Nimepoteza hamu kwa mke wangu,nifanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimepoteza hamu kwa mke wangu,nifanyaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Attache, Sep 25, 2012.

 1. Attache

  Attache Senior Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 171
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Ni muda mfupi tangu nimuoe mke wangu na tumebahatika kupata mtoto wa kiume mwaka jana. Tatizo ni kuwa,muda huu mke wangu kaongeza mapenzi kwangu ila mimi simpendi tena kama ilivyokua zamani na hata hamu naye imepungua. Sina nyumba ndogo na sijawahi kutoka nje ya ndoa hata mara moja wala sina mwanamke nje anayenichanganya. Hali hii imetokea ghafla na ninadhani bado hajatambua lakini ninawasiwasi atatambua punde kwa sababu hata kumuambia nakupenda imekua vigumu sana nowadays. Je hii ni kawaida katika ndoa na ni kipindi cha mpito? nifanyaje niweze kuondoa hali hii?
  Ninaomba msaada wana jf.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,569
  Trophy Points: 280
  Fanya kila uwezalo ili asijue kwamba huna hamu naye na uendelee kumwambia unampenda hata mara mbili/tatu kwa siku. Haikupunguzii lolote katika kumwambia unampenda kila siku iendayo kwa Mungu...inawezekana labda una mkanganyiko wa akili, kama ni hivyo basi unahitaji msaada wa wataalamu.
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Kazini kuko sawa?
  Familia yako haisumbui?

  Kama hayo yote yako sawa, katambike kidogo.
   
 4. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  vipi kuhusu matarajio yako ya kimaisha?
  unardihika ulipo kazini?
  mkeo unahisi amebadilika umbile alilokuwa nalo mwanzo?
  unahisi mkeo ana attention sana na mtoto kuliko wewe?
  kifedha je unamudu kuprovide kwa familia yako?
  unajiamini uwezo wako wa kijinsia uko poa?
  kuna kitu negative umesikia kuhusu mkeo?
  unahisi mkeo amekudominate kiuchumi,kielimu,kimawasiliano,?
  hebu funguka zaidi kwa mwongozo huo hapo juu!
   
 5. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Aisee unahitaji kusali sana na kuomba Mungu yaani ikatae hiyo hali katika jina la Yesu; nina imani kwa maombi utashiand. Pia tumia mbinu aliyokupa BAK, kwamba ujitahidi usimuoneshe. Jaribu kumuomba au kutengeneza utaratibu wa kusali naye jioni kabla ya kulala. Ni upepo huu, ukipita waweza pita na ndoa yenu; hivyo upunguze nguvu kwa kusali.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,852
  Trophy Points: 280
  mkuu Attache nakupongeza sana kwa kuwa mkweli sana na kutuonyesha uhalisia ambao watu wengi huukataa ama huona kama dhambi kuukiri kwamba wanapita katika hali hiyo.

  kwanza nakutia moyo si jambo la ajabu kwa mtu na mkewe kupotezeana hamu. hali hii hutokana na sababu nyingi sana na nitajaribu kusema chache nyingine wadau wataongezea.

  1) kukinai- kama ambavyo mtu akila menu moja mara nyingi hukinai kadhalika na wapenzi hukinaiana hali hii usipokuwa makini nayo unaweza kujikuta unakwenda kutafuta ladha tofauti nje na ya hapo kwako. ni vyema ukajua hili kisha ukatafuta namna ya kunogesha penzi lako humo ndani.

  2) kuchokana kutokana na kuzoeana kuliko pitiliza- ni wazi kwamba kwenye mapenzi mazoea hayatakiwa hata kidogo. kila siku inabidi wenzi wajitahd kuimprovise mambo mapya ili kutokuzoeana hili litapunguza ile hali ya kuona ni kawaida tu awepo asiwepo.

  3) mapenzi kwa watoto- hali ya kuzaliwa mtoto katika familia huleta furaha kwani ni baraka ya ajabu kati yenu. lakini sasa mapenzi haya yakielekezwa kwa watoto tu yakasahahulika kwa upande wa nyie mnaowaunganisha hao watoto mambo huenda kombo.

  4) matamanio ya life style za wengine- hii ni kutokana na exposure ambayo mmoja wa wapenzi anaipata so kama mmtu ana marafiki ambao life style yao ni aya aina fulan na ukiangalia ya kwako ni tofauti basi automatically utaishia kutokuyapenda maisha yako simply kwasababu unaona hayafanani na yale ambayo unatamani mkeo awe anayafanya yanayosadifu uliyoayaona.

  5) overexpectation especially before joining together. kuna watu wengi ambao enzi za uchumba watakuwa wana over expectation nyingi juu ya wenzi wao sasa wanapokuja kuish maisha halisi hali huwa tete manake anakuta alotarajia sio hivyo hukosa hamu nae kabisa.

  6) pretendence hili husababishwa na maigizo mengi yasiyokuwa ya kweli wakati wa uchumba sasa unapokuja ndania kila mtu anaonekana jinsi alivyo ndipo kuchokana kunapokuja.

  7) kulea- wengi wa akina mama hubadilika maumbo na harufu za mwili wanapokuwa wanalea watoto wadogo sasa kama mkeo amebadilika labda kawa mnene zaid ama ana harufu fulan ama nywele zake ndefu zimekatika katika ama ngozi imekuwa sio nyororo tena ama kifua kimetanuka sana nk


  namna ya kufanya ili kuepukana na hali hii.

  chunguza kwa makini sababua ya wewe kumchoka je ni kwasababu analea, ama upendo kahamishia kwa mtoto nk? ukishajua fanya haya yafuatayo.

  1) yale ambayo ni yake binafsi like usafi, uvaaji nk yarekebisha kwa kumwelekeza kwa upendo. mgharamie nywele ziwe utakavyo na hata ngozi iwe upendavyo.

  2) yale ambayo yanatokana na tabia labda aliigiza sasa badili mid set yako kwamba she is real now and anza kuishughulikia tabia moja baada ya nyingine hadi ziwe kama upendavyo.

  3) kama sababu ni kukinai ama mazoea ama yakufanana na hayo, just try to improvise sio kila siku mlale kitandani siku nyingne tupa godoro chini mlale chini ili tu kuwepo na kaupya fulan humo ndani, pia mshirikishe mubuni njia tofauti ya kupeana mapenzi na mshirikishe kweny kuimprovise.

  ikishindikana kabisa take a vacation mwambie labda aende kijijini kusalimia ama wewe chukua likizo safiri just fofr a weak ili umiss naamin akirudi mambo yatakuwa safi. kamwe usitoke nje ya ndoa yako.

  nakuitia pia snowhoite aje aendelee hapa nilipoishia. ila usiogope tafuta suluhu ya tatizo lako kwa makini. kumbuka kusali daima.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  nimeitika mapema my dear nimempa hints hapo juu achek anafall wapi then tuzungumze zaidi ila umefunguka vizuri sana my dear hapo atujuze zaidi ili tujue tunafanye,mi nimependa pia he is so honest!kitu ambacho wengi wetu kinatushinda sana,kesi yake ni rahisi since ameshagundua tatizo na anakiri udhaifu hivyo ni tahisi sana kumsaidia
  hili la KUSALI nalo la msingi sana tunajisahau sana kuombea ndoa zetu tukiwa pamoja!
   
 8. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  gfsonwin umeichambua vizuri ashindwe mwenyewe sasa. Ila nimempenda kuseek advice kabla hajaharibu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Penelope

  Penelope JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 654
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 80
  Kuna mtu mzima fulani (mwanaume)nlishakaa nae akaniambia katika ndoa sa nyingine hali ya kuchokana ipo na upendo kuhis kupungua kwa mwenzako.I hope hayo ni mapito tu katika ndoa,,cha msingi we ndo unajua kama kweli ulimpenda huyo mama watt wako then she deserve a chance,take your time to find wht is missing.
   
 10. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Ni upepo tu utapita....sina uzoefu na hili maana halijanipata ila nimesoma ushauri wa snowhite mwalimu wangu na gfsonwin my sweeeeeeeeeeeeeeetlooooo umeeenda shule uzingatie. Kipengele cha kusali, Kaunga kakisema vizuri, huyo ni mwanafunzi wangu wa kiroho.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,852
  Trophy Points: 280
  thanks Kaunga, hata mie nimempenda sana kwani kawa muwazi na kasema before anything bad has happened.
  hivi wajua love grows exponentially? na inapofikia climax huwa stationary na baadae huanza kudrop tena. but mara nyingi sana wanawake ndo huwa na uwezo wakuifanya i peak tena sasa kama mkewe sio mtu mwenye exposure sana anaweza kuishia kuona kama anasalitiwa ama maisha hayampendi tena.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,852
  Trophy Points: 280
  my swtlo mzima weye?
   
 13. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Kemea kabisa, pepo vunja ndoa linakunyemelea. Ikabidhi ndoa yako mikononi mwa Mungu.
   
 14. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  mzima sana sweetlo, juhudi zako za mtori na uji wa ulezi....aaaah mi wala sina wasi wasi...lol....hebu kujapande zile
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  pole,

  hauna stress?

  Badilisheni mazingira, tafuteni waga mpya, na usali kuombea ndoa yako
   
 16. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #16
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  mimi ndoa nazi:yo:, maana kila leo, aheri ya jana! kila nikiingia MMU nakutana na kisa kizito zaidi ya kingine! TUSISAHAU KUSALI!
   
 17. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #17
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  mke mwenza, nimekumisss sana ujue!
   
 18. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #18
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,322
  Likes Received: 2,301
  Trophy Points: 280
  Kweli dunia ni duara.......lakini nimekumbuka roho ziko nyingi hakika.
  Back to the topic: Sina uzoefu wa ndani lakini kwa kusikia na kuona.....mleta sredi amefanya timing nzuri sana kuona tatizo mapema.............ukimjibu hayo maswali hapo juu aliyokuuliza snowhite tunaweza pata njia maana nia ipo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #19
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,322
  Likes Received: 2,301
  Trophy Points: 280
  Ndoa nazi ndiyo nini hicho
   
 20. Elijah

  Elijah JF-Expert Member

  #20
  Sep 25, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 1,671
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mtafutie mtu mwingine wa kumliwaza,au mlete kwangu
   
Loading...