nimetoa cheka na kitime?

nimetoa cheka na kitime?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,650
Reaction score
20,993
MWANAKIJIJI 1: Aise nataka kwenda Dar
MWANAKIJIJI 2: Lazima ufike Sinza kuna baa inaitwa SHKAMOO
MWANAKIJIJI 1: Kwanini?
MWANAKIJIJI 2: Hapo ukiingia wanakupa kinywaji bure, halafu unapotoka unapewa mpenzi bure
MWANAKIJIJI 1: Dah huko lazima niende, we uliwahi kufika huko?
MWANAKIJIJI 2: Hapana lakini mke wangu kila akienda Dar lazima afike hapo
 
Ilikuwa Jumamosi asubuhi, kazee kamjini kakaingia na kabinti kazuuri kwenye yard ya magari mapya.
KAZEE: Chagua gari unalotaka mpenzi....kabinti kakazunguka na kwa msaada wa mwenye wa mwenye yard kakapata Verrosa nyeupe nzuri sana.
MDADA: Mi naitaka hii
KAZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima uwe una draiv mwenyewe. Kakatoa kitabu cha cheki na kuandika cheki palepale na kumpa mwenye yard
MUUZAJI: Sasa mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa una pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee
KAZEE: Hilo nilijua. Haya twende zetu sweety Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lako..................Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.
MUUZAJI: We mzee kavu sana, akaunti yako ilikuwa haina hata senti tano.
KAZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.

KITIME: Nataka nimfanyie mke wangu bonge ya suprise Valentine ya mwaka huu, sijui nimfanyie nini?
ABOUDONA: Mkutanishe na nyumba ndogo yako
 
Kwa kweli nilikutana na binti mmoja juzijuzi Njenje, roho ikanitoka. Kila nikitry kumkonyeza wala haniangalii. Nikamtuma weita amuulize anataka drink gani, kagoma kunywa chochote, nikaona problem yake ndogo, mji mzima umejaa matangazo ya waganga wanaoweza kukufanya upendwe. Nikamuendea mganga mmoja aliyedai anaweza kukufanya umpate mpenzi bila jasho, nikampa the whole ishu, witchdoctor akanambia dawa rahisi sana atanipa pete inaitwa Touch and follow. Ila nimtumie airtime ya shilingi alfu thelathini kwenye hendset yake. Haraka sana nikafanya hivyo nikakabidhiwa pete. Masharti rahisi sana kazi yangu ni kutafuta yule demu nihakikishe pete inamgusa tu atanifollow kila mahala. Basi nikamsaka demu nikamkuta Lango la Jiji anasikiliza Taarab, nikamgusa na pete kisha nikatoka ukumbini kumsubiri, ngojaaa ngoja na wewe, dah hakuna cha kunifwata wala kunifollow. Nikasepa home nimenuna kishenzi. Kufika home nafungua Whatsapp nicheki washkaji nikakuta demu kanifollow, kucheki Twitter kanifollow, Instagram, Tango, Badoo, Facebook kila mahala kanifollow duh. Kesho yake mapema nikaenda kwa mganga na kumpandishia, nikamuuliza mbona yule binti nimemgusa hakunifuata?. Nae kaja juu, 'We ---- nini siku hizi mambo kidijitali. Huoni sikukuomba kuku wala mbuzi nimeomba unilipe airtime, na kwa hiyo huoni binti anakufwata kila mahala kidijitali? Hebu sepa" Nikawa mpole mwenyewe
 
Mjamaa alikwenda mji mmoja jina kapuni kumtembelea rafiki yake, chakula kikaja, akajikuta kapewa ugali na nyama nyingi na mwenyeji wake pia akapewa ugali na nyama nyingi, watoto na mke wakawa pembeni wanakula ugali na mboga za majani. Jamaa lika mtach lakini akanyamaza akapanga wakimaliza kula amuulize rafiki yake kwa nini anafanya uchoyo huu. Walipomaliza sahani zimekwisha tolewa na baada ya kunywa maji baridiiiiiii;
JAMAA: Aise sijapenda hii tabia, sisi tumekula ugali na nyama kibao mkeo na watoto wamekula mboga za majani bila hata kipande cha nyama
MWENYEJI:Mi sio kosa langu, wao wenyewe hawataki kabisa kula nyama ya mbwa, sasa mi nifanyeje?
 
BINTI: Baba mi nina mimba
BABA: Loh mwanangu loh
BINTI: Baba najua umefadhaika sana nami nasikitika kukupa uchungu namna hiyo, naona bora nijiuwe nisiishi kabisaa hapa duniani
BABA: Tulia kwanza mwanangu, zaa kisha tufanye vipimo vya DNA pengine huo mtoto sio wako
 
Jamaa kasimamishwa na trafiki kwa kosa la mwendo mkali;
TRAFIKI: Mheshimiwa unajua ulikuwa unakimbia spidi kali sana?
DREVA: Sasa leseni sina, gari niliiba, halafu chini ya kiti nina pisto ya wizi unadhani ntaendesha polepole
TRAFIKI: Mungu wangu kumbe we jambazi?
DREVA: Si jambazi tu, pia huwa nauza viungo vya binadamu, kwenye buti kuna vipande vya miili vya watu....trafiki haraka akaita msaada wa polisi wenzie waliofika baada ya muda mchache wakiogozwa na afande mkubwa
AFANDE: Askari vipi tena hapa?
TRAFIKI: Afande nimelikamata jambazi sugu. Halina leseni, gari ni la wizi, limeficha pisto chini ya kiti na kwenye buti kuna vipande vya miili ya binadamu.
AFANDE: Leseni yako iwapi?
DREVA : Hii hapa afande na kadi ya gari hii hapa
AFANDE: Askari mbona leseni iko safi, na gari ni lake sio la wizi? Hebu sachini gari kama kuna hivyo vitu alivyoviona askari....gari likasachiwa lilikuwa safi
DEREVA: Afande askari kaninyanyasa sana huyu kasema yote hayo asiponibambika atasema nilikuwa naenda mwendo kasi
AFANDE: Mheshimiwa wewe nenda, jeshi litajua namna ya kushughulika na huyu askari aliyekusumbua

mtu kama john kitime angekuwa directa wa vichekesho ingekuwa poa sana.
 
Ilikuwa Jumamosi asubuhi, kazee kamjini kakaingia na kabinti kazuuri kwenye yard ya magari mapya.
KAZEE: Chagua gari unalotaka mpenzi....kabinti kakazunguka na kwa msaada wa mwenye wa mwenye yard kakapata Verrosa nyeupe nzuri sana.
MDADA: Mi naitaka hii
KAZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima uwe una draiv mwenyewe. Kakatoa kitabu cha cheki na kuandika cheki palepale na kumpa mwenye yard
MUUZAJI: Sasa mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa una pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee
KAZEE: Hilo nilijua. Haya twende zetu sweety Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lako..................Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.
MUUZAJI: We mzee kavu sana, akaunti yako ilikuwa haina hata senti tano.
KAZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.

hii mbinu ntaitumia siku moja!!

ngoja nijiandae....
 
John kitime ambaye ni mwanamuziki namkubali sana kwa kutoa vichekesho.
 
Ilikuwa Jumamosi asubuhi, kazee kamjini kakaingia na kabinti kazuuri kwenye yard ya magari mapya.
KAZEE: Chagua gari unalotaka mpenzi....kabinti kakazunguka na kwa msaada wa mwenye wa mwenye yard kakapata Verrosa nyeupe nzuri sana.
MDADA: Mi naitaka hii
KAZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima uwe una draiv mwenyewe. Kakatoa kitabu cha cheki na kuandika cheki palepale na kumpa mwenye yard
MUUZAJI: Sasa mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa una pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee
KAZEE: Hilo nilijua. Haya twende zetu sweety Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lako..................Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.
MUUZAJI: We mzee kavu sana, akaunti yako ilikuwa haina hata senti tano.
KAZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.

yalishanikuta
 
Hiyo inaitwa Kata Funua.
 
Mjamaa alikwenda mji mmoja jina kapuni kumtembelea rafiki yake, chakula kikaja, akajikuta kapewa ugali na nyama nyingi na mwenyeji wake pia akapewa ugali na nyama nyingi, watoto na mke wakawa pembeni wanakula ugali na mboga za majani. Jamaa lika mtach lakini akanyamaza akapanga wakimaliza kula amuulize rafiki yake kwa nini anafanya uchoyo huu. Walipomaliza sahani zimekwisha tolewa na baada ya kunywa maji baridiiiiiii;
JAMAA: Aise sijapenda hii tabia, sisi tumekula ugali na nyama kibao mkeo na watoto wamekula mboga za majani bila hata kipande cha nyama
MWENYEJI:Mi sio kosa langu, wao wenyewe hawataki kabisa kula nyama ya mbwa, sasa mi nifanyeje?
[/QUOTE
Aaaarrghh...!!
 
Ngumi mfululizo zinafataaaaaaa
 
Back
Top Bottom