Nimewaza hivi kuhusu elimu yetu

Nimewaza hivi kuhusu elimu yetu

periodic table

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2019
Posts
208
Reaction score
516
Kutokana na kukua kwa teknolojia na taaluma za ufundi duniani Kuna mabadiliko makubwa Sana yanapaswa yafanyike kwenye mfumo mzima wa elimu yetu ili tupate vijana wenye ubunifu na uwezo wa kupiga hatua na kututoa hapa tulipo,hasa kiuchumu na kitekinolojia..

MIAKA SITA HADI MIAKA KUMI..
Hili liitwe darasa la msingi ambapo mwanafunzi atafundishwa kuhusu uzalendo,maliasili za nchi yake,mipaka ya nchi yake,geographia pamoja na historia ya dunia na nchi yake kwa ujumla..

MIAKA KUMI HADI KUMI NA TANO.
Hii itakua Kama stashahada ambapo mwanafunzi atafundishwa kuhusu stadi za ufundi atakaochagua mwenyewe au fani yoyote atakayopenda mfano atafundishwa moja kwa moja kuhusu udaktar kuanzia hatua za awali,uingineer,uhasibu,ualimu..

Na Kama kuhusu ualimu mwanafunz atachagua anapenda awe mwalimu wa nn na historia yake ya mwanzo itambeba pia..

Kwa mfano atabobeakatika hesabu pekee,kingereza pekee,historia pekee,biologia pekee,chemistry pekee,physiology pekee,anatomy pekee,biochemistry pekeee,..au Kama ni daktar basi atasoma vyote vinavyohusu udaktar,au ufamasia..

Hii itafanya vijana wawe wabobezi Zaid na hata kuthubutu kufanya vumbuzi za Aina mbali mbali Kwan watasoma wakiwa wadogo Sana na hii itachochea ubunifu wa Hali ya juu..

MIAKA KUMI NA TANO HADI ISHIRINI
Hapa vijana watabobea Zaid katika fani walizochagua hapo juu na ili akabidhiwe degree lazima afanye ubunif na uonekane kwa vitendo.

Hapa creativity(ubunifu) ndio utapewa kipaumbele na vijana watakua encouraged kua wabunifu ili tuweze kupata wataalam wabobezi zaidi.

Hapo Sasa vijana watakua wameiva na elimu ya vtendo itapewa kipaumbele zaidi..

Baada ya hzi hatua tatu mtu ataamua aendelee na masters au PhD..hapa tutapata wabobezi wa Aina mbali mbali ambao ni vijana pia na watakua na uthubut mkubwa wa kufanya vtu vikubwa katika nyanja zote za sayansi,Sanaa na uchumi..

Nakaribisha mawazo mbadala haya ni mawazo yangu tu.

Matusi na kejeli si uungwana ..karibuni Sana.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kutokana na kukua kwa teknolojia na taaluma za ufundi duniani Kuna mabadiliko makubwa Sana yanapaswa yafanyike kwenye mfumo mzima wa elimu yetu ili tupate vijana wenye ubunifu na uwezo wa kupiga hatua na kututoa hapa tulipo,hasa kiuchumu na kitekinolojia....
Kiongozi, Kwanza nikupe pongezi kwa kuliona hilo. Pili Sina 7babu ya kupinga wazo la mtu linalo tokana na hii mada (kila mwanadamu Ana haki ya kujieleza na kuwakilisha mawazo yke).

Laiti ninge kuwa mm ndio waziri wa elimu au nahusika na maswala ya elimu serikalini. Ninge Nena machache Kama sio mengi kwa faida yako na wengine wenye mawazo mazur Kama yako.🙏🙏🙏
 
Na wale watakao shindwa soma hayo yt mkuu wapelekwe wapii maan ujawazungumziaaa wao piaa maana c wt watawezana kwenyee hzo sayanc wala tecnolojia au ndio wakacheze cmba na yangaa???
 
Tukumbuke Kuna mambo yao kalenda mpya ya mtaala jamani!!
 
Back
Top Bottom