Nimesitisha kumuombea Rais

Nimesitisha kumuombea Rais

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
24,145
Reaction score
56,417
Alipochaguliwa tu alitusihi Watanzania wote bila kujali itikadi zetu, makabila yetu na dini zetu tumwombee, kwa kile alichosema alichokikuta kule kilihitaji maombi.

Kweli kama Mtanzania nilianza maombi ya nguvu, nilitenga siku moja ya mwezi kufunga kwa ajili yake nikijua kazi aliyonayo ni ngumu na ya hatari.
Pamoja na kufanya hivyo, leo takriban mwaka unakwisha bila kuona faida ya maombi yangu. Maisha ndiyo yamezidi kuwa magumu afadhali ya mwaka jana.

Katika maombi yangu nilitegemea atakuwa rais wa wanyonge kama alivyoahidi.
Nilitegemea atakuwa rais wa vyama vyote, dini zote na makabila yote kama alivyoahidi. Nilitegemea rais atakuja kuwapata mikopo wanafunzi wote kama alivyoahidi.

Nilitegemea maombi yangu yatambadili na kutawala kwa haki kwa kufuata utawala wa sheria, rule of law. Nimesubiri ahadi yake ya ajira kwa vijana kama alivyoahidi, matokeo yake kaajiri vijana kwa kuangalia ukada na mbaya zaidi kaajiri vijana wenye ukakasi mbele ya jamii.

Matokeo ya maombi yangu ni kusitishwa kwa ajira, kunyanyaswa kwa watumishi wa umma kwa kisingizio cha kuhakiki wafanyakazi hewa.
Maombi yangu yamesababisha wafanyabiashara kunyanyaswa kwa kuongezewa kodi zisizo na ulazima.

Nilitegemea madawa yataongezeka mahospitalini, matokeo yake hata dawa ya chanjo kwa watoto imekosekana. Naona kama maombi yangu yanazidisha ugumu wa maisha kwa wananchi. Kwanini basi niendelee kuomba?

Kama mwaka jana niliishi vizuri, watoto walisoma bila kumwombea rais aliyekuwepo, ajira zilikuwepo wafanyakazi walipanda madaraja bila kumwombea rais aliyekuwepo, wanafunzi walipata mikopo tena wote bila kumwombea rais aliyekuwepo, kuna sababu gani basi kuendelea kumwombea aliyepo?

Nimestisha maombi.

Ni uamuzi wangu sijashinikizwa na mtu.

Quinine.
 
thinking-happy-face-F3DMfC-clipart.jpg
 
Hongera kwa kumuombea kwa muda wote huo! Maombi hudumu miaka kadhaa naamini kwa muda uliomuombea unatosha maana yatadumu mpaka miaka5 itakwisha kwahiyo tegemea ugumu zaidi ktk miaka yote hiyo
 
Mkuu Quinine Nimekupenda bure! Maamuzi yako yanakutoa kwenye laana, ya kuombea vitu batili kwa Mungu, Bora ukaiombea Israel utapata baraka kwa Mungu, kuliko kupoteza muda kumwombea uchwara
Kweli mkuu, nikiendelea kumwombea nitakuwa namimi kama nayabariki mateso ya wananchi.

Watu wanavyolalamika maisha, ajira, wanafunzi wanavyolalamika kukosa masomo, watumishi wanavyofukuzwa hovyo, yote hayo sitaki kushiriki laana kupitia maombi yangu.
 
Back
Top Bottom