Nimesikitishwa sana na hati ya mashtaka ya utakatishaji fedha kwa ndugu yetu, Mtanzania mwenzetu Tito Magoti

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Mh. Mbowe KUB aliposema taifa lina hitaji maridhiano wakati wa maazimisho ya miaka 58 ya uhuru wa bendera, wapo walio dhani ni maridhiano na CHADEMA!!!

Wengine wakasema kesi imewakalia vibaya ndo maana wanaomba maridhiano, japo haikutumika lugha ya kuomba.

Maridhiano aliyo yasema Mbowe ni kati ya serikali na wananchi. Wananchi wana bambikiwa kesi ambazo zina pora haki ya uhuru wao kwa matashi ya mtawala.

Leo ukimkosoa Rais Magufuli na serikali yake wewe ni mhujumu uchumi, unatakatisha fedha hata kama humiliki fedha.

Jaji mkuu kaona mapungufu ya sheria hii, inayo lalamikiwa na wananchi, kataka yafanyike mabadiliko ya sheria ili kesi zote ziwe na dhamana.

Kwanini hoja ya Jaji mkuu ina mashiko?

MTUHUMIWA hajathibitishwa kuwa guilty mpaka mahakama itakapotoa hukumu, kumzuia dhamana ni kukiuka misingi ya haki za binadamu na kumtia hatiani mtuhumiwa kwa matakwa ya wanasiasa.

Hii haikubaliki, inanyang'anya haki kwa wananchi, lakini ina jenga visasi baina ya raia na raia.

Kukosoa si kosa kwanini tuadhibiwe kwa kukosoa ikiwa mamlaka na madaraka ya serikali yatatoka kwa wananchi kwa mujibu wa ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Kwanini nasema hivi:

Serikali imekuwa ikiwatesa na kuwanyang'anya haki Watanzania kwa sheria kandamizi inayoakisi utawala wa kikoloni.

Ndio maana hoja yangu ya uhuru wa bendera inapojenga mashiko.

Kwa kulijuwa hili kikao cha wazee wastaafu na rais, majaji wakuu wastaafu walionya kuwa sheria yeyote inayo nyang'anya haki za binadamu ni sheria batili na kandamizi.

Leo kila mkosoaji ni mhujumu uchumi, huenda hata nami pia siko salama, maana serikali hii haiambiliki.

Nimesikitishwa sana na charge ya mashitaka ya utakatishaji fedha kwa ndugu yetu, mtanzania mwenzetu Tito Magoti, ila haki huinua taifa.

Uko wapi mhimili wa bunge kama chombo cha uwakilishi wa wananchi, ikiwa kinapitisha sheria za kuwakomoa wanao wawakilisha.

Kwanini serikali inajijengea chuki na wananchi wake kwa sababu zisizo na sababu.

Kwani Rais ni Mungu, hapaswi kukosolewa, kwani serikali ni mamlaka ya Mungu haipaswi kuguswa japo imewekwa kwa dhamana ya wananchi.

Naliona tatizo somewhere, tusipochukua tahadhari ipo siku litatugharimu.
 
Mh. Mbowe KUB aliposema taifa lina hitaji maridhiano wakati wa maazimisho ya miaka 58 ya uhuru wa bendera , wapo walio dhani ni maridhiano na CHADEMA!!!

Wengine wakasema kesi imewakalia vibaya ndo maana wanaomba maridhiano, japo haikutumika lugha ya kuomba!!!!

Maridhiano aliyo yasema Mbowe ni kati ya serikali na wananchi. Wananchi wana bambikiwa kesi ambazo zina pora haki ya uhuru wao kwa matashi ya mtawala.

Leo ukimkosoa Magufuli na serikali yake wewe ni mhujumu uchumi, unatakatisha fedha hata kama humiliki fedha.

Jaji mkuu kaona mapungufu ya sheria hii, inayo lalamikiwa na wananchi, kataka yafanyike mabadiliko ya sheria ili kesi zote ziwe na dhamana.

Kwanini hoja ya Jaji mkuu ina mashiko!?!

#MTUHUMIWA hajathibitishwa kuwa guilty mpaka mahakama itakapotoa hukumu, kumzuia dhamana ni kukiuka misingi ya haki za binadamu na kumtia hatiani mtuhumiwa kwa matakwa ya wanasiasa.

Hii haikubaliki, inanyang'anya haki kwa wananchi, lakini ina jenga visasi baina ya raia na raia.

Kukosoa si kosa kwanini tuadhibiwe kwa kukosoa ikiwa mamlaka na madaraka ya serikali yatatoka kwa wananchi kwa mujibu wa ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Kwanini nasema hivi;

Serikali imekuwa ikiwatesa na kuwanyang'anya haki Watanzania kwa sheria kandamizi inayo akisi utawala wa kikoloni.

Ndiyo maana hoja yangu ya uhuru wa bendera inapojenga mashiko.

Kwa kulijuwa hili kikao cha wazee wastaafu na rais, majaji wakuu wastaafu walionya kuwa sheria yeyote inayo nyang'anya haki za binadamu ni sheria batili na kandamizi.

Leo kila mkosoaji ni mhujumu uchumi, huenda hata nami pia siko salama, maana serikali hii haiambiliki.

Nimesikitishwa Sana na charge ya mashitaka ya utakatishaji fedha kwa ndugu yetu, mtanzania mwenzetu Tito Magoti, ila haki huinua taifa.

Uko wapi mhimili wa bunge kama chombo cha uwakilishi wa wananchi, ikiwa kinapitisha sheria za kuwakomoa wanao wawakilisha!!!

Kwanini serikali inajijengea chuki na wananchi wake kwa sababu zisizo na sababu.

Kwani rais ni Mungu,hapaswi kukosolewa, kwani serikali ni mamlaka ya Mungu haipaswi kuguswa japo imewekwa kwa dhamana ya wananchi!!!

Naliona tatizo somewhere, tusipo chukua tahadhari ipo siku lita tugharimu.

Kuna Wabunge wa Upinzani ni wakosoaji wazuri ila hawana kesi, kwa nini ipo hivyo? Akina Selasini, Prof Jay, Silinde, Cecil Mwambe nk.
Vijana wajitambue, waache kutumika kuleta taharuki kwa maslahi ya wanasiasa.
Mahakama ndio msema kweli hivyo tuziache zifanye kazi kwa Uhuru.
 
Kwahiyo ukosoaji ndio utakatishaji fedha na kumiliki genge/mtandao wa kihalifu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama ndio sehemu sahihi ya kuthibitisha kama ana hatia au la. Kwakuwa unajua kuwa ameonewa, nakushauri uwe sehemu ya ushahidi upande wa utetezi.
 
Watumishi wa Umma wanakuhujumu mchana kweupe sababu wamechoka kudhalilishwa, juhudi zako hazienda kokote. Zaidi ya haya madaraja, hakuna kitakchofanikiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Wabunge wa Upinzani ni wakosoaji wazuri ila hawana kesi, kwa nini ipo hivyo? Akina Selasini, Prof Jay, Silinde, Cecil Mwambe nk.
Vijana wajitambue, waache kutumika kuleta taharuki kwa maslahi ya wanasiasa.
Mahakama ndio msema kweli hivyo tuziache zifanye kazi kwa Uhuru.
Unawambia watu wajitambue kwa mini usijitambue we kwanza,hao uliowataja wengi wanakosoa wakiwa ndani ya binge ambapo wanakuwa na kinga nadhani unajua ni wanasiasa wangapi toka aingie JPM madarakani walio kosoa nje ya bunge kilichowapata.
 
Ni shida sana, ila tujikite kwenye hoja, sijasema Mbowe kaonewa, tujadili bila mihemuko ya kivyama, tutangulize maslahi ya taifa kwanza, hata kama mada zina irritates deeply
 
Pengine sheria ilitungwa kwa nia njema ikiwalenga watu wachache wabaya. Sasa inatumiwa na wanasiasa waliokosa ushawishi na wasiojua maana ya uomgozi wa kisiasa. Sheria hizi kandamizi ni fursa kwa bunge hili la 11 kujitengenezea legacy kwa kufanya marekebisho ya kihistoria. Wabunge wote bila kuangalia vyama amkeni; this is the last chance for you to show your supremacy.
 
Back
Top Bottom