Nimeshikwa pabaya - wakuu naomba msaada tutani!

Deodat

JF-Expert Member
Sep 18, 2008
1,274
272
Mimi niko hapa ughaibuni (nchi kapuni - for security reasons), kama wengi mnavyojua mara nyingi ukiwa huku nje ndugu, jamaa na marafiki kule nyumbani bongo huwa wanaomba kila siku ‘uwavute' nao waje huku (bila kujali si rahisi kihivyo). Mwaka jana rafiki yangu kipenzi (tumesoma pamoja tangu shule ya msingi mpaka chuo kikuu pale mlimani) aliniomba nimsaidie kumfanyia mpango mkewe aje hapa kufanya masters degree, nilijitahidi kwa nguvu zangu zote hata kuingia gharama nyingi na hatimaye shemeji yangu kipenzi akafika hapa.

Hapa tulipo sio mji mkubwa sana, una watu elfu 25 tu na watanzania tuko wachache sana na tunafahamiana kwa kiasi kikubwa. Mara nyingi huwa tunakutana na kupiga soga, kunywa na kula pamoja huku tukikumbushana haya na yale hasa kuhusu nyumbani. Hatuna chama rasmi cha watanzania lakini tunashirikiana vizuri sana na tumekubaliana hatutaanzisha chama kwakuwa mara nyingi mkishakuwa na vyama ndio majungu na ufisadi vinaanza na pia tumekubaliana hatutafungua tawi la nje la chama cha siasa (hasa CCM) labda Chadema tutafikiria.

Stori iko hivi: Katika sisi watanzania tulio hapa kuna jamaa mmoja yeye ni mkongwe hapa, ameeishi kwa miaka saba sasa, ameajiriwa na kitengo kimoja cha serikali kama Strategic Analyst (ana pesa nzuri tu) na ni mtu mkarimu sana kiasi kila mtanzania anayefika hapa huwa anamu-appreciate sana jamaa. Huyu jamaa hana mke, sasa shemeji yangu alipofika nilimtambulisha kwa watanzania wengine akiwepo huyu jamaa, wakazoeana sana, siku za mwanzo nilijua ni kawaida tu lakini baadae niligundua wameanza mahusiano, na kwa hivi sasa napoongea shemeji keshahama hostel anaishi kwa jamaa, wanapika na kupakua.

Hicho kitu kimeniumiza sana hasa ukifikiria ni mke wa rafiki yangu. Kwasababu alijua anachokifanya, shemeji sasa ananionea aibu sana kiasi kwamba hata nikimpigia simu hapokei. Wakati naendelea kutafakari nini cha kufanya, nikapokea simu kutoka kwa huyo rafiki yangu (mwenye mke) akinituhumu kuwa mkewe kampigia simu kuwa mimi nimemtongoza na nataka niwe na mahusiano naye kimapenzi, kwakuwa jamaa anamuamini sana mkewe na anampenda mno, amefedheheshwa sana na taarifa hizo hasa ukizingatia sisi ni marafiki wa siku nyingi, jamaa ameapa ‘kunichinja' siku tukionana. Nimejaribu kumuelewesha jamaa haelewi.

Wandugu nifanyeje?

(Samahani sana kwa kuweka stori ndeeeefu lakini ilibidi nifanye hivi ili issue iwe clear kidogo)
 
Hebu nitumie jina la huyo jamaa anayenimegea mke wangu tafadhali.... Najisikia kuua mtu..... Kumbe mke wangu alinidanganya unamtongoza nikamuamini!

Wanawake bana dah! Nakushukuru eee Mungu wa Mbinguni kwa kuniumba mwanaume. Umeniepusha na vingi likiwemo hili balaa la kukutana na mitarimbo ya ukubwa na sura tofauti.....
 
Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. na siku za mwizi ni arobaioni. mi naamini jamaa takuja kujua ukweli wa kila kitu. we kuwa na subira utashuhudia haya ninayokuambia.
 
Time will tell....
Halafu hii defense mechanism ya kina dada inakera....yaani hata akikulengesha ukachomoa basi anasingizia kutongozwa...:mad2::mad2:
 
Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. na siku za mwizi ni arobaioni. mi naamini jamaa takuja kujua ukweli wa kila kitu. we kuwa na subira utashuhudia haya ninayokuambia.

Asante kwa ushauri.
 
Time will tell....
Halafu hii defense mechanism ya kina dada inakera....yaani hata akikulengesha ukachomoa basi anasingizia kutongozwa...:mad2::mad2:

Yaani kwa hili nawasifu, huwezi amini mumewe mpaka sasa anaamini kabisa anayoambiwa na mkewe. Halafu nahisi walikaa waka-strategize na hili buzi lake, mshikaji ni strategic analyst kwa hiyo sitashangaa kama hiyo atakuwa na amepewa na yeye.
 
Hebu nitumie jina la huyo jamaa anayenimegea mke wangu tafadhali.... Najisikia kuua mtu..... Kumbe mke wangu alinidanganya unamtongoza nikamuamini!

Wanawake bana dah! Nakushukuru eee Mungu wa Mbinguni kwa kuniumba mwanaume. Umeniepusha na vingi likiwemo hili balaa la kukutana na mitarimbo ya ukubwa na sura tofauti.....

Wanaume wa ki-israeli kila siku huwa wana sala yao ya kumshukuru Mungu kwa kuumbwa wanaume.
 
Kila jema hulipwa na jema na kila ovu halikadhalika.
Kama kweli hujatenda naye basi Mungu atakunusuru ndugu yangu.
 
Wandugu nifanyeje? ..

Subiri 'kuchinjwa' tu!:becky::becky:

On a serious note, kwanza pole kwa 'masaibu' unayoyapata. Unadhani inawezekana kwa wewe kuongea na huyo shemejio kuhusu kadhia hii? Kama, jibu ni ndiyo nadhani hapo ndio pa kuanzia. Unaweza kudadisi pia kama ana nia ya kuendelea na mumewe (rafiki yako) au ndo 'keshafika' kwa huyo mpya.
 
Hawana jema!
Mazee,
Huyo rafiki yako mwambie kama ugomvi na iwe ugomvi tu, hamna haja ya kumbembeleza wakati huna makosa. Mwambie huo uliompa ndio ukweli asuke au anyoe, kivyake. Huyo mkewe m-delete kwenye radar zako. Utakufa mapema bure kwa umbwiga wa watu wengine.
 
Umegonga penyewe mkuu...
Hapa nadhan wala asipige simu......aandike email akiweka facts zote...mwisho ampe ultimatum huyu rafiki yake....
Kwa hili huyu rafiki sio wa kulaumiwa....it is a naturala reaction alipopewa taarifa ambazo alitaka zisiwe za kweli!
 
Hebu nitumie jina la huyo jamaa anayenimegea mke wangu tafadhali.... Najisikia kuua mtu..... Kumbe mke wangu alinidanganya unamtongoza nikamuamini!

Wanawake bana dah! Nakushukuru eee Mungu wa Mbinguni kwa kuniumba mwanaume. Umeniepusha na vingi likiwemo hili balaa la kukutana na mitarimbo ya ukubwa na sura tofauti.....

hahahaha kumbe una wivu eeeh mkuki kwa nguluwe
 
Wanawake bana dah! Nakushukuru eee Mungu wa Mbinguni kwa kuniumba mwanaume. Umeniepusha na vingi likiwemo hili balaa la kukutana na mitarimbo ya ukubwa na sura tofauti.....

Lakini unakutana na mashimo ya ukubwa na sura tofauti...
 
Deodat;
Unless story ni ya kutunga, it is very touching!
Ningekushauri pia kisirisiri umpe rafiki yako contacts za simu za watanzania wawili au watatu ; najua sababu shemeji yako, mume wake hayupo kule, watakuwa wameshaji-expose ki-aina to the extent ambayo nina shaka kama kuna mtanzania yeyote asiyejua nini kinaendelea kati ya wawili hao. Awapigie simu na watamweleza aelewe. Hasa ungejaribu kutumia wale wa kike, hasa wale walioko kwenye maisha ya ndoa na wanaishi na waume zao huko
 
Mazee,
Huyo rafiki yako mwambie kama ugomvi na iwe ugomvi tu, hamna haja ya kumbembeleza wakati huna makosa. Mwambie huo uliompa ndio ukweli asuke au anyoe, kivyake. Huyo mkewe m-delete kwenye radar zako. Utakufa mapema bure kwa umbwiga wa watu wengine.
Need I say more?????
 
Back
Top Bottom