Nimesitisha kula nyama kipindi hiki

bushland

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
7,015
4,982
Wakuu habarin za sahizi, jaman kutokana Na hali ya ukame wa sasa Na ukame wa pesa mfukoni nimeona Ni hatari zaidi Kula nyama, Sababu Ni kuwa nyama siku hizi mabuchani haziishi, kila siku nyama zinalala sasa shida inakuja pale unapochanganyiwa nyama iliokaa zaidi ya siku mbili kumbuka mwenye bucha hatokubali Kula hasara

Kitu kingine Ni hii kufa kwa mifugo, kiukweli mifugo inakufa sasa mfugaji nae hawezi kubali Kula hasara, lazima akaongee Na wauza mabucha wapige dili, Na pia naongea haya kutokana Na kuwa nyama nyingi za sasa hivi hazina ladha Ile iliyizoeleka.
Tuwe makini Sana kipindi hiki
 
Wewe nyama ya jana/juzi huijui?,mimi namwambia kata hapa sasa wewe unamwambia nikatie kg 1 nifungie vizuri,kwanini asikuwekee mixer ya jana na leo..
 
Mtu anatakiwa kula nyama Mara 1 kwa wiki

Hongera mkuu umefanya maamuzi mazuri na ya busara na umejali afya yako

Nyama nunua butcher za maana na kama upo Dar nenda star butcher wapo vizuri sana hawachukui nyama hovyo .
 
Nyama inautamu wake, usiache kabisa punguza, nilifanya mapinduzi hayo miaka michache iliyopita, kwa sasa nyama ni weekend tu tena nikipata kuku wa kienyeji na huku kwetu Kwamtogole mchinjaji baadae anatuma mototo na bakuli, etu shingo ya mchinjaji.
 
Kipindi hichi cha magu hata kama ulikuuwa huumwi utajifanya unafwata masharti ya doctor tu
 
mkuu naogopa kuacha kula nyama nywele zangu zisije kuwa ngumu , ndefuu kama wale rasta, asee sijui haziwawashii, na hawajihisi kama wamebeba ndoo ya maji kichwani

√Ndo maana kuku wamepanda bei sababu ya hiyoo
 
Nyama inautamu wake, usiache kabisa punguza, nilifanya mapinduzi hayo miaka michache iliyopita, kwa sasa nyama ni weekend tu tena nikipata kuku wa kienyeji na huku kwetu Kwamtogole mchinjaji baadae anatuma mototo na bakuli, etu shingo ya mchinjaji.
Ngombe nyingi zinakufa kufa hivyo, Kuna uwezekano WA Kula vibudu
 
Wakuu habarin za sahizi, jaman kutokana Na hali ya ukame wa sasa Na ukame wa pesa mfukoni nimeona Ni hatari zaidi Kula nyama, Sababu Ni kuwa nyama siku hizi mabuchani haziishi, kila siku nyama zinalala sasa shida inakuja pale unapochanganyiwa nyama iliokaa zaidi ya siku mbili kumbuka mwenye bucha hatokubali Kula hasara

Kitu kingine Ni hii kufa kwa mifugo, kiukweli mifugo inakufa sasa mfugaji nae hawezi kubali Kula hasara, lazima akaongee Na wauza mabucha wapige dili, Na pia naongea haya kutokana Na kuwa nyama nyingi za sasa hivi hazina ladha Ile iliyizoeleka.
Tuwe makini Sana kipindi hiki
Kula kitimoto awaja athirika na ukame
 
Back
Top Bottom