye kwa miaka minne sasa, katika ndoa yetu tumebahatika kupata mtoto wa kiume mmoja, na baada ya mtoto kutimiza miaka mitatu, tuliamua tupate mtoto mwingine. Tumefanya majaribio kadhaa kwa takriban miezi tisa lakini mke wangu hakushika mimba. Tukaenda kwa wataalamu na baada ya kushauriwa na kupewa tiba, ndipo mimba ikashika, lakini ilianza na matatizo na akahitajiwa akae Bed Rest.

  Wakati ujauzito wa mke wangu ulipotimiza miezi miwili, hivi karibuni akapata msiba wa kaka yake aliyemlea. Mimi sikuwepo mjini kwa sababu nilisafiri kikazi mikoani. Alinipigia simu kunipa taarifa za msiba na akanijulisha kwamba mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda kijijini kwao kwa mazishi. aliniaga kwamba na yeye atasafiri na mwili wa marehemu kwenda kuzika. Nilimshauri asisafiri kutokana na hali yake, na nilimuhakikishia kwamba nitakaporudi nitafanya utaratibu ili twende tukahani msiba. Alikataa katakata na akanioana mimi ni mbaya kwa sababu nimemkatalia kwenda kumzika kaka yake aliyemlea na kumsomesha. Nikamwambia aende lakini sitahusika na lolote litakalotokea akipata matatizo.

  Ni kweli aliamua kwenda lakini akiwa njiani alipata matatizo na ikabidi akimbizwe hospitai ya karibu na ule ujauzito ukatoka. Hakumudu kuendelea na safari na wala hakuhudhuria mazishi ya kaka yake. Nimezipokea taarifa hizi kwa uchungu sana. Sasa najiuliza nikirejea nimfanye nini huyu mwanamke?
   
 2. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,447
  Likes Received: 7,187
  Trophy Points: 280
  Asiyesikia la mkuu,msamehe tu,naamini hakutegemea kama ujauzito ungetoka.Akili yote iliishia kwenda kumzika kaka yake.BIBLIA INASEMA "ENYI WAUME ISHINI NA WAKE ZENU KWA AKILI MAANA NI VIUMBE DHAIFU"
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  ssa wewe hujui kwenye habari za msiba wanawake huwa wanafanya maamuzi ambayo siyo rational??????
   
 4. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  msamehe tu ujue mtu ukifiwa na mtu ambaye alikusaidia katika maisha yako lazima akili itachange ila pole sana mkuu then saikolojikali ameshaharibika wewe mtie moyo then maisha yenu yatakuwa na furaha tena
   
 5. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unajua swala la yeye kushika ujauzito lilitusumbua sana na lilitugharimu pia, inashangaza anachukua maamuzi ambayo sio kwamba yalikuwa yanahatarisha maisha ya hicho kiumbe, bali pia hata maisha yake! hivi alikuwa anatumia akili au matope?
   
 6. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  The Boss nakubaliana na wewe, lakini pale ambapo mume anatoa ushauri tena wa msingi halafu ukapuuzwa, basi hapo kuna walakini. Na huyu amekuwa mtovu wa nidhamu, kushindwa kumtii mumewe wa ndoa.
   
 7. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  Inaonekana una hasira sana mkuu.. just relax ndio yameshatokea hayo msamehe mkeo mkae pamoja mjaribu tena
   
 8. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,447
  Likes Received: 7,187
  Trophy Points: 280
  Hujawahi kufiwa na mtu aliekuwa wa muhimu sana maishani mwako?Mimba itashika nyingine tu.
   
 9. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  It is almost a week since happening, bado sija-relax tu!
   
 10. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Mkuu mpaka dakika hii mkeo ameshapata fundisho, unachopaswa kufanya kwa wakati huu ni kukubali yaliyotokea, kumsamehe kisha kuwa upande wake na kumpa moyo ili arejee katika hali yake ya kawaida..!

  Mapendo.
   
 11. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,447
  Likes Received: 7,187
  Trophy Points: 280
  Tena ikitoka mimba,nyingine inaingia kirahisi,SAMEHE!Anzaneni kutafuta nyingine
   
 12. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #12
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,118
  Trophy Points: 280
  Yaani mi nakuona wewe ni bonge la kilaza, hujui kama hiyo mimba ingetoka kama haikupangwa mtoto kuzaliwa bila kujalisha kama ingetoka akiwa safarini au amekaa?.
   
 13. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  wakati mwingine ukiwafuata sana kina ananilea nkya ndio matatizo kama hayo yanatokea..

  kwani angewaambia nduguze wangemtenga wakati wanafahamu anatatizo. mwambie aache kujistukia itamcost zaidi ya hapo.
   
 14. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #14
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimefiwa na mama, when I was young, na nilifiwa na baba ambaye nilimuuguza mwenyewe na akarudi nyumbani akiwa amepona lakini akazidiwa ghafla na kufariki, but I didin't panic, nilijipanga na kwenda nyumbani kuzika. so what is abig dill kufiwa na kaka! All of us we will die one day, none of us wil live forever!
   
 15. m

  mhondo JF-Expert Member

  #15
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Sasa utajuaje kuwa haikupangwa mtoto asizaliwe. Kusema kuwa ni kilaza siyo sahihi.
   
 16. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #16
  Dec 30, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwani wewe ndo Mungu, hakuna lolote la kumfanya Mungu ndo kajalia mtoto asizaliwe wewe hata ukienda kwa waganga kama mungu hataki upate mtoto hutapata.

  Hata ukiowa wanawake wengine kama mungu hataki wewe kupata mtoto utaishia kwenda kujitubu kwa waganga au madaktari wa kila aina katika hospital za dunia nzima na hupati kitu, tulia kijana na mke wako...Wacha hasira kama mungu kajalia kupata watoto utapata tu siku za mbele.

  FYI mimi najua kuna mwanamke mmoja alikuwa akitaka kutoa mimba-alikunywa madawa ya kila aina na mimba haikutoka....Hapo lazima uweke akili Mungu akisema yes ni Yes tu hakuna No.
   
 17. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #17
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 996
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Mi nadhani ukifika nyumbani wala husimgombeze mkeo,kwanza mpe pole kwa msiba wa kaka yake na yaliyotokea. Ameshajifunza na hakupenda yatokee hayo,pia usifanye mchezo na kufiwa na kaka especially aliyekuleya.....Mungu atawapa mtoto mwingine!!!
   
 18. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #18
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Mbona mimi nilifiwa na aliyenizaa kabisa na wala siku-panic!
   
 19. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #19
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  wanawake hata wao hawajielewi
  tena wakikatazwa ndo hutaka kufanya
  hasa wanapokuwa na uhakika wa Love and protection.

  Wala usimgombeze
  ana machungu ya kufiwa na mimba
  ni fundisho kwa leo na siku zijazo.
   
 20. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #20
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Samehe saba mara sabini.
   
Loading...