Nimetapeliwa na aliyekuwa mpenzi wangu

Habari ya saizi waungwana?? Naamini mu wazima wa afya kabisa. Bila kupoteza muda niingie kwenye maada.

Kwanza kabisa. Mimi ni binti wa miaka 28, sijaolewa bado na mahusiano yangu yamevunjika wiki tatu zimepita na ndicho chanzo cha mkasa wangu.

Hapo nyuma wakati nipo home mama alinipa sh lak tatu nifanye biashara maana aliamini nina mkono wa biashara na kiukweli nilipoaanza kuuza sendo za kimasai zile niliuza kwa mafanikio makubwa. Tuachane na hilo.

Wakati nafanya biashara nilikutana na boyfriend ambaye tulijikuta tunapendana kweli kweli. Huyu bwana alikuwa muuza urembo. Tumedumu nae kwa muda wa miaka mitatu. Alikuwa na wivu mno hadi alivunja laini zangu na kunisajilia mbili kwa majina yake yeye.

Mwaka jana aliniambia tununue uwanja tujenge nikaona wazo zuri, akaniambia bei ya uwanja akapendekeza tuchangiane, kweli nilichangia kiasi fulani hivi tukapata uwanja. Mwaka huo huo akasema tujenge msingi, tukajenga. Na mwaka huu tulikuwa tunamalizia kuijenga.

Mimi kulingana na mtaji wangu na hela niliyotumia kujengea nyumba nikaishiwa kabisa na yeye akaniahidi kunipa mtaji mwingine tena maana alitaka tuchukue mkopo benki kwa dhamana ya nyumba mimi nikagoma kabisa.

Basi majukumu yangu yote akayavaa yeye kuanza kunilisha, kodi ya nyumba na vingine vingi maana mimi niliishiwa hela. Shida imekuja baada ya kodi kuniishia mimi nikamwomba awekee milango nyumba yetu ili mimi nihamie akasema kwa sasa hana hela, nikamwomba basi anilipie kodi sh elfu 75 tena akaanza kalenda.

Nilivyombana sanaa akawa mkali ndipo akafunguka sasa. Kumbe ile nyumba na uwanja si vyetu tena, alikuwa anamsaidia rafiki yake mwanajeshi, kwa hiyo yeye alikuwa msimamizi tu. Hela nilizokuwa natoa mimi sijui alichozifanyia na alivyoona nimekuwa mkali akakimbia na kwenda huko kusikojulikana.

Kwa hiyo nimetapeliwa na huyu bwana kwa namna hiyo. Sasa saizi mwenye nyumba kanibana ananipa vitisho vya kunitimua nami hapa sijabaki na hela. Nimesharipoti polisi kuhusu kutapeliwa na bado anatafutwa kubaini aliko.

Mwisho, naombeni msaada wa hali na mali jamani niweze kulipa kodi ya chumba sh 75,000. Na pili naomba ushauri wenu nifanyaje zaidi ili niweze kurudishiwa hela nilizotaperiwa na je siwezi kusimamisha ile nyumba kuguswa na mtu hadi kibari cha mahakama kitoke kwa maridhiano?

Naomba kuwasilisha.
Wewe ni muongo na unataka kutapeli watu hapa kwa sababu zifuatazo:
1. Kwa kuwa, mlichanga mkanunua kiwanja ina maana ulishiriki kwenye manunuzi hayo kwa kusaini mkataba kama shahidi au mnunuzi wa eneo hilo.
2. Na kwa kuwa, ulishiriki moja kwa moja kwenye manunuzi ya eneo hilo, unataarifa zisizotia shaka kwamba ilipojengwa nyumba unayosema kwenye andiko lako imejengwa kwenye eneo lenu au laa
3. Kwa kuwa, ulichangia kununua materials ya kujengea sidhani kama ulikuwa unatuma kwa njia ya mtandao au kumkabidhi jamaa yako bila kufika site hata siku moja japo kuona maendeleo ya ujenzi tu.
4. Hivyobasi, kwa kuwa andiko halina ushahidi wowote na limejaa maneno dhaifu sana yenye kila viashiria vya kiutapeli, nashauri usisaidiwe mpaka hapo utakavyoweza kutushawishi kwa ushahidi kamili.

Naomba kuwasilisha.
 
He3 mambo ya girlfriend na boyfriend halafu mlipendana sana na kutapeliana? Hayo mambo ni ya facebook huku tunajadili hoja nzito za kuipeleka nchi kwenye maziwa na asari.
 
Back
Top Bottom