Nimezaa na mke wa mtu

Wakuu pasipokujua niliazisha uhusiano na mke wa mtu tukiwa chuoni,mpaka kupelekea kumpa mimba ndipo nilijua kuwa ni mke wa mtu kwani aliamua kuniweka wazi, sasa jana nimekutana nae akiwa na mtoto kwa kweli mtoto ni mzuri sana nifanyeje ili nimchukue
huyo si mtoto wako, ni mtoto wa mwenye ndoa. unaweza kuona hata kwenye kadi ya kliniki waliweka jina la huyo mwenye ndoa, na mtu pekee atakayethibitisha kuwa huyo ni mtoto wa nani ni huyo mwanamke kwasababu yeye ndiye anayejua lini alikuwa siku za hatari hata kupata mimba ya nani....au la wewe mwenyewe uanze kwenda kujilisha kwenye mdomo wa simba, uanze kuingilia ndoa ya watu (unafuata kifo?) uwaambie unahisi huyo mtoto ni wako hivyo mkapime dna ndipo pengine itathibitishwa. kitu kigumu sana icho, kwenda kwa mume wa mtu kumwambia mimi nililala na mkeo nikampa mimba nahisi huyo mtoto wako ni wangu...imagine kama pembeni yake kuna upanga utapona kweli...hahaha,

nakushauri achana na ndoa ya watu, usijitafutie matatizo bure, wala usivuruge ndoa ya wenzio. kama uyo ni mtoto wako atakuja kufahamika kwa wakati wake ambao Mungu ataupanga kwasababu naamini hata kama uyo ni mtoto wa kambo tena wa kuingilia ndoa, bado Mungu anampenda huyo mtoto kama anavyowapenda wanadamu wengine wote tu, na atamsaidia hata atakapokuwa mzee.

bofya hapa SHERIA KWA KISWAHILI

View attachment 103708View attachment 103708
 
tafuta mke zaa nae kama shida ni mtoto au mbegu zimeisha? usijitafutie balaa ndugu yangu.we umeona mtoto unakurupuka wako huyo dada alikuambia mtoto wako?au unadhan we ndo unajua kugegeda kuliko mume wake?acha hizo
 
Mlikuwa mnasomea cheti cha nini wote wawili hata msitambue umuhimu wa afya zenu? Hope elimu zingine haziwasaidii kabisa bora mkahudumu usafi maofisini.
 
Wewe una hamu ya kuliwa KABANG!!!!!!!!! WATU WATARARUA MARINDA HAYO, SHAURI YAKO
 
Kuna posts humu ndani zinatisha watu kui.gia kwenye ndoa aiseee.....
 
Wakuu pasipokujua niliazisha uhusiano na mke wa mtu tukiwa chuoni,mpaka kupelekea kumpa mimba ndipo nilijua kuwa ni mke wa mtu kwani aliamua kuniweka wazi, sasa jana nimekutana nae akiwa na mtoto kwa kweli mtoto ni mzuri sana nifanyeje ili nimchukue
Tunaomba mrejesho mtoto umefanikiwa kumchukua.
 
wakati meingine lazima ukubaliane na matokeo ya uzinzi ,sio kuukosa ufalme wa Mbinguni tu,hata hasara nyingine utazipata hapa hapa dunia. tulia hivyo hivyo,hesabu ni matokeo ya dhambi na ndio hasara yake
 
Wakuu pasipokujua niliazisha uhusiano na mke wa mtu tukiwa chuoni,mpaka kupelekea kumpa mimba ndipo nilijua kuwa ni mke wa mtu kwani aliamua kuniweka wazi, sasa jana nimekutana nae akiwa na mtoto kwa kweli mtoto ni mzuri sana nifanyeje ili nimchukue
Muibe
 
Back
Top Bottom