ngungwangungwa
JF-Expert Member
- Jul 23, 2013
- 644
- 569
Wana MMU
Salaamu,
Me nimeoa miaka 18 iliyopita, kwenye hii mitandao ya kijamii nilibahatika kukutana na binti mmoja mwaka 2008. Wakati huo alikuwa kidato cha 6. Hapahapa Dar.
Kama ilivyo kawaida, tulianza kwa ku-chat kisha tukaonana na baadae nikaomba mzigo, haikuchukua muda sana nikapewa penzi. Tukaingia rasmi kwenye uhusiano tangu wakati.
Baada ya kumaliza masomo yake ya A-level, aliendelea na elimu ya juu katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Kwa sasa amehitimu na anafanyakazi kwenye taasisi moja kubwa tu ya Serikali.
Wakati anasoma, nimemsaidia sana kwa kweli, sikuwa na namna ya kutomsaidia kwa jinsi nilivyokuwa namuona kama mtu mwenye maono na malengo. Kulikuwa na tatizo moja lililokuwa linanisumbua kipindi chote, hakujua kama NIMEOA!
Na kwa kweli aliamini nitakuja kuwa mumewe. Mwaka juzi 2014 aligundua kama mimi nina mke. Aliumia sana kwa kweli, lakini tuliongea nikaomba radhi na akanisamehe kwa sharti la kuwa ndugu tu, mapenzi tena hapana!
Nilikubaliana nae na akaomba nimruhusu akipata mtu aolewe..! Sikuwa na kinyongo nilimruhusu kwa moyo mweupe. Hatukuonana tena tangu siku hiyo, na mawasiliano yetu yalipungua sana! Mwaka jana mwezi wa 7 akanitumia picha za kitchen party, send-off na za harusi.
Nikampongeza kwa kuolewa. Yeye anafanyakazi mkoani lakini kaolewa na mume anayeishi Dar.
Mwezi wa 12 alikuja likizo, akaja hadi kwenye biashara yangu bila hata kunijulisha. Alikuwa amependeza sana, tuliongea mengi sana. Kuna sehemu najenga na alikuwa anaijua. Akaniuliza nimefikia wapi, nikamueleza, baadae tukaenda hadi kwenye jengo lenyewe. Nilikuwa nimemaliza kujenga lakini sikuwa tena na hela za bati.
Kwa vile ni nyumba ya kuishi, sikuwa na haraka nayo. Lakini alipoiona na nikamueleza jinsi nilivyo na hali mbaya, kuimaliza itachukua si chini ya miaka 3. Akaniahidi akirudi atanitumia hela kidogo niezeke. Baadae tukatoka si unajua tena hatukugombana ki-vileee! Haikuwa rahisi kuachana hivihivi. Tukaenda kukumbushia.
Jana alinipigia simu akaniambia leo atanitumia hizo hela. Kweli nimepokea leo milioni 3. Kwa kweli nimekosa hata maneno mazuri ya kumuelezea shukrani zake kwangu. Kesho pia ataingiza kama hizo. Nipo na fundi hapa hivi sasa ananipigia hesabu ya mbao na bati.
Kumbe yale maneno ya mapenzi au mchumba hasomeshwi, hayana ukweli. Wale mnaosomesha fungeni mkanda tu inalipa...!
Nawasilisha.