Pole sana kwa kulea mtoto peke yako hasa katika kipindi ambacho ulihitaji ukaribu wa mzazi mwenzio, inauma sana, pole sana.
Kusema ukweli baadhi ya wanaume (na niseme walio wengi) huogopa kitu mimba hasa kinapotokea nje ya ndoa. Sielewi ni kwa nini lakini hupenda sana kuitwa baba wanaume wa namna hii.. Niliwahi kusimuliwa kisa cha namna hii na mdada ninayefahamiana naye kikazi na yeye hili limemtokea mara mbili kutoka kwa mwanaume huyo huyo mmoja. Yaani alimmimba na kusepa, alipojifungua baada ya miezi kadhaa kupita akamtuma rafiki yake akachungulie kama mtoto anafanana naye, akakuta ni hivyo, alikujaje haraka haraka na pickup la mahitaji ya mtoto na samahani zisizo na idadi... Mtoto alipofikisha umri wa miaka miwili na zaidi mdada wa watu mimba nyingine ya huyu huyu bwana... Bwana kujua hilo akakata mguu bibi kahangaika na mimba hadi dakika za mwisho karibia na kujifungua, ikawa bahati mbaya mdada kalazwa Tumbi zaidi ya wiki maana mimba ilikuwa imeharibika kipindi, kujiuguza mwenyewe, kwa miezi kadhaa hadi kutengamaa kurejea kazini na kunihadithia kisa chote bwana hana hata taarifa ya kinachoendelea!!
Ila huyu bwana ni mume wa mtu. Ushauri jifikirie mara kadhaa ukiweza msikilize kwa minaajili ya kupokea msaada wa malezi ya mtoto lakini angali usiingie katika mtego wa kutoa penzi na kubeba ya pili ukatekelezwa tena...., kubali matunzo ya mtoto kwa kuwa kama alivyosema mmojawapo humu kwamba mtoto akikua atamtafuta babaye na hasa kama mtoto ni wa kike ndo kabisa akimjua babaye huna lako wakati ulihangaika peke yako kumlea wakati nafasi ya mzazi mwenzio alijileta kutaka kuchangia malezi... Utaumia zaidi ya unavyohisi...