Nimereje tena

Abdallah M. Nassor

JF-Expert Member
Mar 20, 2008
600
620
Ndugu WanaJamii Habarini za Asubuhi na Poleni sana na mambo yanayo-trend mitandaoni kwa sasa.

Nilijiunga na Jamiiforums mwaka 2008 lakini sikuwa active na baadae nikaacha kabisa ku-login. Na sikuwa na mpango kabisa wa kurejea.

Ila kilichonirejesha ni hili la [HASHTAG]#daudibashite[/HASHTAG] kwani ni suala lililovuta hisia zangu nikisubiri maamuzi ya haraka kutoka kwa Mheshimiwa Mkuu wetu wa Nchi lakini hadi sasa ishu kaipotezea na hakuna uwezekano wa siku chache zijazo kuitolea maamuzi.

Nimerudi jamvini kuendelea kuwaunga mkono wale wote tunaotaka kujua ukweli wa sakata hili ambalo hadi sasa lipo midomoni mwa watu na mitandaoni wakati ilitakiwa vyombo husika kama Wizara ya Elimu, Takukuru, TISS, Polisi, na Uhamiaji.

1. Nikianza na Wizara ya Elimu ilitakiwa kutoa majibu ya haraka kuhusu sakata hili kwani ikumbukwe kwamba Wizara kupitia Baraza la Mitihani walitoa tangazo la kuwaomba wananchi kutoa taarifa kwa mtu/watu wanaotumia vyeti feki au vyeti sio vyao kwa msisitizo zaidi wakatoa hadi namba kwa ajili ya mawasiliano ya haraka huku wakiahidi kutunza siri za watoa taarifa. Lakini hili suala la [HASHTAG]#daudibashite[/HASHTAG] hadi sasa wala hakuna cha NECTA au Wizara iliokwisha litolea ufafanuzi.

2. Takukuru kama chombo cha dola chenye jukumu la kufuatilia jinai mbalimbali zinazohusu udanganyifu nayo imekaa kimya kama hili jambo haliwahusu.

3. TISS nayo ikiwa na wajibu wa kuhakikisha tunakuwa na viongozi walifanyiwa VETTING na kuwa na sifa stahiki kushika wadhifa husika nao wamepatwa na ganzi juu ya [HASHTAG]#daudibashite[/HASHTAG] .

4. Polisi nao kama chombo cha dola chenye mamlaka ya kuhakikisha usalama wa raia na mali zao na kuzuia uhalifu bado imekaa kimya kwa tuhuma za kihalifu katika suala la [HASHTAG]#daudibashite[/HASHTAG] .

5. Idara ya Uhamiaji ikiwa ni mdau wa VETTING nao wamekaa kimya pamoja na kuwepo tuhuma kuwa jina [HASHTAG]#bashite[/HASHTAG] lina asili ya nchi jirani (Kagame's) na pia mkewe nae inasemekana pia ni allien.

Hivyo basi wanaJamvi, ukumbi wa Ma-Great Thinkers naomba mnipokee ndugu yenu tuendeleze hizi harakari za kuujua ukweli.

Asanteni kunipokea.
 
Hakuna kitakachoweza kufanyika ktk balile scam kwa sababu ni amri kutoka juu. Kuna msemo like father like son. Tumwombe tu Mungu amfufue saa8 kokote aliko ili aje atupe yake ya moyoni
 
huu uzi uunganishwe kwenye mada za bashite

maana huku ni kujaza seva.
 
Back
Top Bottom