Nimerudi ghetto nimekuta wameiba kila kitu

Nimerudi ghetto nimekuta wameiba kila kitu

DOCTOR UZI

Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
99
Reaction score
80
Wakuu

Kila janga ni fursa

Moja kwa moja kwenye mada nina geto Dodoma. Lipo ndani ya uzio(ukuta na geti) wapangaji wengi ni wanachuo na baadhi wasio wanachuo, pia mwenye nyumba haishi hapo.

Mnamo tarehe 13/03/2020

Niliondoka nakuingia mjini Daslam na kupelekea kukaa mpaka janga la corona likaingia nchini hivyo sikurudi Dom mpaka wiki iliyopita baada ya kupigiwa simu na manzi mmoja alikuwa anaishi nextdoor (geto la pembeni yangu) kuwa vitu vyake vimeibiwa,kufika na mimi nikakuta yaleyale kwanzia kitanda mpaka nguo walichoacha ni pazia tu na kwa manzi napo hivo hivo. Ukija kwa mama mwenye nyumba jibu lake ni moja “ anakwambia wezi hawana huruma,naomba kodi ya mwezi mmoja uliopita pia” nb kodi iliisha 15/05/2020 so anataka kodi ya kipindi hicho mpaka saivi na niongezee ya miezi mitano mingine.

Update:
Story ni ndefu ila mpaka leo nimefanikiwa kuhama pale nilipoibiwa na kudaka geto lengine nikianza na kitanda, godoro na vitu vya matumizi ya kila siku.

Kodi alinikopesha jamaa angu mmoja hivi ambaye nimepiga nae mishe nyingi sana tulikubaliana mpaka tar 20/06/2020 saa 23:59 (tano usiku ) nitakuwa nishamrudishia hiyo 200k,
F6A82636-38F3-4ADC-9450-A61B1C9BE999.jpeg
mpaka leo nimefanikiwa kupata 100k na jamaa hataki anadai “strictly to the plan”

Nb: Huyu jamaa kabla sijaingia DSM nilikuwa namdai 40k na kipindi chote hicho alinizungusha sana na hadi leo anadai atanipa mimi ni blood wake. Wakuu ushauri.🙏🏿
 
Ni chang'ombe ama maili mbili kama sio m'buyuni...
 
Ghetto ndani ya uzio! Wapangaji wengi! Huyo mwizi vitu kama kitanda kaviibaje?

Halafu alipigiwa simu na jirani, ni jirani ambae nae pia aliibiwa vitu vyote!

Mbaya zaidi kumbe anadaiwa kodi, na hana mkataba halali wa kuishi hapo. Maana kodi yake ilishaisha kitambo. Mwenye nyumba anataka hela fasta hajali na hataki maelezo.

Hahaha... Bongo nyoso.
 
WAKUU
KILA JANGA NI FURSA
MOJA KWA MOJA KWENYE MADA NINA GETO DODOMA. LIPO NDANI YA UZIO(UKUTA NA GETI) WAPANGAJI WENGI NI WANACHUO NA BAADHI WASIO WANACHUO ,PIA MWENYE NYUMBA HAISHI HAPO.
MNAMO TAREHE 13/03/2020
NILIONDOKA NAKUINGIA MJINI DASLAM NA KUPELEKEA KUKAA MPAKA JANGA LA CORONA LIKAINGIA NCHINI HIVYO SIKURUDI DOM MPK WIKI ILIYOPITA BAADA YA KUPIGIWA CMU NA MANZI MMOJA ALIKUWA ANAISHI NEXTDOOR(GETO LA PEMBENI YANGU) KUWA VITU VYAKE VIMEIBIWA,KUFIKA NA MM NIKAKUTA YALEYALE KWANZIA KITANDA MPAKA NGUO WALICHOACHA NI PAZIA TU NA KWA MANZI NAPO HIVO HIVO.UKIJA KWA MAMA MWENYE NYUMBA JIBU LAKE NI MOJA “ ANAKWAMBIA WEZI HAWANA HURUMA,NAOMBA KODI YA MWEZI MMOJA ULIOPITA PIA” NB KODI ILIISHA 15/05/2020 SO ANATAKA KODI YA KIPINDI HICHO MPAKA SAIVI NA NIONGEZEE YA MIEZI MITANO MINGINE.


Usitufokee sasa
 
Ndo maana uwa nikiskia mwiiiiiizi uyooo akidakwa uwa napeleka petrol kwa garama yoyote ile

I hate those fools...
 
Back
Top Bottom