Nimerudi nimekuta Jirani yangu (Mke wa mtu) kanifulia nguo

Hiyo wenzako tumeshazoea... kipindi nipo chuo (college) nilipanga chumba mtaani basi mambo hayo yamenikumba sana mpaka nikawa nashangaa

1.nimeshabebewa maji sana na wake za watu pamoja na mabinti wa wake za watu. Unakuta nimeacha ndoo bombani niende chuo nikirudi nakuta zimechotwa na zimebebwa

2.wamewahi kupanga zamu za usafi wa chooni lakini akajitokeza mpangaji mmoja mke wa mtu akasema atafanya ikifika zamu yangu kwahiyo mimi wasinisumbue. Hivyo mimi nililetewa tu taarifa na mama mwenye nyumba kwamba tulikuwekea zamu ya usafi kila weekend lakini fulani amesema atakufanyia kwahiyo kama mtaelewana utakuwa unamng'oa ya sabuni (cha ajabu muhusika alikataa akasema nisijali)

3.nguo ndo kabisa nina uvivu basi nikiloweka niseme nifue kesho au baadae nakuta tayari zimefuliwa sasa kuzichukua kwenye kamba naona aibu unakuta zinakusanywa naletewa kabisa

4.kupika ndo kabisaa... mboga za majani tulikuwa tunaona uvivu kununua kwajili ya ishu ya kuchambua tukawa kama tukinunua tunanunua iliyo andaliwA tayari sasa wakawa wakiona vile wanasema tusinunue ile kwakuwa haijaandaliwa vizuri bali tununue hiyohiyo halafu wao watatengeneza
Una nyota ya ndoa nzuri kijana.. ukamwone bro Mshana Jr kwa ushauri zaidi
 
Wakuu ushauri naomba,

Hapa ninapokaa tupo kama watu 12 hivi, sasa nina jirani yangu (Mke na Mme na watoto wawili) wamehamia siku si nyingi. Sasa tuliwakaribisha vizuri nami ninaishi mwenyewe familia iko mbali.

Leo nimerudi, wakati nasalimia nikasikia "samahani jirani, Nguo ulizoanika kwenye kamba zilianguka zikalowana na matope, nimekufulia zote". Katika hizo kuna boxer zangu nne, Taulo mbili na Underwear moja Eti nazo alizifua. Dah...nimeshtuka lakini nikabaki kumshukuru sana...

Mlangoni niliacha rubber zangu asubuhi huwa nafanya jogging kidogo kujiimarisha kiafya. Nimekuta nazo zimeoshwa zinang'aa kweli kuzidi mke wangu anavyooshaga. Yaani nimepata mshtuko sana kiasi nikashindwa kabisa namna ya kushukuru kwa kujishtukia. Nimeingia ndani bado natafakari hili lilotokea ni jambo zuri lakini limepitiliza mno.

Nimepigwa butwaa hata sielewi inakuwaje hii,kutoka nje sasa hivi naogopa najishtukia sana.

Hapa wapendwa nifanyeje maana hili tukio kwangu si la kawaida kufuliwa hadi nguo za ndani na kuoshewa viatu kwangu si la kawaida. Naogopa Mme wake akijua hilo si litaleta sintofahamu wakati mimi kabisa na mawazo yafananayo na urafiki na huyo mke wa mtu??!!!

Je, Ni UPENDO wa kijirani ama ninini?
Je,Mumewe akisikia itakuwaje jamani wooooooohiii Mungu wangu nyieee....Ntaweka wapi sura yangu ikatokea nimehukumiwa kosa ambalo hata mpango wa kulifanya sipo nao????

Msaada wakuu
Kichwa cha chini kimeanza kuwaza kazi yake
 
Shida ni CHUPI yangu au siyo?
Hiyo chupi ni mtumba kutoka wap mkuu?

Uliinunua hapa haoa bongo au uliagiza?

Vipi ukivaa, inazuia nini hasa?

Hiyo chupi ulikuwa umeanika nje ndipo ikadondoka au ulitoa nje ikiwa chafu?

Majibu tafadhali
 
Back
Top Bottom