Nimetoka kifungoni, nisamehewe na Vijana tuijenge Nchi yetu

Sumti

JF-Expert Member
Jan 30, 2016
2,311
2,157
Ni takriban wiki nimekula BAN la nguvu kwa mjadala uliokuwa unamhusu Mh. Tundu Lissu. Mimi kama kijana mwenzenu, nashukuru kwa kurudishwa tena jukwaani na kuomba msamaha kwa lile lililotokea.

Rai yangu kwa wanajukwaa wote ambao tunajipambanua kama the great thinkers ni tujeni Uzalendo kwa Nchi yetu. Adabu na utii kwa viongozi wetu ni jambo la msingi sana. Kijana mwenye uchungu na Nchi yako ukionekana kushabikia matusi b kejeli kwa viongozi wako basi hapo kuna walakini na sidhani kama kuna mwelekeo chanya wa kuitakia mema Nchi Yetu.

Nchi itajengwa na sisi vijana na pia itaharibiwa na sisi vijana. Lakini pia ni lazima tujifunze kukubaliana kutokukubaliana. Mbarikiwe nyote.
 
Ulishindwa kufungua I'D nyingine???Hata ukitukana kwa kifupi ujumbe unakuwa umefika ila pole kwa BAN
 
ukila BAN nenda kwenye browser yako clear cache, cookies na password history zote, fungua ID nyingine maisha yanaendelea
 
Aisee hakuna kitu nakichukia jf kama Ban aisee niliipata mara moja na sijatokea kuitamani tena.

Ila nina swahiba wangu huyo kwake ni kama dozi haimkalii mbali kule siasani.
 
Hahahahha uliponda chadema eee?shauri yako tutakuremove huku kbs...
Mkuu nilikuwa sijui kuwa humu ukiitukana CCM unashangiliwa kama shujaa ila ukiwa mtetezi wa hoja za Serikali unaonekana wewe ni adui.
 
Back
Top Bottom