Leo majira ya saa 5 asubuhi nimeenda kupiga kura (uchaguzi wa wenyekiti) Mimi sio mwanasiasa na sijui hata majina ya wanao gombea, lakini nilijipanga kuenda kuwachagua wagombea wa upinzani pekee.
Nilipofika nimekutana na mambo haya.
Nilianza kwa kutafuta jina langu kwenye makaratasi yaliyo bandikwa ukutani, lakini askari polisi akaniambia usijali nenda kule jina watakutafutia wenyewe (yaani jina watalifauta wanao simamia uchaguzi)
Baada ya kuiingia kwenye chumba Cha uchaguzi, yule wakala akaniuliza jina langu then nikamtajia, akajifanya analitafuta then ndani ya dk Moja tuu akalipata. (HUU NI UDHAIFU MKUBWA, inamaanisha hata Mtu ambae hajajiandikisha basi anaweza kupiga kura )
Baada ya hapo nikapewa karatasi tatu za kuwapigia kura wagombea, ndani ya hizo karatasi nimeona Maajabu, yaani wagombea ni watatu lakini wote ni wagombea wa CCM, kwaiyo natakiwa nimchague mmoja katika hao wagombea watatu wa CCM (hili limeniuma sana ) sijaona mgombea wa upinzani
Nimeamua kutumbukiza karatasi ambazo sijamchagua mgombea yoyote.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.