Nimetapeliwa na aliyekuwa mpenzi wangu

judy0

Member
Mar 28, 2021
92
140
Habari ya saizi waungwana?? Naamini mu wazima wa afya kabisa. Bila kupoteza muda niingie kwenye maada.

Kwanza kabisa. Mimi ni binti wa miaka 28, sijaolewa bado na mahusiano yangu yamevunjika wiki tatu zimepita na ndicho chanzo cha mkasa wangu.

Hapo nyuma wakati nipo home mama alinipa sh lak tatu nifanye biashara maana aliamini nina mkono wa biashara na kiukweli nilipoaanza kuuza sendo za kimasai zile niliuza kwa mafanikio makubwa. Tuachane na hilo.

Wakati nafanya biashara nilikutana na boyfriend ambaye tulijikuta tunapendana kweli kweli. Huyu bwana alikuwa muuza urembo. Tumedumu nae kwa muda wa miaka mitatu. Alikuwa na wivu mno hadi alivunja laini zangu na kunisajilia mbili kwa majina yake yeye.

Mwaka jana aliniambia tununue uwanja tujenge nikaona wazo zuri, akaniambia bei ya uwanja akapendekeza tuchangiane, kweli nilichangia kiasi fulani hivi tukapata uwanja. Mwaka huo huo akasema tujenge msingi, tukajenga. Na mwaka huu tulikuwa tunamalizia kuijenga.

Mimi kulingana na mtaji wangu na hela niliyotumia kujengea nyumba nikaishiwa kabisa na yeye akaniahidi kunipa mtaji mwingine tena maana alitaka tuchukue mkopo benki kwa dhamana ya nyumba mimi nikagoma kabisa.

Basi majukumu yangu yote akayavaa yeye kuanza kunilisha, kodi ya nyumba na vingine vingi maana mimi niliishiwa hela. Shida imekuja baada ya kodi kuniishia mimi nikamwomba awekee milango nyumba yetu ili mimi nihamie akasema kwa sasa hana hela, nikamwomba basi anilipie kodi sh elfu 75 tena akaanza kalenda.

Nilivyombana sanaa akawa mkali ndipo akafunguka sasa. Kumbe ile nyumba na uwanja si vyetu tena, alikuwa anamsaidia rafiki yake mwanajeshi, kwa hiyo yeye alikuwa msimamizi tu. Hela nilizokuwa natoa mimi sijui alichozifanyia na alivyoona nimekuwa mkali akakimbia na kwenda huko kusikojulikana.

Kwa hiyo nimetapeliwa na huyu bwana kwa namna hiyo. Sasa saizi mwenye nyumba kanibana ananipa vitisho vya kunitimua nami hapa sijabaki na hela. Nimesharipoti polisi kuhusu kutapeliwa na bado anatafutwa kubaini aliko.

Mwisho, naombeni msaada wa hali na mali jamani niweze kulipa kodi ya chumba sh 75,000. Na pili naomba ushauri wenu nifanyaje zaidi ili niweze kurudishiwa hela nilizotaperiwa na je siwezi kusimamisha ile nyumba kuguswa na mtu hadi kibari cha mahakama kitoke kwa maridhiano?

Naomba kuwasilisha.
 
pole, muda wote unayajenga na mwenzio sirini, ulitakiwa ufunguke kwa ndugu/rafiki zake na zako ili wajue mnajenga pamoja, ili haya yote yanapotokea upate pa kuanzia.

Tembelea dawati la jinsia utapata mwongozo mzuri ...mahakamani ni ngumu endapo huna wadhamini na vithibitisho
 
Habari ya saizi waungwana?? Naamini mu wazima wa afya kabisa. Bila kupoteza muda niingie kwenye maada.

Kwanza kabisa. Mimi ni binti wa miaka 28, sijaolewa bado na mahusiano yangu yamevunjika wiki tatu zimepita na ndicho chanzo cha mkasa wangu.

Hapo nyuma wakati nipo home mama alinipa sh lak tatu nifanye biashara maana aliamini nina mkono wa biashara na kiukweli nilipoaanza kuuza sendo za kimasai zile niliuza kwa mafanikio makubwa. Tuachane na hilo.

Wakati nafanya biashara nilikutana na boyfriend ambaye tulijikuta tunapendana kweli kweli. Huyu bwana alikuwa muuza urembo. Tumedumu nae kwa muda wa miaka mitatu. Alikuwa na wivu mno hadi alivunja laini zangu na kunisajiria mbili kwa majina yake yeye.
Mwaka jana aliniambia tununue uwanja tujenge nikaona wazo zuri, akaniambia bei ya uwanja akapendekeza tuchangiane, kweli nilichangia kiasi fulani hivi tukapata uwanja. Mwaka huo huo akasema tujenge msingi, tukajenga. Na mwaka huu tulikuwa tunamalizia kuijenga. Mimi kulingana na mtaji wangu na hela niliyotumia kujengea nyumba nikaishiwa kabisa na yeye akaniahidi kunipa mtaji mwingine tena maana alitaka tuchukue mkopo benki kwa dhamana ya nyumba mimi nikagoma kabisa.

Basi majukumu yangu yote akayavaa yeye kuanza kunilisha, kodi ya nyumba na vingine vingi maana mimi niliishiwa hela. Shida imekuja baada ya kodi kuniishia mimi nikamwomba awekee milango nyumba yetu ili mimi nihamie akasema kwa sasa hana hela, nikamwomba basi anilipie kodi sh elfu 75 tena akaanza kalenda. Nilivyombana sanaa akawa mkali ndipo akafunguka sasa. Kumbe ile nyumba na uwanja si vyetu tena, alikuwa anamsaidia rafiki yake mwanajeshi, kwa hiyo yeye alikuwa msimamizi tu. Hela nilizokuwa natoa mimi sijui alichozifanyia na alivyoona nimekuwa mkali akakimbia na kwenda huko kusikojulikana.

Kwa hiyo nimetaperiwa na huyu bwana kwa namna hiyo. Sasa saizi mwenye nyumba kanibana ananipa vitisho vya kunitimua nami hapa sijabaki na hela. Nimesharipoti polisi kuhusu kutapariwa na bado anatafutwa kubaini aliko.

Mwisho, naombeni msaada wa hali na mali jamani niweze kulipa kodi ya chumba sh 75,000. Na pili naomba ushauri wenu nifanyaje zaidi ili niweze kurudishiwa hela nilizotaperiwa na je siwezi kusimamisha ile nyumba kuguswa na mtu hadi kibari cha mahakama kitoke kwa maridhiano?

Naomba kuwasilisha.
Uko mkoa gan weka namba hapa nikuchangie
 
Dawati la jinsia nadhani lina dili na wana ndoa sio wapenzi
hata wasio wanandoaaa (hata wenye watoto pamoja na hawajafunga ndoa) - hapa mleta mada kwa miaka mitatu walikuwa hawajapata mtoto/watoto (Duh - utamu wa asali jamaa kagoma chonga mzinga)

Dawati la jinsia - wanaweza kuwa na ushauri wa kumsaidia, kutokana na huduma watoazo

vinginevyoo amsameheee huyo ex-boy wake, aanze upya kuyajenga maisha yake.
 
Back
Top Bottom