Vawulence
JF-Expert Member
- Jan 4, 2009
- 1,931
- 2,114
Wakuu habari za mchana na poleni kwa majukumu.
Nimeajiriwa kama mwalimu katika shule moja inayomilikiwa na kanisa. Mnamo tarehe 07/04/2017 mkuu wa shule alitutaka tufike kazini japo ilikuwa ni sikukuu ya kitaifa (Karume day). Nilitoa udhuru kwamba licha ya kuwa ni siku ya mapumziko pia nilikuwa na masuala ya kifamilia niliyopanga kurekebisha siku hiyo.
Baada ya siku hiyo mkuu alikuja akatangaza kuwa anatoa likizo kwa wafanyakazi wote kuanzia tarehe 12/4-23/4/2017 isipokuwa mimi niendelee kufika kazini kama kawaida. Nilitimiza amri yake na kufika shuleni siku zote bila kunung'unika au kulalamika hadi jana shule ilipofunguliwa.
Cha ajabu ni kuwa leo amekuja na kunitaka nikabidhi mali za shule na kunipa barua ya kunisimamisha kazi afanye uchunguzi halafu ataniita kwa utetezi.
Kosa kwenye barua ni hilo la kutofika kazini siku hiyo.
Sina rekodi ya makosa na sijawahi kupewa barua yoyote ya onyo.
Kwa ninavyomjua ni dhahiri kuwa kifuatacho ni barua ya kunifukuza kazi.
Ninaomba ushauri wenu nifanye jambo gani maana naona wazi haki zangu zinaminywa na mkataba wangu unaelekea kumalizika.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushauri mtakaonipatia.