Wewe jamaa kama ni kweli basi una character ya kipekee sana! Namna unavyo jibu watu, bila hasira wala mihemko. Endelea hivi hivi, kila siku ingia JF, Soma, anzisha thread na jibu watu. Tafuta mtu wa karibu yako ambae ataweza kukufundisha jinsi ya kutumia vizuri JF. Pia uwe unasoma magazeti na maandishi yoyote kwa ujumla.
Shehe mbona hii kazi mkuu unataka kutupa,umeshaambiwa bonyeza we kazi yako ni kubonyeza mengine utajuwa ukishapabonyeza,ok angalia hii
kumjibu mtu bonyeza hapo nilipozungushia kijiduara kisha itakuja kama hii picha ya pili utaandika unachotaka kumjibu hapo nilipoandika kawaida then bonyeza juu pale nilipopazungushia kiduara picha ya tatu ili kupost
Note:Hii ni kama unatumia app ya JF japo nina uhakika ndiyo unayotumia kama unatumia browser sema usaidiwe tena.