Nimepoteza Amani na hamu ya chakula, naombeni msaada

jjs2017

JF-Expert Member
May 25, 2019
2,023
4,213
Ndugu zangu..

Habari za wakati huu


Mimi kijana wenu umri miaka 30+, sijaona na wala sina mpenzi maalumu wa kuja kunipikia hata mara mojamoja,

Nimekua kijana mtiifu sana wa kula katika magenge tofauti tofauti yanayo uza chakula, ila baada ya kushuhudia yanayoendelea huko kama kushikikiwa mboga na mikono sometime, kuonjewa mboga na vidole una kuta mtu kashika pua mara uchafu mara kaosha mtoto alafu anaweka vidole kwenye chakula ukijipindua tuu kuangalia pembeni

Kadhaa ya vyombo kuwa na harufu ya sabuni, vyombo kutokuosha na maji safi, mazingira ya kutatanisha ninayo kutana nayo kwenye hayo magenge na vioksi vya chakula,

Nimejaribu kula kweye mahoteli mbali mbali ila garama ya huko nikubwa sana na chakula ni kidogo mno.

Nikaona kuliko kuteseka, kupoteza hela nyingi sana pamoja na kula vyakula vichafu nakupata wasiwasi na hofu moyoni acha nianze kujipikia mwenyewe rasmi.

Ndugu zangu baada ya kuanza kujipikia kwa siku nne mfululizo nimejikuta, nimekumbwa na kadhia yakupoteza hamu ya chakula kabisa pale ninapo maliza kujipikia na sijui inasababishwa na nini, wakati mwingine nikimaliza kupika na hisi nimeshiba nakubaki kukiangalia chakula nilichopika na kuishia tuu kuwapa mifugo.

Kijana wenu najishangaa sana nikisema nikale njiani napata hamu ya kula ila sio kwa kupika, kuna kipindi nilipika nikashindwa kabisa kula ikabidi nigawe chakula kwa jirani na mimi kwenda kula njiani kwa kweli nimekuwa nikiteseka sana.

Ndugu zangu nifanyeje mimi ili niweze kula kwa amani ikizingatiwa nipo single , siwezi kukaa na njaa kwani nikijaribu kukaa na njaa na dhohofika sana, na bado sijapata mwanamke wa kueleweka kuwa mke wangu


Nishaurini wakubwa na wadogo zangu nifanyeje ili niweze kuwa na amani ninapo hitaji kula pamoja nakupata hamu ya chakula nikijipikia mwenyewe.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
1.hakikisha unapika mwenyewe
2. Fanya mazoezi asubuhi na jioni
3. Tumia bangi hakikisha unakula high grade ama skanka, ukila kushabu utadata.
Ni hayo tu kwa leo
 
Back
Top Bottom