Wakuu nina ndoa ya kama Mwaka mmoja hivi!
Wife tulioana kila mtu akiwa na maisha yake, I mean alikuwa anajitegemea na mimi najitegemea!
Tukaamua kuanzisha makazi mapya, tuachane na yale ya zamani, hii sehemu aliunganishiwa na marafiki zake wa karibu kwa sababu na wao wanaishi hapo, ni nyumba nzuri tulivyoamia mambo yalikuwa poa sana, bahati nzuri wote ni watumishi na tunakisehemu cha kufanya ujasiriamali.
Hao marafiki zake wawili ni watumishi pia, na mara nyingi mke wangu ndio huwa wakwanza kuwahi kurudi nyumbani kabla yao!
Ishu inakuja hapa, kwa takribani kama miezi 3 hivi naona wife ndio amegeuka kama mpishi wao! Kila akipika ni lazima wawe na share kwenye msosi wake, kwa wanawake wanaojitegemea kabisa! Na kila mtu ana nyumbani kwake.
Nilijiuliza wife huwa anapata msaada gani kwa hao wadada hadi awapikie kila siku nikakosa jibu.
Wao kupika ni week end tu! Na hawawezi kuleta msosi kwetu kama wife anavyowapelekea, she use her own money to buy all staffs bahati nzuri she never ask any money for food, due to some agreement, pesa yangu ikuze mtaji na kuendeleza ujenzi na yake ishughulike na mambo ya ndani yote ikiwemo mavazi na chakula Ishu inakuja hapo kwenye hizo affairs nyingine, natamani kumpiga stop! binafsi naona kama hili swala halijakaa vyema wakuu, Tushauriane!!