Nimerudi tena: Natafuta mke wa kufanana nami

monde arabe

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
8,487
13,018
Habari za leo wana jukwaa,

Miezi michache iliyopita nilileta uzi hapa wenye kichwa cha habari " Natafuta mke mwema"

Tangu kipindi hicho nilipopandisha uzi huo nimegundua kuwa wa2 waliowengi wanatudharau sana sisi tunaotafuta wapenzi kwa njia ya mitandao,wanahisi kuwa sisi ni binadamu wenye kasoro ama za kitabia au kibaiolojia (kama vile abnormal mental fit) ndyo maana hatupati wapenzi huku/huko tutokapo...,kama kuna m2 anazo fikra duni kiasi hicho basi namwomba abadilike, na wale wanaokuja pm na kuleta masikhara pia nawaomba na wao waache!

Nimeamua kurudi tena,naombeni mnisaidie kuonyesha ushirikiano...,mimi ni mwalimu nipo jijini Mwanza na hata huyo partner ninayemtafuta itakuwa vema kama na yeye atakuwa around the lake zone (nahtaji mwanamke wa kabila lolote kasoro mchagga) na awe na sifa zifuatazo;
1.Umri kuanzia miaka 20-27
2.Hata kama atakuwa ni mtumiaji wa pombe basi asiwe mlevi kupindukia (japo mimi situmii alcohol)
3.Awe ni mwenye kujipenda mwenyewe (msafi wa mwili na mavazi), kujiheshimu na kuwaheshimu wazazi wake na ndugu zake
4.Asiwe na magonjwa ya kuambukiza wala ya kurithi(HIV/AIDS, pumu, sickle cell,nk)
5.Awe amemaliza kusoma (asiwe na ndoto za kwenda masomoni tena...,kwa kuwa mwaka uliopita nilihtimu elimu ya juu-Bachelor of education in Arts/Degree ya Elimu na ninapaswa kuwekeza nguvu kwenye familia na huyo mwenzangu badala ya mmoja kati yetu kwenda masomoni)
6.Nitampokea kwa mikono miwili kwa hali yoyote atakayokuwa nayo (haijalishi anaelimu kubwa au ndogo kiasi gani, haijalishi ni masikini au tajiri kiasi gani...nahitaji awe na akili timamu tuuu!)
7.Asiwe amezaa (kama itatokea alizaa na mumewe akafariki basi nitampokea na huyo mtoto nitamuhudumia kama mwanangu wa kumzaa kwa kuwa najua kuna siri watu wengi hawaifahamu kuhusu watoto wa namna hii)
8Awe mtu wa imani yoyote ( japo itakuwa vizuri kama atakuwa ni mkristo)
9.Awe na muonekano wowote (mweupe au mweusi)

Naombeni muungane nami katika hitaji langu wanafamilia wenzangu.

Asanteni sana na Mungu awabariki

Ameen!
 
Mkuu safi

Ningeomba utupe siri ya hao watoto ili nasi tuweze kufaham

Na kwanini wachaga umekataa,naona wengi hawawataki...tupe tusiyoyajua mkuu
 
Mke wa kufanana naye yupo hapo hapo Staff mkuu,ila kama wote Wasukuma Eishhh una haki ya kuja huju.


Wasukuma wana maumbo complicated sana mikono tu mfano kama ya Jokeri .
 
Daah mkuu hutaki mchaga??yaan katika makabila yooote mia ngapi umemtoa mchaga pekeyake.doh
 
UTAMPATA MWANAMKE LAKINI SIO WA KUFANANA NA WEWE-HIVYO VEGOZO ULIVYOWEKA AMBAVYO WEWE HUNA HATA KUWA TENA WA KUFANANA NAWE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom