Nimesitisha uhusiano na rafiki wa mume wangu, hataki kukubali

pendo shununu

Member
Apr 23, 2016
32
28
Mm ni mama wa watoto wawili, nafanya kazi na nimeolewa.

Nikiri tu kwamba nimekua na uhusiano usiofaa na rafiki wa Mr wangu kwa karibu miaka miwili, kituo cha kazi cha Mr ni nje ya dar, kazi zetu ni too demanding kiasi kwamba nafasi ya kutembeleana imekua ni Shida sana, mfano mm nafanya kazi hadi Saturday saa kumi jioni, mara nyingi hata jumapili naitwa kwenda jambo ambalo ni kawaida sana, hivyo naogopa kutoka nje ya dar katika weekend maana naweza kuitwa any time, kwa upande wa Mr nae ni hivyo.

Kwa Hali hii tunaweza maliza miezi mitatu na zaidi Bila kutembeleana, hadi mtu uombe ruhusa rasmi kazini.

Ni katika hali hii nikajikuta naanzisha urafiki usiofaa na best friend wa mume wangu, tumedumu kwa miaka miwili, yeye anaishi na familia yake hapa hapa dar Ingawa yy na mkewe wanapitia kipindi kigumu sana kwa sasa ni kama wanalea watoto tu,

Hivi karibuni katika hali isiyotarajiwa Mr akapata uhamisho kurudi dar, kwa kweli wote tulifurahi sana, ni hapo sasa ndipo niliamka usiku mmoja na kuanza kutafakari kuhusu uhusiano wangu na rafiki wa Mr, kwamba itakuaje sasa, ni rahisi kushikwa, tutauendeshaje huu uhusiano na Mr akiwepo? Je naweza kumudu kuwa na wanaume wawili, katika maswali yote niliyojiuliza majibu yakawa ni NO haiwezekani, hivyo nikanuia kuuvunja uhusiano huo haramu.

Nikatafuta nafasi nikakaa nae yule mpenzi wangu nikamwambia kwa manufaa ya pande zote mm na wewe basi kila mtu aendelee na familia yake, kwa kweli alilia kama mtoto mdogo, akinikumbatia miguuni, nikasisitiza msimamo wangu na nikaondoka maana watu walianza kutushangaa.

Nifupishe tu kwa kusema kwamba, Huyu bwana amegoma kukubali matokeo na kuanza ku behave kama mtoto mdogo hivyo kuhatarisha ndoa yangu, amemchukia mume wangu ghafla na ni kama amegeuka adui, kiasi kuwa juzi Mr ameshangaa sana na kuniuliza kuwa mshikaji tumemkosea nini mbona juzi nimeenda kwake kanichunia, akaondoka na kuniacha sebuleni kwake?
Mr akaniuliza wewe unajua chochote juu ya mabadiliko haya, maana hata simu hapokei, mm nikamjibu sijui chochote.

Sasa hivi ameanza kunipigia simu na kunitishia maisha na mambo mengine, nafikiria kumripoti polisi lakini naogopa mambo yakishafika hatua hiyo kila kitu kinaweza kuwa wazi, halaf ndoa yangu ikavurugika. Au niendelee nae hivyo hivyo kwa kificho na umakini?

Naombeni ushauri wenu, maana mm nilitaka kuachana na hili jambo moja kwa moja lakini situation imekua very tense.

Kiukweli nilikua na mshikaji kwa kampani tu ila nampenda Mr wangu, hivyo naomba isieleweke kuwa mm ni mhuni, na ni shetani tu ndio alinidanganya nikajikuta nimeanzisha uhusiano huo

Help please.
 
Pole sana. Ila siku zote ukimwabudu shetani lazm akuabishe tu kwa namna moja au nyingine. Hapo inabid usisitize kile unachomaanisha, usiendelee na huo uhusiano kbsa. Najua hata mr wako anahic kitu ila hana uhakika. Ukiendelea naye halaf mr akajua hapo huenda ndoa ikavunjika.

Cha msingi block kbsa, acha kuwasiliana naye, hata akipiga usipokee wala kumjibu sms.Ila kumbuka shetan hana urafiki na mtu mwisho wa kaz yake ni aibu na fedheha.

Mlioko kwenye ndoa tulieni, sio km unamkomoa mumeo au mkeo bali ni watoto. Mtakapo tengana watoto huathirika sana. Miaka 2 unacheat, kwa mfano mumeo akiwakataa hao watoto utamlaumu??!! Inawezekana hata watoto 2 sio watoto wake. Tulieni kwenye ndoa mtatesa watoto.
 
Kutembea nje ya ndoa hata kama ni mara yako ya kwanza wewe ni muhuni tu na kama sio muhuni kwanini usingempa mara moja tu na ukaachana naye,iweje utembee naye kwa miaka miwili halafu usiwe muhuni,hii ndio sababu kubwa huwa siamini mapenzi hata siku moja.Hakuna ukweli kwenye mapenzi kabisa.Hebu angalia jamaa yake alivyokuwa blind na cha ajabu anaweza asijuwe mpaka wanaingia kaburini na kwa maisha hayo utaacha kulea watoto wasio wa kwako kweli?
 
Kwa taarifa ulizoweka hapa,kama mumeo yuko humu na ni mtu makini,utakua umejijengea mazingira magumu zaidi,maana akikumbuka kwamba yeye kahamishiwa dar na rafiki yake kamchunia,hatohitaji tena ushahidi.
Baadhi ya wanawake cjui kwanini mliingia kwenye ndoa,kutembea na rafiki wa mumeo ni tusi kubwa sana,hata shetani unaemsingizia hana ujasiri huo
 
Mm ni mama wa watoto wawili, nafanya kazi na nimeolewa

Nikiri tu kwamba nimekua na uhusiano usiofaa na rafiki wa Mr wangu kwa karibu miaka miwili, kituo cha kazi cha Mr ni nje ya dar, kazi zetu ni too demanding kiasi kwamba nafasi ya kutembeleana imekua ni Shida sana, mfano mm nafanya kazi hadi Saturday saa kumi jioni, mara nyingi hata jumapili naitwa kwenda jambo ambalo ni kawaida sana, hivyo naogopa kutoka nje ya dar katika weekend maana naweza kuitwa any time, kwa upande wa Mr nae ni hivyo
Kwa Hali hii tunaweza maliza miezi mitatu na zaidi Bila kutembeleana, hadi mtu uombe ruhusa rasmi kazini

Ni katika Hali hii nikajikuta naanzisha urafiki usiofaa na best friend wa mume wangu, tumedumu kwa miaka miwili, yeye anaishi na familia yake hapa hapa dar Ingawa yy na mkewe wanapitia kipindi kigumu sana kwa sasa ni kama wanalea watoto tu,

Hivi karibuni katika hali isiyotarajiwa Mr akapata uhamisho kurudi dar, kwa kweli wote tulifurahi sana, ni hapo sasa ndipo niliamka usiku mmoja na kuanza kutafakari kuhusu uhusiano wangu na rafiki wa Mr, kwamba itakuaje sasa, ni rahisi kushikwa, tutauendeshaje huu uhusiano na Mr akiwepo? Je naweza kumudu kuwa na wanaume wawili, katika maswali yote niliyojiuliza majibu yakawa ni NO haiwezekani, hivyo nikanuia kuuvunja uhusiano huo haramu

Nikatafuta nafasi nikakaa nae yule mpenzi wangu nikamwambia kwa manufaa ya pande zote mm na wewe basi kila mtu aendelee na familia yake, kwa kweli alilia kama mtoto mdogo, akinikumbatia miguuni, nikasisitiza msimamo wangu na nikaondoka maana watu walianza kutushangaa
Nifupishe tu kwa kusema kwamba, Huyu bwana amegoma kukubali matokeo na kuanza ku behave kama mtoto mdogo hivyo kuhatarisha ndoa yangu, amemchukia mume wangu ghafla na ni kama amegeuka adui, kiasi kuwa juzi Mr ameshangaa sana na kuniuliza kuwa mshikaji tumemkosea nini mbona juzi nimeenda kwake kanichunia, akaondoka na kuniacha sebuleni kwake?
Mr akaniuliza wewe unajua chochote juu ya mabadiliko haya, maana hata simu hapokei, mm nikamjibu sijui chochote

Sasa hivi ameanza kunipigia simu na kunitishia maisha na mambo mengine, nafikiria kumripoti polisi lakini naogopa mambo yakishafika hatua hiyo kila kitu kinaweza kuwa wazi, halaf ndoa yangu ikavurugika

Au niendelee nae hivyo hivyo kwa kificho na umakini?

Naombeni ushauri wenu, maana mm nilitaka kuachana na hili jambo moja kwa moja lakini situation imekua very tense

Kiukweli nilikua na mshikaji kwa kampani tu ila nampenda Mr wangu, hivyo naomba isieleweke kuwa mm ni mhuni, na ni shetani tu ndio alinidanganya nikajikuta nimeanzisha uhusiano huo

Help please

Una karata moja kubwa ya kujaribu, kumweleza ukweli wote mume wako,ukweli wote kabisa.

Kitakachotokea, jamaa atamind na atataka muachane, kwa sababu umekiri mwenyewe beba mizigo au yeye aondoke, baada ya kama mwezi mmoja atakutafuta mtaombana msamaha yataisha, ila uwezekano ni mkubwa mapenzi yasirudi kama zamani.

Ukiamua kudili nalo peke yako bila yeye kufahamu, likelihood ni kubwa kwamba atajua, na akijua kupitia kwingine kokote ndoa hakuna mazima.

Huyo mwanaume wako mwingine tayari hana ndoa, hatakaa afurahie kuona rafiki yake ana ndoa, tena alishajipenyeza kwenye ndoa yenu tayari, kwa hiyo atakuharibia tu ili kama kukosa mkose wote, kisirani cha ndoa yake kitahamia kwenu nyinyi.

Huo ni mchango wangu kwa leo.
 
Kiukweli nilikua na mshikaji kwa kampani tu ila nampenda Mr wangu, hivyo naomba isieleweke kuwa mm ni mhuni, na ni shetani tu ndio alinidanganya nikajikuta nimeanzisha uhusiano huo

Help please
Pendo katika wanaume wote unaowafahamu hukuona hata mmoja isipokuwa best wa mumeo?!!
Huyo shetani aliyekudanganya naona alipiga kambi kabisa kwako maana huo uhusiano wenu una miaka miwili!!
Ndoa ya huyo best wa mumeo unasema inapitia ktk kipindi kigumu,huoni hata wewe una mchango ktk kuongezea ugumu huo?!
Ila now you want to save your marriage!!

Mwisho umesema tusikuchukulie wewe kama ni mhuni, ila tafakari kati ya hawa watu wawili utuambie wewe ni nani.

Definition ya "Mhuni" kuoka ktk Kamusi ya Kiswahili karne ya 21 (LONGHORN) inaeleza:-
1 Mtu mwenye tabia mbaya;mkora
2 Mtu ambaye hajapata kuoa wala kuolewa;mseja
 
Dhambi na usaliti umeishafanya ,sasa kama uko serious acha huo uhusiano hata kama akijiua hiyo ni problem yake kuwa na msimamo na usisahau kupima afya yako kabla ya kumpa mzee chakula chake halali.
 
aise kwa hali ya uchumi wa hii nchi inapoelekea kuna mambo mengi tutajionea hiv nikuulize kitu unakuja kutuomba ushauri kwani wakati unataka kuchepuka ulimuomba nani ushauri Pumba Tupu ndiyo maana hakuna thamani ya ndoa siku hizi aise
 
Back
Top Bottom