Nimewapiga wote na kesho shaurini

Nimewapiga wote na kesho shaurini

Trimmer

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2014
Posts
2,800
Reaction score
4,907
Ndio ilibidi niwapige wote ili waache ugomvi uishe..
Ilikuwa hivi...
Mke wangu yuko kwenye bifu kubwa na mwanamke mwingine jirani yetu siku nyingi wamekuwa katika bifu ambalo kiukweli hata sijui kwanini wamefikia hatua hii ya kurushiana makonde....
Yaani nafika tu hivi home mara nakuta hao mkono unatembea kisa...
Eti wanagombea maji ya mvua kwamba wife kakinga maji then jirani kayachukua... Khaa..! Ivyo tu na mvua bado inanyesha why..? Nikaachanisha ugomvi...
Wakaachiana lkn kumbe bado wanataka waoneshane nani mbabe..
Ujinga nilichoamua ni kuwatandika makofi wote si mke wangu si jirani wote na baada ya hapo ugomvi ukaisha..
Kumbe jirani kachukia sana hivi ninavyoandika nimepokea barua ya kuitwa shaurini kesho ofisi ya Kata sasa wadau hata sielewi nitajitetea vipi maana ni kweli nahisi ni makosa kuwapiga hawa wanawake...
 
Kama una nguvu sana uwe unapigana na wanaume wenzio, au hata piga ngumi ukutani hasira ziishe, mwanamke hapigwi
 
Machale yanani-play kuwa kuna kinachogombewa zaidi ya maji.

Chunguza utajua.

I can't conclude that kuna serengeti boy wanamgombea au ni sugar daddy ila chunguza utajua tu.
 
Kama una nguvu sana uwe unapigana na wanaume wenzio, au hata piga ngumi ukutani hasira ziishe, mwanamke hapigwi
Kama umesoma vizuri andiko langu ni kwamba nilitumia nguvu sana kuwaachanisha lkn hawakunielewa solution niliona ni hiyo tu ya kuwa refresh maana niliona akili zao zimefreez kwa hasira
 
Usijali, sema ulikwazika na ugomvi Wa kitoto na usijali polisi hutafikishwa na hata ukifikishwa hutaenda jela, we sema ulishikwa hasira, wazee wakikuambia uombe radhi omba yaishe. Ila waambie ulikuwa ( provoked) ni kinga kisheria endapo utapelekwa mahakamani (ground ya defence)
 
Yaani unaitwa Ofisi ya kata?
Jirani yako sio mzima....ulitakiwa uwe unanyea debe saa hizi

Hiyo miguvu ingeitumia kwenye kulima na hizo mvua ungekuwa umefanya la maana
 
Jirani ni mkee wa mtu ? Kama mkee wa mtu muuombe samahani mumewe kwanza then.....

Simple eleza bifu lao toka nyumaaa na sababu kuu ya bifu wewe huijui na leo unapendaa uijui tokaa kwa hao

Swala la kumpigaa omba samahanii akiikubali tu kukusamehee kaziaa kujuaa bifu nini utagunduaa mengine

Mwisho usipuuzie kwenda hio kesjo
 
Kama umesoma vizuri andiko langu ni kwamba nilitumia nguvu sana kuwaachanisha lkn hawakunielewa solution niliona ni hiyo tu ya kuwa refresh maana niliona akili zao zimefreez kwa hasira

Kama kupiga ni solution basi kesho uwapige waliokuita pia
 
Wee nenda ila eleza ukweli tu na ni katika hali ya kuamulia ugomvi ikanibidi niwachape kidogo waachane LA sivyo wamgeuana. Kwa sababu namtoa A, B analetavurugu, unamtoa B, A anaendeleza vagi, kwa hiyo nikatumia nguvu kidogo kuamua. Wataadhibiwa wao
 
...uliwapapasa tu wewe!...huyo jirani angekuwa hospitali sahizi!
...afu kumbe kuonaona ikulu,central,mahakama kunasaidia!...kuitwa ofisi ya kata ndo unajinyea??
...aaaarrrrggh!
 
Wee nenda ila eleza ukweli tu na ni katika hali ya kuamulia ugomvi ikanibidi niwachape kidogo waachane LA sivyo wamgeuana. Kwa sababu namtoa A, B analetavurugu, unamtoa B, A anaendeleza vagi, kwa hiyo nikatumia nguvu kidogo kuamua. Wataadhibiwa wao

Asante mkuu nitaanzia hapa
 
Umetumia busara sana! Tena ukifika huko komaa ujue chanzo cha ugomvi, otherwise wataendelea kukuchezea
 
Back
Top Bottom